Unafanyaje kuimarisha kinga ya mwili kipindi hiki cha mlipuko wa COVID-19?

Status
Not open for further replies.
Kwa africa tujitahidi na Duaa nyingi, Malimao, Tangawizi, Vitunguu haswa swaum, Maparachichi, Ndizi mbivu, Dandelion, mandarin nk...

The Pandemic is on its way to your Motherland! Take care
 
Jagi la juice ya mlonge asubuhi

Mchana jagi la juice ya alovera

Usiku jagi la juice ya mwarobaini.

Corona akiipangua hii combination nitakata rufaa kwa israeli
Mimi namix zote hizo mpwaa sitakishidaa yaani chooni vinatoka vitu vinatembea kama vilikuww vinasubiri ninywe balaa
 
1586930978166.png


ULAJI wa mlo kamili zikiwemo mbogamboga, matunda na maji kwa wingi, imelezwa kuwa ni miongoni mwa virutubisho vinavyoongeza kinga ya mwili katika kupambana na virusi vya corona. Aidha, imetolewa angalizo kwa jamii kuepuka upotoshaji unaoenezwa kwamba kujifukiza ni moja ya tiba ya virusi vya corona, akisema njia hiyo sio sahihi kwa sababu inaweza kuleta athari ya kuunguza njia ya hewa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Programu wa Elimu ya Afya kwa Umma katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Tumaini Haonga amesema mlo kamili na unywaji maji kwa wingi, vinasaidia kujenga kinga imara zitakazoweza kukabiliana na virusi hivyo, vinavyosababisha homa kali ya mapafu (Covid-19). “Katika kipindi hiki cha mlipuko ni muhimu kuzingatia lishe sahihi yaani ulaji wa chakula ambacho ni mlo kamili.

Mtu mwenye hali nzuri ya lishe ana uwezekano mkubwa wa kuwa na kinga imara ya mwili na hivyo mwili wake utaweza kupambana na vimelea vya magonjwa ikiwemo virusi vya corona kwa kiwango kikubwa zaidi ukilinganisha na wengine,” alisema Dk Haonga. Alisema mlo kamili ni chakula chenye virutubisho vyote muhimu ikiwemo wanga, protini, mafuta kiasi, madini joto, vitamini, mbogamboga na maji ya kutosha mara kwa mara. “Tunapoangalia mlo kamili tuangalie mchanganyiko wa vyakula kulingana na upatikanaji na uwezo wa mtu kuendelea kuvipata, mboga za majani aina zote, matunda na maji kwa wingi ni muhimu sana katika kipindi hiki,” alifafanua daktari huyo.

Dk Haonga alisema ulaji wa kiwango cha juu cha virutubishi fulani, huimarisha mfumo wa kinga, huku ulaji wa kiwango cha chini ukidhoofisha kinga na kuvutia maradhi ya maambukizi. “Kinga imara mwilini inaweza kusaidia kukabiliana na virusi, na pia inaweza kuwasaidia baadhi ya wagonjwa kupona kwa haraka,” alisisitiza. Alitaja virutubisho vinavyoweza kuimarisha kinga ya mwilini ni kama vile madini ya zinki, iron na vitamin A, C, D, E, B-6, vyakula kama vile kabichi, broccoli, mchicha, chai ya kijani, samaki, maharage, uyoga, viazi vitamu na matunda kama tufaa, mananasi, maembe na machungwa, machenza na mengineo.

Alisema vyakula hivyo ni muhimu katika kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa ya milipuko. Baadhi ya madaktari walisema matunda kama vile machungwa, yana vitamin C nyingi ambayo ina uwezo wa kukabiliana na magonjwa. Pia virutubisho hivyo vinasaidia kuzuia uvimbe kupitia kiasi na uharibifu wa tishu, unaosababishwa na virusi hivyo, ambao unaweza kusababisha majeraha ya mapafu na hata kifo. Aidha, Dk Haonga alisema vyakula hivyo vinaweza kuwa muhimu kwa watu wazima, ambao wako hatarini zaidi kuambukizwa maradhi ya Covid-19.

Alisema uzoefu kutokana na milipuko mingine ya magonjwa ya maambukizi, unaonesha wazi kwamba watu wanaokula lishe duni wako hatarini zaidi kuambukizwa virusi hivi. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya hadi juzi mambukizi mapya ni 17, waliopona na kuruhusiwa ni saba, vifo vitatu hivyo kufanya mambukizi kufikia 49. Pia takwimu hizo zinaonesha wanaofuatiliwa kubaini kama wameambukizwa au la ni 590, waliomaliza ufuatiliaji ni 413 na wasafiri waliopo kwenye karantini ni 84. Maeneo ambayo ugonjwa huo umeripotiwa nchini ni Dar es Salaam (wagonjwa 32), Zanzibar (12), Arusha (3), Kagera (1) na Mwanza (1).
 
Protini huimarisha kinga ya mwili, si lazima iwe nyama. Jamii ya kunde, karanga, korosho, ni muhimu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom