Akili 7
JF-Expert Member
- Apr 22, 2019
- 731
- 1,416
Mbona kuna kipindi mtu ukiwaza sana pesa au.kazi kwa muda mrefu kichwa kinauma na mishipa ya fahamu inasimama hii siyo hatari kwa afya?Asante sana Neo. Nitajaribu kukujibu vyema.
Kwa lugha rahisi wengi husema kuwa mawazo ni kama vile bubbles zinazotoka kwenye kisima cha akili. Au ni sawa na kusema kuwa Subconscius part inatazama kioo, kioo hicho ni conscious mind, na mawazo ni kama ukungu unaozuia subconscious kutazama conscious part.
Ili kuelewa vyema mawazo ni nini, chukulia mfano wa redio. Mwanadamu ni redio, mawazo ni mawimbi yako ya umeme. Kila wazo lijapo, ukilikubali na kulishikilia basi wazo hilo hutuma waves/mawimbi kwenye ulimwengu (To The Universe) na hufanya mpangilio wa universe kujiweka katika reality hiyo ya wazo hilo. Hivyo mawazo sio mabaya bali ubaya ni kuwaza mawazo mabaya na mawazo yasiyo na umuhimu katika safari ya maisha. Kama utajishikilia na mawazo na kuamini kuwa wewe sio kiongozi wa mawazo yako basi mawazo yatakutawala na utakuwa mtumwa wa kuitikia mawazo yako bila kujijua. Wengi sana wanatenda, wanaongea, au wanawaza kile kijacho akilini bila kuwa na time na space ya kujichunguza.
Hivyo ni vyema kuwa askari wa kutazama mawazo unayoyatazama bila kujishikilia nayo. Na ili kuweza kufanya hivyo ni kuweka mawazo yako au akili yako katika jambo moja. Ni kitu ambacho unaweza kuona ni rahisi lakini ni kigumu sana kwani hapo mwanzo katika dakika za mwanzo unaweza kumudu lakini baada ya muda akili itakudanganya kuwa its booring to do that na itaanza kuama na kuanza kuona kuwa
ni vigumu kuweka akili kwenye wazo moja.
Miaka ya kale watu walikuwa wanapata busara, hekima, nguvu ya maajabu, kuona nguvu za Mungu, na Kufunuliwa kupitia mafunzo yaliyokwepo ya kufundisha watu kuongoza akili zao.
Mfano mzuri unaotumika ni sala, nyimbo, meditation, yoga, n.k vyote hivi lengo lake kuu ukichunguza ni kukuongezea concentration. Unapoweka akili kwenye jambo moja na kuweza kumudu katika hali hiyo kwa muda mrefu kama lisaa, siku n.k unaongeza nguvu yako ya asili. Thats the fact. Ndio maana watu walioweza kufunuliwa hapo kale walishapitia kipindi cha kujitesa mfano kufunga, meditation, kuwa mbali na watu (kujitenga) n.k Katika kipindi hiko wanapata strength.
Third Eye ni sehemu ya nyuma ya macho na juu kidogo katikati ya macho yako. Ndani kuna peneal gland. Hii ni gland ambayo inatoa kemikali maalumu mara mbili tu katika maisha yako kemikali hii inatoka yenyewe.
Inatoka
Kemikali hii imegundulika kuwa kwa watu wanaofanya meditation huwa inatoka pale mtu anapokuwa katika very deep meditation. Au pale unapoweka akili kwenye kitu kimoja au wazo moja tu basi unaamsha kemikali hii.
- Siku ukizaliwa
- Na wakati unakata roho.
Pia ni vyema kufahamu Chakra ni nini. Ni sehemu kuu saba za nguvu ya mwili. Sehemu hizi hufunguka moja moja kutoka chini ya uti wa mgongo mpaka kwenye utosi. Nazo zinahusika sana ili kuelewa Third Eye.
Sent using Jamii Forums mobile app