Unaelewa nini kuhusu tofauti za "Roho" na "Moyo"?

amnenuka

New Member
Mar 10, 2010
3
0
Maneno ya Kiswahili, "roho" na "moyo" hutamkwa mara kwa mara katika maisha ya Mswahili. Baadhi ya utumizi wa maneno haya ni "ana roho ya paka", "ana roho ngumu" "ana roho ya korosho" n.k., halikadhalika neno moyo hupatikana katika misemo kama vile "nilimpokea kwa moyo mweupe", "ana moyo mgumu" n.k.
Naomba misemo ya aina hiyo yenye kuhusisha maneno hayo, yaani roho na moyo, kisha ningependa kujua maana rahisi ya maneno hayo na tofauti ya maneno hayo. Andika chochote unachojua kuhusu maneno hayo.

Nawasilisha.
 
nadhani moyo ni ogani ya kibaiolojia, na hutajwa in biological aspects.
Roho ni uhai wa mtu, thats why akifa, tunasema roho imemtoka,
huhusianishwa na moyo, labda kwa kuwa moyo ndio msingi wa uhai a.k.a kisukuma damu.
Roho hutajwa tunaporejea spiritual act za mtu...
Thats all I know.
 
Maneno ya Kiswahili, "roho" na "moyo" hutamkwa mara kwa mara katika maisha ya Mswahili. Baadhi ya utumizi wa maneno haya ni "ana roho ya paka", "ana roho ngumu" "ana roho ya korosho" n.k., halikadhalika neno moyo hupatikana katika misemo kama vile "nilimpokea kwa moyo mweupe", "ana moyo mgumu" n.k.
Naomba misemo ya aina hiyo yenye kuhusisha maneno hayo, yaani roho na moyo, kisha ningependa kujua maana rahisi ya maneno hayo na tofauti ya maneno hayo. Andika chochote unachojua kuhusu maneno hayo

Nawasilisha.
Roho ni kitu kisichoonekena ambacho hufikiriwa kuwa ni sehemu ya mwili wa kiumbe ambayo hukiwezesha kuwa na uhai.
Moyo ni kiungo cha mwili kilichopo kwenye sehemu ya kifua kati ya mapafu, ambacho husukuma damu ili ienee mwilini kw kupitia mishipa
 
roho simple ni kiini cha uhai wa kiumbe chochote kinachoishi. hivyo basi hakuna tafsiri ya nini au kiungo gani ni roho. roho inahusisha uwezo wa kula, kunywa, kuvuta hewa na vyote vitakavyokusaidia uendelee kuwa hai. Moyo ni kiungo ambacho moja kwa moja kinahusiana na mzizi wa Afya ya kiumbe chenye uhai. ili kiumbe kiwe na afya nzuri lazima kiwe na moyo ili kuratibu shughuli zote za kiafya. na ndiyo maana hata JIPU lina moyo.
 
Na mtu akisema roho inauma ana maanisha nini?

maana yake ni nafsi yake imeumizwa na jambo fulani, mathalani, wazazi huumia roho wanapoona watoto wao wanakaidi kufuata maelekezo na mafunzo mema kutoka kwao na hatimaye kuishia kupata matatizo.
 
sasa inakuwaje moyo mweupe wakati unasukuma damu ambayo nyekundu

moyo mweupe ni tamathali ya semi....maana yake mtu ameridhia wewe ufanye jambo fulani.

ni kama vile mkubwa wako ofisini akikwambia kwa kizungu, "am giving you the green light....", maana hapo si taa ile ya kijani inayoruhusu gari kupita barabarani bali ni ruhusa ya kufanya jambo mfano wa ile taa ya kijani inapowaka kuashiria ruhusa ya magari kupita.

kiswahili kitamu, basi tu, penye miti hapana wajenzi!
 
Nakupenda kutoka moyoni

moyo ni kiungo adhimu sana katika mwili wa mwanadamu ambacho kikipata khilafu aghalabu afya ya mwanadamu huwa shakani.

ikiwa mtu amekupa nafasi ya kukaa katika moyo wake, basi amekutukuza sana na ni stahiki kwako kulipa heshima hiyo ingawa si mara nyingi twafanza hivyo.

kwa hivyo kupendwa kutoka moyoni maana yake ni mtu kupewa nafasi adhimu katika maisha ya kimapenzi ya mtu huyo. n
 
Back
Top Bottom