Unafahamu unaweza kuamua muda unaotaka intaneti izime kwenye simu?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Unajua unaweza kuamua muda unaotaka intaneti izime kwenye simu ?

Katika ulimwengu wa sasa vifaa vya kidijiti vinatengezwa kuweza kufanya kazi mbalimbali ambazo hata bila ya mhusika kutumia nguvu; teknolojia ya leo unaweza ukaiweka simu kwamba ikifika saa fulani izime/iwake, ipige kengele, intaneti izime, n.k.

Binafsi ni mtu ambaye natumia muda mwingi tuu kwenye mtandao nikifanya vitu mbalimbali na nimekuwa nikiwaza sana namna ambayo mtu anaweza kuamua saa ngapi intaneti izime kama ambavyo anaweza kupanga simu yake imkumbushe kuwa muda umefikia wa kufanya jambo fulani.

FIkiria wewe ni mmoja wa wale ambao wanapenda kufanya kazi mtandaoni usiku wa manane lakini ikafika muda fulani ghafla tuu ukapitiwa na usingizi huku ukiwa umeacha intanei ya kwenye simu yako inaendelea kutumika. Au umejiunga na kifuruushi cha usiku tu (intaneti) halafu inafika saa 12 asubuhi wewe umeshalala maana yake ni kwamba intaneti inaendelea kutumika mpaka hapo utakapoizima/kitakapokwisha.

katika njia sahihi ya kuweza kuzuia Hilo Jambo nikakutana na program moja hivi ambayo inapatikana play store CleverConnectivity +++Battery je inafanya kazi hiyo app ?

Kuzima/kuwasha intaneti (WiFi/3G). CleverConnectivity +++Battery inawezesha kuzima intaneti kulingana na vigezo ambavyo utakuwa umevichagua mathalani wakati wa kupumzika, pale ambapo intaneti haitumiki baada ya muda fulani kupita au ikifika muda fulani basi intaneti izime.

Sasa utaweza kuzuia matumizi hovyoo ya intaneti kwenye simu yako kwa kuweza kuzuia tatizo la kutumia internet hata wakati umepitiwa na usingizi .

unaweza jiunga nasi kwenye link hapo chini kujifunza mengi kuhusu masuala ya teknolojia Sasa

Instagram
20201111_134956_0000.jpg
 
Back
Top Bottom