Unadhani Tanzania kuna fursa kubwa ya kutoka kimaisha kuliko nje?

Heavy Weight

JF-Expert Member
Mar 1, 2014
888
875
SABABU YA KURUDI TANZANIA

Tajiri Mo Dewji amejaribu kuelezea sababu iliyofanya arudi Tanzania, baada ya kumaliza masomo yake Marekani na kufanya kazi kwa muda.

Je unahisi Tanzania kuna fursa nyingi za kutoka kimaisha kama alivyoelezea?

Nilipomaliza masomo yangu ya shahada nikiwa nchini Marekani niliamua kubaki huko na kufanya kazi. Nilitumia muda na nguvu nyingi kazini lakini pesa ambayo niliipata haikukidhi kufanikisha malengo yangu.
Ndipo Baba yangu akanishauri nirejee nyumbani Tanzania na nilipofatilia kwa kipindi hicho niligundua kwamba Tanzania kuna fursa nyingi za kibiashara na hapo ndipo nilipoamua kurudi na kujiunga katika biashara ya familia.

Muhimu kufahamu ni kwamba mafanikio sio lazima uende kuyatafuta nje ya nchi, hapa hapa nchini kwetu kuna fursa ambazo ukifanyia kazi utafanikiwa.
Unafikiri kwanini baadhi ya watu wanapenda kuishi/kufanya kazi nje ya nchi?
__________________________
WHY I MOVED BACK TO TANZANIA
After completing my degree program in America, I decided to stay back and work. I used a lot of my time and energy at work but what I earned was not enough to allow me to meet my goal.

That’s when my father advised me to come back home Tanzania and after a bit of research I came to realize that there are a lot of business opportunity in Tanzania by then and hence I decided to move back here and join in the family business.

It is important to note that success is not necessarily found abroad, but there are opportunities here at home where if you work on them you can become successful.
Why do you think that some people prefer to live/work abroad?
 
Wanaofanya kazi nje ya nchi ni kwa sababu ya kipato,lakini kipato wanachokipata wakiwa kule kinakuwa ni kidogo kuwekeza katika nchi ile;ndio maana kuna wengine wanawatumia ndugu zao huku wawasaidie kuwekeza,ingawa pia kuna changamoto zake.Kwa mwenye malengo,hutakiwi kufanya kazi nje kwa muda mrefu,tafuta mtaji na urudi nchini bado kuna nafasi kubwa ya uwekezaji.Kwa hapa nchini wengi wanalipwa chini ya kiwango ukilinganisha na elimu walizonazo,na hii inasababishwa na tatizo la ajira.
 
Ni rahisi kupata mtaji ukiwa nje kuliko bongo nadhani ndio maana wengi wanazisaka ili waje kuwekeza tz
 
Ni Kweli,ila wengi wanarudishwa nyuma na ndugu au watu waliowaamini katika utekelezaji wa ndoto zao;wanatuma ela wakitegemea mwisho wa siku wakute 'lodge' matokeo yake unakuta kibanda
Ni rahisi kupata mtaji ukiwa nje kuliko bongo nadhani ndio maana wengi wanazisaka ili waje kuwekeza tz
 
Back
Top Bottom