#COVID19 Unafanyia kazi nyumbani? Madokezo haya yanaweza kukusaidia katika kufanikisha majukumu yako

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Kwa watu wengi kufanya kazi wakiwa nyumbani ni uzoefu mpya na wasichojua ni kuwa inahitaji nidhamu ya juu kumaliza kazi na kupata matokeo chanya. Fanya haya ili uweze kupata matokeo chanya.

1. KUWA NA SEHEMU MAALUM YA KUFANYIA KAZI
Sio kila mtu ana chumba cha kujisomea au ofisi ya nyumbani. Ila sehemu yoyote ambayo ni rahisi kwako unaweza kuifanya ndio 'Kituo cha Kazi', sehemu hiyo itakupa ari ya kazi. Ukiwa sehemu hiyo itasaidia pia wengine kuelewa kuwa hauuhitaji usumbufu.

2. TENGENEZA SEHEMU YAKO YA KAZI KUWA KAMA YA OFISINI
Ili kutengeneza mazigira kama ya ofisini na usijione mpweke, unaweza kutengeneza sehemu moja ambapo wewe na mweza wako mtaitumia kama ofisi lakini pia watoto watatumia kama sehemu ya kusomea. Kuwa na kila mmoja sehemu hiyo kutakufanya uone mnafanya kazi kwa pamoja.

3. WEKEZA KATIKA MTANDAO NA ZANA ZA MAWASILIANO
Kufanya kazi kutoka nyumbani, haswa wakati huu, inamaanisha kuwa hauwezi kuongea na wenzako uso kwa uso. Hata hivyo, unaweza kuwasiliana na wenzako na ulimwengu wote kupitia njia mbalimbali za mtandaoni. Lakini pia unahitaji muda wa maongezi wa kutosha kwenye simu yako.

4. ANZISHA UTARATIBU NA JIJENGEE MAZINGIRA YA KAZI AKILINI
Uzuri wa kufanyua kazi nyumbani sio lazima undane na ratibu ya ofisini kuwa ni kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Tengeneza utaratibu utakaoendana na mazingira ya nyumbani. Utaratibu bora unatakiwa kukuwezesha kufikia malengo mengi iwezekananyo katika muda mfupi.

5. FUATILIA MAENDELEO YAKO KWA ORODHA YA VITU VYA KUFANYA
Orodhesha majukumu unayotaka kufanyia kazi, yakiwemo yale madogo madogo kama kupiga simu. Kama sehemu uliyopo kuna usumbufu unaweza kuisha kutofanya chochote zaidi ya kuongea na nduguzo. Hakuna ubaya kuongea na nduguzo ila unaweza kuongea nao huku ukiwa hata unafua na kusaidia kutopoteza muda bure.

6. TUMIA KANUNI YA 20-20-20
Kuangalia Kompyuta au simu kwa muda mrefu kuna athari mbaya kwa macho yako, mwanga unaotoka kwenye vifaa hivyo husababisha kavu ya macho. Ukiwa ofisini, muda wa chai na mikutano husaidi kutoangalia kompyuta kwa muda mrefu. Kanuni inasema "Kwa kila dakika 20 unazotumia kuangalia Kompyuta, angalia kitu kingine kilichopo umbali wa Futi 20 (Mita6) kwa sekunde 20".

7. USIOGOPE KUWASILIANA ZAIDI NA WENZAKO
Mawasiliano ya mara kwa mara ni muhimu wakati wa kuratibu majukumu kwa mbali. Utahitaji kusasisha kila mmoja zaidi kuliko vile ungefanya kwa siku ya kawaida kwa kila kitu kuendeshwa vizuri.

Kuweka simu isitoe mlio au kuwa kwenye vibration na kushindwa kupitia barua pepe zako mara kwa mara kunaweza kuzuia wewe kuwasiliana na wenzako mara kwa mara, fanya bidii ya kuwasiliana na wenzako mara kwa mara na kuwepo muda wowote iwapo chochote kitatokea

Ikiwa wenzako wengine wanaotumia makundi ya WhatsApp na Telegram kama mabaraza makuu ya mawasiliano, wewe kukaa kimya kwenye makundi hayo ni sawa na kutokuonekana kazini.

8. ANZA KUFANYA MAZOEZI
Kwa kuwa utakuwa unakaa sehemu moja muda mrefu inamana mazoezi ya mwili yataanza kupungua, mfano unaweza kuwa na ugumu kwenye magoti na maumivu ya mgongo ikiwa kiti unachotumia sio vizuri, unaweza pia kupata maumivu ya shingo.

9. WAZAWADIE WATOTO KWA SHUGHULI ZAO NA NIDHAMU
Kama unavyohitaji kuendelea kufanya kazi, watoto pia hawawezi kupuuza masomo yao. Wapangie ratiba kuonesha wazi muda wa kufanya kazi na wa kupumzika. Tafuta namna ya kuwapa zawadi wakifuata maagizo. Tumia muda huu kuwafundisha kuzingatia muda

Pia soma > Mwongozo wa kufanyia kazi Nyumbani wakati huu wa Mlipuko wa Corona - JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom