Mr. Purpose
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 1,439
- 2,690
Habari wakuu!
Ili kuishi maisha ya furaha na kuwa na afya njema kulala usingizi mzuri ni sehemu muhimu ambayo huweza kuimarisha afya ya akili na mwili pia.
Leo naomba tujadili, wewe ili upate usingizi mzuri, unafanya nini kabla ya kulala?
Nikianza Mimi Mr. Purpose binafsi, ili nipate usingizi mzuri ni lazima nifanye moja ya vitu vifuatavyo au vyote kwa pamoja:-
1. Mazoezi ya viungo.
Jioni nikifanya jogging au mazoezi yoyote ya viungo huwa akili inatulia hivyo kupata usingizi mzuri bila tatizo.
2. Kuoga maji ya baridi kabla ya kulala.
3. Kufanya meditation jioni kabla ya kulala.
Hii huwa na mchango mkubwa sana na huwa hata nikiamka asubuhi mambo yangu huwa yanaenda vizuri sana.
4. Kusoma kitabu au makala yoyote.
5. Tendo la ndoa.
Hii nayo huwa ni sehemu ya kupata usingizi mzuri hasa pale ambapo limefanyika kwa umakini na umaridadi wa kutosha huwa nalala vizuri sana.
NB: kumbuka tendo la ndoa ni dawa na inasaidia kutibu magonjwa kadhaa, ntaleta uzi kulielezea kwa kina.
Sasa mdau, turudi kwako, wewe unafanya nini ili kupata usingizi mnono na kuamka ukiwa mchangamfu kiakili nakimwili pia?
Karibu tujadili.