Unafanyaje unapogundua ulipewa urithi na mzazi mlezi ila familia ilificha usijue

Oct 16, 2016
34
10
Habari zenu wadau

Niende moja kwa moja kwenye hoja miye nilizaliwa na mama yangu ila nikiwa bado mdogo wa miezi miwili baba yangu mzazi akafariki uyu baba yangu mzazi hakuwa na ndoa na mama

Kwaiyo mama alipata mwanaume mwingine badae ambaye nilimwita baba baba kwakua tulikuwa tunaishi nyumba za kupanga ile kuhama huku mala Kule basi mitaa mipya tuliohamia walijuaga uyu baba ni baba yangu mzazi kitu ambacho si kweli ila uyo baba alinipenda na alinilea kiukweli mpaka napata ufahamu wangu nilimwita baba ingawa yeye alikuwa na mji wake mke wake na watoto wake ambao ni wakubwa zaidi yangu

Miaka imeenda kipindi umefikia umri wa kwenda shule nikaja chukuliwa na shangazi zangu upande wa baba yangu mzazi lakini kipindi niliporudi msalimia mama kijijini nilimkuta yule baba mlezi
Kwaiyo maisha yalienda hivyo mpaka miye namaliza elimu ya msingi, secondary niko kwa shangazi zangu nikapataga tarifa yule baba mlezi Kule jijini amefariki basi maisha yakaendelea hivyo hivyo

Sasa juzi nimeenda jijini msalimia mama, nimeshangaa wazee wakijiji wakiwa na mwenyekiti wa mtaa pamoja na mtendaji wananiambia bora nimefika naitajika mahakama ya mwanzo ile familia ya baba wangu wakufikia ina niitaji tukagawane mirathi nikasema hiyo mirathi mbona hainihusu wakatoa wosia wa marehemu baba wa kufikia ukionyesha kuwa baazi ya Mali endapo akifa nipewe miye

Kiukweli hii suala limenichanganya sana kuanzia miye mpaka mama mzazi sema mama mzazi umri umeenda sana na kinachonichanganya uyu baba mlezi kafariki zaidi ya miaka 25 iliyopita, na nilishaga msahau kabisa

Je hapo unafanyaje maana uyu mzee siyo baba yangu mzazi, tachukuaje Mali isiyo ni husu

Ushauri wenu muhimu sana.
 
Chukua marehemu si ndio aliamua wasi wasi wako nini chukua chako mkafurahie maisha na bi mkubwa wako
 
Mtu anaruhusiwa kutoa mirathi kwa mtu/watu/taasisi. As long as mirathi hiyo haizidi robo ya mali zake zote na hiyo robotatu ndo iende kwa wanafamilia wake.
 
hapo kwa mfumo wa kisecular una haki ya kurithi, na hata kwa sharia za kiislamu una haki ya kurithi hadi 1/3 ya mali ya marehemu kwa kadri mwenyewe marehemu alivyotaka , kwasababu kakutambua kwenye wosia, hilo ni jambo zito.

na kwa sharia mtu asiye ndugu anaweza kurithi hadi 1/3 ya mali kama ikiwa imeoanishwa kwenye wosia ila tu isizidi hiyo 1/3.

watu wenye undugu wa damu wa marehemu wana haki ya 2/3 ya mali za marehemu kama urithi wao iwapo kuna wosia,

pia wana haki ya 100% kama hakuna mke ama mume wa ndoa na hakuna wosia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wadau

Niende moja kwa moja kwenye hoja miye nilizaliwa na mama yangu ila nikiwa bado mdogo wa miezi miwili baba yangu mzazi akafariki uyu baba yangu mzazi hakuwa na ndoa na mama

Kwaiyo mama alipata mwanaume mwingine badae ambaye nilimwita baba baba kwakua tulikuwa tunaishi nyumba za kupanga ile kuhama huku mala Kule basi mitaa mipya tuliohamia walijuaga uyu baba ni baba yangu mzazi kitu ambacho si kweli ila uyo baba alinipenda na alinilea kiukweli mpaka napata ufahamu wangu nilimwita baba ingawa yeye alikuwa na mji wake mke wake na watoto wake ambao ni wakubwa zaidi yangu

Miaka imeenda kipindi umefikia umri wa kwenda shule nikaja chukuliwa na shangazi zangu upande wa baba yangu mzazi lakini kipindi niliporudi msalimia mama kijijini nilimkuta yule baba mlezi
Kwaiyo maisha yalienda hivyo mpaka miye namaliza elimu ya msingi, secondary niko kwa shangazi zangu nikapataga tarifa yule baba mlezi Kule jijini amefariki basi maisha yakaendelea hivyo hivyo

Sasa juzi nimeenda jijini msalimia mama, nimeshangaa wazee wakijiji wakiwa na mwenyekiti wa mtaa pamoja na mtendaji wananiambia bora nimefika naitajika mahakama ya mwanzo ile familia ya baba wangu wakufikia ina niitaji tukagawane mirathi nikasema hiyo mirathi mbona hainihusu wakatoa wosia wa marehemu baba wa kufikia ukionyesha kuwa baazi ya Mali endapo akifa nipewe miye

Kiukweli hii suala limenichanganya sana kuanzia miye mpaka mama mzazi sema mama mzazi umri umeenda sana na kinachonichanganya uyu baba mlezi kafariki zaidi ya miaka 25 iliyopita, na nilishaga msahau kabisa

Je hapo unafanyaje maana uyu mzee siyo baba yangu mzazi, tachukuaje Mali isiyo ni husu

Ushauri wenu muhimu sana.
Unaonekana na wasiwasi sana aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasubiri kuona Majembe majembe akijibu hoja kwa hoja kwa Kila comment maana majibu ya msingi ya Nini kufanya yanatokana na comment za wadau hapo juu na Tena Kuna baadhi ya taarifa jamaa ajaweka sawa Sasa kupitia kujibu comment Mambo yote yatakua open

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mimi ni wewe na muislam kama mie basi ningechukuwa huo urithi. Lakini ningeutolea sadakatul jaria kwa ajili yake(baba mlezi)3/4 na 1/4 ilobakia kwa ajili ya mama na wewe.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Nasubiri kuona Majembe majembe akijibu hoja kwa hoja kwa Kila comment maana majibu ya msingi ya Nini kufanya yanatokana na comment za wadau hapo juu na Tena Kuna baadhi ya taarifa jamaa ajaweka saw
Inaonekana alichokuachia hakileti pesa ndio maana una mashaka.

Komenti tayari
Hapana kilichoachwa kinathamani ya pesa tena pesa mzuri tu hofu yangu katika Mali alizoacha marehemu zote ndugu na jamaa wamezimaliza kilichobaki ni hiki ambacho inaitajika nipatiwe na kimebaki sababu documents ambazo walitajika hazionyeshi kama wao ndio wahusika hata walipoenda mahakamani kubadilisha walitajika kupeleka mitahasari ya vikao vya familia vikionyesha kuwa kuna mabadiliko kwakua marehemu aliamua hivyo baadhi ya wanafamilia waligomea suala hilo na kilichopelekea miye kujua hilo suala ni migongano na malumbano baina yao wana familia walipoitaji kuuza hiyo mali, nakuzidiana ujanja ndipo wakapelekana mahakamani hapo ndio mambo yakaibuka kuwa wanachoitaji kukiuza hakiwahusu wao hivyo gawana haki
 
Miaka 25 tangu afariki. Wewe ni muhenga mkuu na bado hujaoa. Kwann muda wote huo hukwenda kumsalimia bi mkubwa
 
Back
Top Bottom