Unaenda lini 'site' kuendelea na ujenzi?

Mbao Tanzania

Member
May 31, 2021
55
125
Kwanza tunawapongeza wote mnaoendelea na ujenzi wa makazi. Kumiliki nyumba kuna heshima yake.

Lakini hebu tuambieni, ratiba za kwenda site huwa zikoje?

Mfano wewe unayejenga; site unaenda kila wikiendi kwa ajili ya kusimamia mafundi, au kila unapopata hela ya kujazia jazia vifaa na malipo ya hapa na pale?

Ruhusa kushea picha ya mjengo na mahesabu hasa ya mbao za kupaua kwenye uzi huu ili "kuwatia hasira" na wengine wahamasike!
 

Mbao Tanzania

Member
May 31, 2021
55
125
Mimi site nilikuwa ninaenda kila jioni kuangalia maendeleo na kujua kasoro, ilinisaidia sana kujua matatizo mapema kabla ujenzi haujafika mbali, ila bado kuna mambo nilijifunza ambayo nitaboreha kwenye ujenzi wa pili.
Maana yake umeshamaliza ujenzi wa kwanza. Hongera sana Mkuu.

Unashauri ni vizuri kwenda kila jioni au kila mwishoni mwa wiki?
 

mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
761
1,000
Matatizo gani mfano?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Mimi nilishakuwa nimeandaa madirisha yangu na milango ya nyumba nzima kabla sijaanza ujenzi, na kumpa fundi vipimo vyake, walipoanza walikosea ukubw akidogo ila sababu kila jioni ninaenda nikawa ninajua mapema tukairekebisha kabla ya kuta kuanza kupanda, hilo moja ninalokumbuka kwa haraka.
 

Mbao Tanzania

Member
May 31, 2021
55
125
Tupe na bei elekezi.
Kwanza lazima ujue mbao zetu zinatokea Mafinga na zimechemshwa na mashine ya dawa (treated).

Bei ya sokoni ni kama zifuatavyo:

FUTI 12
2*2 = 2900/=
2*4 = 5800/=
1*8 = 14000/=
1*10 = 18000/=

FUTI 20
2*2= 400/=
2*4= 750/=
2*6 = 1200/=

Ukitupigia simu ukataja unatokea JamiiForums tutakufurahisha kwenye bei. Usafiri mpaka site ni BURE kwa Dar es Salaam.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom