Unafanyaje ukifumania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafanyaje ukifumania?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bishanga, Aug 23, 2009.

 1. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Hii ni real story:Una ka small house,unakagharimia kila kitu kodi,chakula,umeme,maji mpaka usalama umemwekea Knight Support na biashara nzuri tu umemfungulia na gari juu(Harrier). Huyo bi mdogo anakutambulisha kwa kivulana kwamba ni cousin wake,kila kukicha yuko naye kwenye gari (dogo dereva) na mtoto anadai hicho kivulana kinamsaidia shughuli zake za biashara(ambayo umemfungulia wewe na unai support).Dubai, Guanzou,Hongkong anasafiri nako eti kanamsaidia shopping huko. Tufupishe story.Siku ya siku kwa kuwa una ufunguo wa small house unakuja bila kutarajiwa (si kwako bwana?) unafungua mlango wa mbele,kuingia ndani unasikia funny sounds,kufungua mlango wa bedroom(ambao kwa kujiamini wameacha wazi) unakuta dogo kaning'inia juu ya mamie,na kibaya zaidi bi mdogo anatoa kilio ambacho katu hujawahi kukisikia pamoja na 'ujuzi'wako! Mdau unafanyeje? Kumbuka wewe katika jamii unaitwa 'baba wa heshima' mwenye familia imara na kanisani wewe ni 'mzee wa kanisa'( kanisani una kiti maalum front bench).
   
 2. Violet

  Violet Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lol! Nyumba ndogo always zina vijumba vidogo pia, hawi wako peke yako. Inategemea anampenda kiasi kipi, angeweza kumwacha tuu aendelee na kakijana kake, kama bado anataka kuchomolewa basi baadae aongee naye amsikie bibie atasemaje
   
 3. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Violet,katika purukushani kidogo iliyotokea babu anasema dogo alikuwa peku peku! (actually mzee alipigwa kata funua akabaki chali hoi)
   
 4. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,185
  Trophy Points: 280
  mtu unasmall house ya nini sasa?si usingeoa?hivi kwa akili zenu mnafikiri small houses zinawapenda?ziko pale kwa kuchuma tu.
   
 5. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Tunatafuta kuliwazwa mama baada ya kazi nzito za 'ujenzi wa Taifa'. Si unajua nyumbani kina Mama Chakubimbi kazi masimango tu,tunachoka ati!
   
 6. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,185
  Trophy Points: 280
  sasa hayo ndo malipo ya kuliwazwa,inawezekana big house inakusimanga coz of ufataki wako.Tulia uone kama utasimangwa
   
 7. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kama uliweza kumfanyia yote hayo kwanini usioe kabisa ili kuweka mambo bayana
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Yes.Unavuna uliyoyapanda,na yale umtendeayo mwenzio ndo na wewe yanakukuta.
  Tena shukuru malipo unayapata kwa hiyo nyumba ndogo na huyo bibie wa nyumba kubwa bado anakuheshimu hajakutenda kama wewe unavofanya.
   
 9. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  HM ndoa ya mzee ni ya kikristu,ujanja huo hawezi kufanya.
   
 10. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Lazima uelewe kwamba hii nyumba ndogo na yenyewe inataka baadae iwe nyumba kubwa so mwache dogo aendelee kukandamiza na kama vp kubali we ndo uwe mwizi.Ukifanya hvyo wala hautaona au kusikia pressure ina panda au kushuka!
   
 11. t

  theoinreading New Member

  #11
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 23, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo inaitwa gusa unase, mkome msirudie kuiba Mke mmoja Mume mmoja Full Stop
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...na ukimfumania mkeo je?
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mzee wa kanisa, una familia, mzee wa heshma halafu nyumba ndogo?!!- ngoja ntarudi baadae kidogo.
   
 14. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kila kitu kibaya malipo yake huwa ni hivyo hivyo suppose hizo pesa ungewasaidia watoto wako na familia yako badala ya hiyo hema. Lakini unaweza kuta hata watoto wake wa kuzaa wanaishi maisha magumu pesa inaishia kwa bi mdogo. What goes around comes around.
   
 15. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  what goes around comes around
   
 16. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mambo kama haya ndiyo yanayonitisha katika suala zima la kuoa
   
 17. D

  Dawson Member

  #17
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huku kwetu kila nyumba yoyote kubwa kwa kawaida inakuwa na nyumba ndogo pembeni ambayo ni CHOO kama unajua una nyumba ndogo elewa hiyo ni choo harufu na hadha yake yakubidi kuivumilia, Mwenye sikio na asikie
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ndio maana UKIMWI huwachukua kwa wingi wanafiki kama hawa.
   
 19. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Binafsi siamini msemo wa "what goes around comes around"! Huu msemo unanikumbusha falsafa ya Karl Marx na religion. Misemo mingine imetungwa kuwaogopesha watu tu.

  Binafsi naamini nyumba ndogo (both za kiume na za kike) zinasaidia sana katika ku manage na kupunguza stress and depression. Bila nyumba ndogo wanaume kwa wanawake tungekuwa tunakufa au kuparalyze kila leo mamia kwa maelfu kutokana na kero za ndoa. Na kwa wenzangu wakristo mke mmoja mpaka kifo kiwatenganishe, ndo balaa!! Kina mama vitulizo vyao wanaume wa nje na sie kina baba vitulizo vyetu mabibi wa nje.

  Tusidanganyane wadau, ni muda, style na mazingira tu ndo yanatofautiana, lakini mchezo ni ule ule. (rejea Marxist theories)

  Kuhusu cost incurred kwenye hizo nyumba ndogo, mi naona ni justifiable given madhala na mudhi ya nyumba kubwa!! Besides starehe gharama ndugu zangu!!!
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapo Bishanga huyo dogo hana kosa kabisaaaaaaa mwenye kosa hapo ni huyo small house kwa kutokuwa mwaminifu hapo hapo ningekuwa mimi hapo namruhusu huyo dogo avae aondoke salama kisha na deal na huyu small house naita fusso naita dereva napakia kila kilicho changu namwacha simpigi wala sifanyi nini kisha nasepa namwacha kwa amani lakini vyangu vyote nachukua na duka kule nafunga nazoa vyangu vyote basi biashara inakwisha.
   
Loading...