Unaelewa nini juu ya gharama za uendeshaji wa viwanja vya ndege..?

Mzalendo-Tz

Member
Apr 19, 2017
81
125
36910943_2165181167035135_8631662935174807552_n.png

Kama ilivyo kawaida ya watu wengi walioshindwa maisha kuamini kwamba kwa njia ya kuwachafua wenzao ndio kufanikiwa kwao,tangu ujio wa ndege mpya iliyonunuliwa na serikali aina ya Boeing 787-8 Dreamliner kwa ajili ya kulifufua shirika la ndege la Airtanzania naona wameanza kuibuka watabili na wapiga ramli wengi kuitabilia ndege hiyo hasara na kushindwa kwa shirika la ndege katika kujiendesha,tumeshuudia viongozi mbalimbali wa vyama pinzani wakiandika kauli mbovu juu ya ujio wa ndege hiyo na hata kuikosoa serikali juu ya uamuzi wa ununuzi wa ndege hiyo.

Kilichonisikitisha zaidi ni mjinga mmoja kuanza kupotosha na kuaminisha mambo mengi yasiyokuwa na tija kwa taifa na kwa ustawi wa shirika letu la ndege la airtanzania juu ya gharama za uendeshaji wa ndege hiyo katika safari mbalinbali itakazokuwa inafanya.

Katika kufanya biashara ya aina yeyote kuna gharama za uendeshaji ambazo hutumika katika kuiendesha biashara hiyo mfano mdogo ni biashara ya ubuyu.

Ubuyu ni malighafi ya biashara ya ubuyu lakini ili iweze kukamilika na kupata wateja na kuwalizisha wateja wako kuna hatua kadhaa za kupitia ili kufanikisha biashara ya ubuyu. Zifutazo ni hatua za kukamilisha biashara ya ubuyu,

I.Gharama za kununua malighafi(ubuyu,sukali,rangi na mifuko ya kufungashia ubuyu)

II.Gharama za usafilishaji kutoka shambani kwenda kiwandani

III.Gharama za uzalishaji na uendeshaji wa kiwanda (umeme au moto kwa ajili ya kufungia ubuyu)

IV.Gharama za usambazaji

V.Kodi ya mamlaka ya mapato(TRA)

Sasa turudi kwenye hoja ya msingi kwa kawaida seemu yeyote duniani hakuna kitu cha bure na endapo kuna mtu atatokea kunibishia kuwa kuna kitu cha bure na aje na hoja ya msingi, basi kama hakuna tuendelee.

Mashirika yote ya ndege Duniani yana ingia gharama mbalimbali katika kuendesha mashirika yao na hata kufanikisha biashara hiyo ya ndege,hakuna kizuri kisichokuwa na gharama na ndio sababu watu uingia gharama ili kupata huduma nzuli na zenye kuwaridhisha kulingana na thamani ya pesa zao, gharama hizo ambazo watu uingia ndizo upelekea utendaji kazi mzuri wa shirika la ndege kwa kupitia huduma wanazozitoa.Ndio sababu hata Shirika letu la ndege la airtanzania litalazimika kuingia hizo gharama kwa ajili ya kufanikisha biashara ya ndege na kutoa huduma nzuri kwa wateja wake.zifuatazo ni baadhi ya gharama ambazo mashirik ya ndege duniani uingia katika kufanikisha safari zake na huduma kwa ujumla katika nchi husika na kwingineko duniani.

I.Gharama za wafanyakazi

II.Polisi, Gharama za ulinzi, Gharama za zima moto(Uwanja wa Ndege)

III.Mazingira

IV.Gharama za Matengenezo ya magari

V.Gharama za Masoko, Mauzo na Matangazo

VI.Matengenezo ya kiwanja

VII. Utawala(fedha, HR, kisheria, mtendaji,manunuzi,na kadhalika.)

Izo ni baadhi tu ya gharama zinazutimika katika kuendesha na kusimamia shughuli mbalimbali za biashara ya ndege lakini pia tusisahau gharama zote uingiwa na kampuni husika ili kufanikisha safari zake ikiwa angani na ardhini.yaani inalipia anga ya nchi husika ndege inapokatisha na inapotua.
Mfano Ethiopia airline ikipita anga la Tanzania inalipia kwa sababu wafanyakazi wa mamlaka ya anga Tanzania ndio wanaohusika katika kuiongoza ndege hiyo iwapo anga la Tanzania,inafanya hivyo sio Tanzania tu bali popote inapopita italipia kwakuwa sio anga lake.kwahiyo hakuna kitu cha bure na gharama haziepukiki katika biashara,wataaram wa biashara wanasema ukiwa mbahili na muoga kweye kuwekeza uwezi kuwa tajili,kwa hiyo tusitishane nyie Airtanzania fanyeni kazi.

[HASHTAG]#vivatanzania[/HASHTAG]
[HASHTAG]#vivaairtanzania[/HASHTAG]
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,256
2,000
Ninachoelewa ni kwamba Tanzania inajaribu kupunguza hizo gharama kwa kuacha vyoo vichafu mara nyingi, na kuweka scanner za ukaguzi wa mizigo upande wa domestic arrivals bila sababu ya msingi ili kutoa fursa za ajira kwa Watanzania katika awamu hii ya tano ya maajabu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom