Unafanya nini Mtandaoni?

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,265
2,000
Tunaishi zama za TEHAMA

Naamini kabisa unaposoma andiko hili unatumia kifaa cha tehama na unatumia bando hata kama hujalilipia ili uweze kuisoma hii taarifa.

Mwaka 2000 wakati bado teknolojia ni changa nilwahi kumwambia rafiki yangu mmoja juu ya maono yangu kuhusu teknolojia. Kipindi hicho ilikuwa ni zama PENTIUM, na Floppy DISK na CD-R na CD-RW ilikuwa ni kipindi cha Internet Cafe.

Teknolojia ilikuwa juu na simu za mkononi zailikuwepo pia. Hata hivyo kiwango cha teknolojia cha kipindi hicho hakilingani na kipindi cha sasa na wa la hakitafanani na aina ya teknolojia ambayo inakuja.

Nilimwambia kwamba kwa jinsi teknolojia inavokua kwa kasi basi kuna siku itafika ambapo mtu atakaa kwenye kiti ndani ya eneo la mita moja na mraba na ataingiza mabilioni ya pesa bila kusogea wala kwenda POPOTE.

Ilikuwa ni zaidi ya miaka 20 iliyopita teknolojia ilikuwa ya kawaida na maisha yalikuwa ya kawaida. Mwaka 2011 nilianzisha ofisi yangu ya kwanza ya nyumbani nikitumia internet ya sasatel, computer DELL huku nikitoa huduma ndogondogo tu kwa watu wachache nikiwa na PRINTER ya HP.

Mpaka kufikia mwaka 2016 ofisi yangu ya nyumbani ilikuwa inaniingizia kipato kidogo lakini niliendelea kupambana hivo.

Nimejifunza kuhusu blogging, adsense, adwords, webdevelopment, android development, fore trading, software development Katika kipindi cha miaka 7+.

Vilevile nimejifunza elimu mbalimbali za aina tofauti katika fani na nyanja tofauti kwa kadiri nilivopata muda na uwezo. Kwa wastani nimefikia hatua ambayo ukinikuta niko GEREJI natengeneza Magarai uanweza FIKIRI mimi ni engineer mkubwa sana wa Magari, Ukinikuta nashughulika na masuala ya Psychology unaweza fikiri Mimi ni level ya kina Sigmund Freud na ukinikuta katika masuala ya afya utafikiri mimi ni MD wa kiwango cha juu.

Nimejikuta nina ufahamu mpana wa mambo mengi ingawa hata hivyo sijafikia kiwango cha kujiita Master katika lolote so siwezi kujiita mtaalamu lakini kwa hakika ninayo maarifa ambayo yananitosha kumudu maisha yangu ya kila siku bila wenge.

Kitu ambacho naweza kusema kwa hakika ni kwamba maarifa haya yote niliyapata ndani na nje ya mtandao.

Swali ambalo nimeuliza hapa leo ni JE unafanya nini mtandaoni?Mtandaoni imekuwa ni sehemu bora zaidi ya kuzurura kuliko mtaani.

Kupitia mtandao unaweza kuzurura hadi vijiwe vya madaktari wa fizikia, au ukazuru hadi Marekani bila kutoka hapo ulipo. Je unatumia hio fursa ipasavyo?

Usikubali kuachwa nyuma. Kuwa sehemu ya mapinduzi ya mtandao na ushiriki katika kuwa sehemu ya mtandao kwa kutumia mtandao kujipatia maarifa na taarifa.

Tumia maarifa na taarifa hizo kujenga maisha yako ila zaidi JIJENGE WEWE mwenyewe.

Nakutakia kila la heri
 

Luckman1

JF-Expert Member
Feb 8, 2017
2,682
2,000
Tunaishi zama za TEHAMA

Naamini kabisa unaposoma andiko hili unatumia kifaa cha tehama na unatumia bando hata kama hujalilipia ili uweze kuisoma hii taarifa.
Mwaka 2000 wakati bado teknolojia ni changa nilwahi kumwambia rafiki yangu mmoja juu ya maono yangu kuhusu teknolojia.Kipindi hicho ilikuwa ni zama PENTIUM, na Floppy DISK na CD-R na CD-RW ilikuwa ni kipindi cha Internet Cafe.Teknolojia
Word!!!
 

Daviie

JF-Expert Member
May 20, 2016
1,246
2,000
Unfortunately watu wengi wanatumia mitandao kupromote vitu vya kijinga so hata ukiingia mtandaoni kuzura labda utakutana na kitu kizuri cha kujifunza unakutana na vikwazo kibao unaweza jikuta umepoteana hapo katikati umbea umeshika sana kasi
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
10,958
2,000
Dah Mimi naingiaga site za porn,jf, WhatsApp kdg,Kisha nacheki movie au walking tour ulaya huko
 

online24

Member
Jul 20, 2020
96
125
Unfortunately watu wengi wanatumia mitandao kupromote vitu vya kijinga so hata ukiingia mtandaoni kuzura labda utakutana na kitu kizuri cha kujifunza unakutana na vikwazo kibao unaweza jikuta umepoteana hapo katikati umbea umeshika sana kasi
Inategemea Umeingia kijiwe gan mkuu, mtandaon ni kama Mtaan tu, vijiwe vya wavuta bangi vipo lkn vijiwe vya mambo ya msingi pia Vipo ko Ni wewe tu,
 

Caps Lock

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
328
1,000
Uzi mzuri huu.
Kiasi mtandao umenisaidia jinsi ya
a) kujua njia za kumanage pesa hii hii ndogo nayoipata.

b) kupitia YouTube tutorials nimejua Adobe photoshop kwa kiasi chake
c) Imeniwezesha kupata vitabu na kuongeza maarifa
d) imeniwezesha kujua na kuendeleza hobbies zangu
e) imeniwezesha kukutana na mitandao miwili mikubwa hapa duniani quora na jamii forum

KUBWA ZAIDI IMENIWEZESHA KUPATA ANDIKO LAKO BORA KWA WEEK HILI.
 

Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
25,335
2,000
Kazi ninayoifanya now ni mitandao imesaidia na bado najifunza mengi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom