Unafahamu kuwa kila Mwanadamu anayo nafasi ya kwanza?Acha kuigiza na kushindana

Victor Mlaki

Verified Member
May 1, 2016
2,406
2,000
Watu wengi leo tunaumia sana kwa sababu tunapingana na asili yetu " upekee" tulioumbiwa na Mungu.Hayupo Mwanadamu ambaye hana upekee wake unaoweza kumuweka katika nafasi ya kwanza kwa sababu hayupo mwingine mwenye nao.

Inamgharimu Mwanadamu nguvu nyingi mno kufanya jambo kama mtu mwingine kuliko kufanya jambo kama yeye. Hatukuumbwa kushindana ila tumeumbwa kila mmoja kuwa nafasi ya kwanza kwenye upekee wake.

Haipo haja ya kuwa na uchungu moyoni pale mwenzako anapofanya vizuri jambo lolote kuliko wewe.Usijilinganishe naye kwa kufikiri na wewe ni kama yeye, kumbuka kuwa wewe pia una upekee wako ambao yeye hana na hawezi kuwa kama wewe.

Nafasi yako ni ya pekee sana katika ulimwengu huu kama ukichukua jukumu la kufikiri kwa kina na kukubali katika upekee wako. Kila Mwanadamu anacho anachoweza kukifanya kwa ubora na wepesi na kwa utofauti kuliko mwingine yeyote.

Jifunze misingi ya asili yako na siyo kushindana nayo ili yanayofanywa na wengine yasiwe kikwazo cha wewe kufanya yako ila yawe sababu ya wewe kuhamasika kufanya cha kwako.

Dunia ingekuwa siyo mahali pazuri kwa Mwanadamu kama tungeumbwa kwa katika misingi ya kushindana na kukosa upekee.Inawezekana utajiri na mafanikio mengine yote yangekuwa ya ubaguzi sana lakini misingi yetu inaonesha " wakati na bahati huwapata wote".

Kuwa wa kwanza katika nafasi yako ( upekee wako) ni rahisi sana kuliko kujilinganisha na kutaka kufanana na wengine.
 

Mkogoti

JF-Expert Member
May 3, 2020
1,747
2,000
Jirani yangu hapa kanunua subwoofer Weeee nikaona asinitanie nami nimeenda kukopa hela nikaenda kuchukua Seapiano, sahivi nipo nachungulia madirishani kumkwepa mdeni wangu, 🤕😞
 

Styles

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
294
250
Jirani yangu hapa kanunua subwoofer Weeee nikaona asinitanie nami nimeenda kukopa hela nikaenda kuchukua Seapiano, sahivi nipo nachungulia madirishani kumkwepa mdeni wangu, 🤕😞
Duh..pambana Sasa ulipe Deni la watu..😂😂
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom