Kicheche mkali
Senior Member
- Nov 3, 2021
- 126
- 107
Ona muongo mwingine huyu!Mimi kabla sijajenga nilinunua Kirikuu ambayo imenisaidia sana kama kupeleka mafundi site, kununua mwenyewe material kama cement nk. Nasimamia ujenzi mwanzo mwisho na wakimaliza jioni nawabeba nawarudisha, hakuna aliyeniibia, zaidi sana mimi nina uelewa wa ufundi hadi ratio za cement nilikuwa nawaelekeza.
Sikuchukua mafundi expensive ila hawa hawa wadogo nilikuwa nawaelekeza navyotaka mimi na sio ushauri wao. Mjengo umeisha na ninaishi himo na familia yangu, kazi nyingi za finishing kama water system, sanitation kama jikoni kuweka marble, kufunga WC (water closet) kupiga gypsm na skimming pamoja na Painting nimefanya mwenyewe!
Nilikuwa nafanya hivi, nikimwita fundi site na nikiona ana gharama kubwa labda kutokana na kazi inahitaji vifaa basi mimi nanunua vifaa hivyo nafanya mwenyewe kazi ikiisha napata faida ya vifaa. MFANO fundi bomba akija anataja gharama yake anaweza kusema kila kupiga thread joint moja ni 500, basi nikanunua Die za bomba pamoja na Vice pamoja na pipe wrench kazi ikiisha vinabaki kuwa vyangu.
Fundi wa mageti nkaona gharama zake ni kubwa anasema kutengeneza geti ni 450,000 basi mimi nanua mashine ya welding ya 280,000 na material za 150,000 nafanya mwenyewe kwa vile naweza kuthubutu, hivyo nimebaki na mashine ya welding na geti nikalishona mwenyewe, hadi sasa nina mashine nyingi za kazi nafanya mwenyewe kurekebisha nyumba pale linapotokea tatizo kwa vile vitendea kazi ninavyo.