Unafiki huu mpaka lini? Kila Zuri sifa Rais, Umeme ukikosekana lawama kwa Waziri

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,758
71,136
Huu mwenendo hautusaidii Watanzania. Na umeletwa na CCM kwa sababu zao za kutaka fikra ziwe kwenye uchaguzi tuu.

Inakuwaje kila jambo jema linalofanywa na Serikali hii ya CCM sifa anapewa Rais na hasa mambo haya yalianzia kwa Magufuli na sasa yameota mizizi.

Lakini Serikali hiyo hiyo inaposhindwa jambo mfano hili janga la Umeme sasa hivi husikii akitajwa Rais Samia wala Serikali ya CCM bali January Makamba.

Au mambo ya Wamachinga, ukosefu wa maji Dar, kushindwa kwenye michezo, ukosefu wa ajira nk Rais hahusishwi kabisa bali yeye wanasubiri avae gwanda la Jeshi basi maccm yote yanalundikana kumsifu tuu.

Huu unafiki utatufikisha wapi? Jee hawajui kuwa kuficha donda ni kulifanya liwe donda ndugu?
 
Arusha,Morogoro,Mwanza,Tabora,Kahama,Singida Leo hii Hakuna Umeme
na Jitu linaingia Wizarani na Michuki kwa JPM Mtu hatunae tena
Tanesco Inarudi Nyuma Miaka 10 Kutoka sasa
Inakera sana
 
Back
Top Bottom