Unafahamu VPN Bora ya Simu kuwa Nayo

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Unafahamu VPN Bora ya Simu kuwa Nayo

tunafahamu story ya mjini siku hizi Tanzania ni suala la VPN kwenye simu zetu za mkononi mtu Ana hamu ya kuwa nayo na kujua matumizi yake usijali nakujuza.

mnamo mwaka 2018 March, NordVpn uliunda mfumo wa kuwazuia watu kuweza kudukua taarifa za watumiaji wa vifaa vya kieletronikia ambayo yalipelekea machafuko katika Tasnia ya VPN duniani.
lengo lao lilikua kuweza kulinda taarifa za watu dhidi ya hackers wadukuzi wa taarifa za watu katika simu za mkononi. Ila kampuni hiyo ilikua na seva ambayo ni ndogo, Hii ilifanya watumiaji wafikiri kwamba ikiwa wanapaswa kuiamini kampuni hii au la. Kama mitandao ya VPN inalinda, watumiaji wake kuhifadhi data walianza kutafuta njia mbadala zaidi ya NordVPN ambazo zinaaminika Sana.

VPN kirefu chake ni Virtual private network ambayo kazi yake kuu ni kumsaidia mtu na kifaa chake kwa kuweza kulinda kisiweze kudukuliwa na watu taarifa zake(kuangalia au kupeleleza data yake) wakati anatumia mtandao (interneti ) kwenye simu au kompyuta.

ikiwa hutumi huduma yoyote ya VPN jua kuwa data zako kuingiliwa na kudukuliwa kwa urahisi Sana inaweza kuathiriwa na mashirika makubwa na hata ya serikali. Kwa hivyo kaa Sasa bila kujulikana kwenye interneti, wavuti Sasa kwa kutumia VPN iliyosalama kwako.

Ila sio Kila VPN ni salama kwako zingine sio nzuri tambua Hilo kwaiyo nimeamua kukuletea baadhi ya VPN za kuwa nazo hakika ni nzuri na uta enjoy ukitumia.

Private internet Access (Pia)
Express VPN
Mullvad VPN
TunnelBear
cyberGost
Pure VPN
Surfshark
Ip Vanish pamoja na
Proton VPN

ngoja nieleze mojawapo tu sio zote jamani

PIA , PIA ni moja wapo ya majina ya kuaminika katika tasnia ya VPN. Ina zaidi ya miaka 10 bado inaendelea kupiga kazi, pia ni moja Kati ya VPN ya kitambo kwenye industry.
kampuni yake Mara nyingi inafanya update ya mifumo ya server yao ili kuipa nguvu na kuipa ulinzi imara dhidi ya hackers.
inaendeshwa na zaidi ya mifumo miwili za hali ya juu zaidi za usalama
L2TP/IPSec na OpenVPN
zimehifadhi seva nyingi kwani haijawahi kuona ukiukaji/ ubabaishaji wowote kwenye usalama hadi sasa. Inatoa usimbuaji wa data wa AES 128-bit na 256-bit.
faida:
Itifaki ya usalama wa kiwango cha ulimwengu was juu.
Inaweza kuunganisha vifaa hadi 10 bila kupunguza kasi ya mtandao.
hasara:
Ni kampuni ya Amerika, kwa hivyo inafuata sheria za Amerika
gharama:
Ni bei rahisi kabisa kwa mpango huanza kutoka $ 3.33 sawa na tsh 7,726.47/=
kila mwezi na pia ya mwaka hipo.

hivyo tuishie hapo tu kwa machache .
VIPI UNATUMIA VPN gani kwenye simu yako
tuachie maoni yako Sasa;
 
Nipo na Proton VPN nilikua na mashaka nayo sna Ila asante Kwa kunitoa hofu
 
Mkuu naskia watu wanakamatwa kwa kutumia VPN kuna jamaa yangu kanipigia ananiambia kuna dogo yupo kituoni kisa VPN ananishauri niitoe.vp kuna ukweli wowote kwamba TZ ni marufuku VPN
 
Mkuu naskia watu wanakamatwa kwa kutumia VPN kuna jamaa yangu kanipigia ananiambia kuna dogo yupo kituoni kisa VPN ananishauri niitoe.vp kuna ukweli wowote kwamba TZ ni marufuku VPN
Huyo atakua alikamatwa physically pengine akiwa anaongea maneno ambayo yanaashiria kua ni mtumiaji wa vpn.

Sitaki kuamini kwamba idara ya mawasiliano ilimnasa kupitia hacking sysytem

Kwaiyo sikushauri uitoe hiyo vpn kwasababu juzi lipumba amepost huko twitter, bonnah naye kapost na harmonize pia kapost akiomba tcra wafungue internet ili aachie wimbo wake

Sasa kama ni illegal serikali ilitakiwa ianze kudili na watu kama hao. Pia nao TCRA niliona wamepost kwenye page yao sasa, walitegemea huo ujumbe wao usomwe na kina nani wakati wao ndio waliofunga mitandao kwanini wasitumie redio au television kuwasilisha habari yao?
 
Kwamba TCRA walitumia VPN kutoa taarifa ya kuzuia watu kitumia VPN...
Yale yale ya wanakusanyana ili kitukataza tusikusanyike
 
Back
Top Bottom