50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 3,875
- 3,730
Wahenga: Mtegemea cha ndugu hufa masikini.Ukinyimwa msaada na ndugu au rafiki yako ambaye ni tajiri au mtu mwenye uwezo mzuri kidogo kifedha usichukue, usilalamike, usimsimange wala usimseme vibaya kwamba ana roho mbaya au ni mchoyo.
Katika jamii maskini kama zetu watu waliofanikiwa ni wachache na wanaombwa misaada na watu wengi wanaowazunguka sio wewe peke yako, hivyo ni bora kuwa muelewa pale unapokosa msaada unaoutarajia kwa mtu uliyemuomba huo msaada.
Hii imesemwa zamani kweusi.