Unadhani kati ya kanuni mpya za mafao ya wastaafu na kanuni mpya za bendera ya taifa rais alipaswa kufuta kipi?

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Kwa mtazamo wako, unadhani kati ya kanuni mpya za mafao na kikokotoo cha mafao ya wastaafu na kanuni mpya za bendera ya taifa na wimbo wa taifa ni kitu gani hada kimeleta mgogoro na mkanganyiko mkubwa katika jamii ambacho rais alipaswa kukifuta baada ya kuleta sintofaham katika jamii?

Rais alipaswa kufuta kanuni mpya za mafao au kanuni mpya za bendera ya taifa?

Kati ya hivyo vitu hapo juu ni kipi chenye maslahi na manufaa kwa wananchi ambacho rais alitakiwa kukifutilia mbali au kutoa muongozo mpya?

Wewe unafikiri kipi hapo? Mimi bado nafikiri, sijapata jibu kwa kweli.
 
Kufuta kanuni mpya za kikokotoo kwa sababu kanuni hizi zinawagusa si watumishi tu bali wananchi walio wengi kwa kuwa wanawategemea sana hao watumishi kuendesha maisha yao.
 
Tatizo hajui vipao mbele, ukimuwekea ndoano na samaki atachagua samaki hata kama yupo kando ya ziwa, badala ya kujenga miundo mbinu ya uzalishaji yeye anaweka miundo mbinu ya kukamua kodi kwa walalahoi
 
Hilo la bendera,angeipotezea ki utu uzima kwa kumwita waziri chemba,anaikanusha waziri mwenyewe.Hilo alilofanya Mh Rais;waziri alitakiwa kujiuzulu mara moja
 
Kwa mtazamo wako, unadhani kati ya kanuni mpya za mafao na kikokotoo cha mafao ya wastaafu na kanuni mpya za bendera ya taifa na wimbo wa taifa ni kitu gani hada kimeleta mgogoro na mkanganyiko mkubwa katika jamii ambacho rais alipaswa kukifuta baada ya kuleta sintofaham katika jamii?

Rais alipaswa kufuta kanuni mpya za mafao au kanuni mpya za bendera ya taifa?

Kati ya hivyo vitu hapo juu ni kipi chenye maslahi na manufaa kwa wananchi ambacho rais alitakiwa kukifutilia mbali au kutoa muongozo mpya?

Wewe unafikiri kipi hapo? Mimi bado nafikiri, sijapata jibu kwa kweli.
Naona Rais hatimaye kajibu swali lako mkuu.
 
Back
Top Bottom