Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
JE UNAFAHAMU WEWE UNAYO DAMU YA KUNDI GANI NA TOFAUTI ZAKE?
Katika pekua yangu nimegundua leo hii kuwa watanzania wengi hatujui tupo katika kundi gani la damu.
Na mbaya zaidi utakuwa wakina mama wana kundi labda -O, au kundi lenye Negative huwa wanajifungua mtoto mmoja tu halafu hajifungui tena au wakijifungua mtoto akifa hawajifungui tena, hii inatokana na kutojua kundi la damu la mama na kundi la mtoto aliyezaliwa, kama mama hatapimwa na kujulikana kundi lake la damu basi ataonekana tasa, hazai.
Kinachotakiwa kufanyika ni mama kutambua kundi lake la damu, na atakapojifungua tu mtoto naye achukuliwe damu kwa ajili ya kujua kama wanafanana kundi au laa, kama hawafanani ni lazima mama achomwe sindano pale pale inayoitwa Ant-D ili imuwezeshe kupata ujauzito tena na kujifungua.
Bila hivyo mama kupata tena ujauzito ni hadithi na atatembea sana kwa waganga, hospitali, makanisani akitaka msaada kama hawajagundua hili.
Nawashauri watanzania wenzangu tupime ili tutambue makundi yetu ya damu.
Pia unaweza kusoma:
1) Je, unajua kuwa tabia ulizonazo ni kutokana na kundi lako la damu?
2) Naomba Kusaidiwa Kufahamu ni Makundi gani ya Damu ambayo Watu wenye nayo Hawaruhusiwi/si vyema Kuoana?
3) Yafahamu makundi ya damu na mahusiano yake na magonjwa
4) Je, ni kweli wenye damu kundi O huwa hawana risk kubwa ya magonjwa ya maambukizi? Hasa ya magonjwa zinaa?
5) Kuna uzushi ya kwamba watu wenye damu group O, wanapata shida kupata Mtoto