Unabii wa T.B Joshua na yanayotokea South Sudan

Omuregi Wasu

JF-Expert Member
May 21, 2009
749
148
T.B Joshua alitabiri mauaji na kutekwa kwa Rais wa nchi. Tunakoelekea inaonekana unabii unaenda kutimia maana damu imeshamwagika kwa zaidi ya watu 500 kuuawa. Ngoja tuona maana biblia inasema neno langu halitarudi bure bila kutimiza kusudi lake. Nguvu ya waasi imekuwa kubwa kiasi cha kupiga ndege za Marekani zilizoko kwenye shughuli za amani.
 
Kama ni mauaji,mbona CAR wanauana kila siku kabla ya huko s.sudani! Akitekwa kiongozi, hapo utabiri wake utakuwa wa kweli.
 
Dah,mnatisha kwahiyo mnataka mpatie nafuu joshua kwa staili hiyo.?.
Si tunajua alisema kiongozi atatekwa na tunasubiri.
 
alichofanya rais wa sudan kuwatimua mawaziri ambao pia walifight wote lazima yangetokea haya.

pia makamu wake alipotangaza nia ya kugombea urais uchaguz ujao na jamaa akaona amtimue ilo ni janga pia.

nilishawai kuwaambia watu lazima kitanuka south sudan muda si mrefu kwa sababu hizo na kweli. sijaonyeshwa na yeyote bali nimeangalia mambo anayofanya uyo rais nikajua kitanuka.

pia south sudan walikuwa wana matarajio ya maisha bora baada ya kujitenga lakin hawajapata viongoz wao wanafisadi mabillion ya dollar.

ukiona apo juba panatia huruma mji mbaya sana
 
Huo utabiri wa T.B. Joshua bado usielekezwe South Sudan. Alitabiri kiongozi wa nchi atatekwa na hilo ndilo tunalolisubiri. South Sudan sio Afrika Mashariki hata kama wanataka kujiunga nasi. Tunasubiri utabiri wa kutekwa kwa kiongozi E.A. Nimekuwa na mashaka na PG kupotea kwa news hata alipoenda kwa msiba wa Mandela alienda kisirisiri na kuondoka kisiri. Kwenye sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Kenya sikumbuki kama nilimuona PG nadhani amegusiwa kuwa ajitahadhari.
 
T.B Joshua alitabiri mauaji na kutekwa kwa Rais wa nchi. Tunakoelekea inaonekana unabii unaenda kutimia maana damu imeshamwagika kwa zaidi ya watu 500 kuuawa. Ngoja tuona maana biblia inasema neno langu halitarudi bure bila kutimiza kusudi lake. Nguvu ya waasi imekuwa kubwa kiasi cha kupiga ndege za Marekani zilizoko kwenye shughuli za amani.
Mbona TB Joshua hakutabiri kifo cha Mandela, na jinsi viongozi wengi sana walivyofurika Afrika ya Kusini.
 
wakuu kuna nchi za jumuiya ya afrika mashariki na kuna nchi za africa mashariki.

nchi za afrika mashariki ni
Burundi
Comoros
Djbout
Eritrea
Ethiopia
Tanzania
Uganda
Rwanda
Kenya
Madagascar
Malawi
Mauritius
Mayotte
Msumbiji
Reunion
Seychelles
Somalia
Zambia
Zimbabwe

hivo rais atatekwa kwenye nchi hizo msije mkajua nchi jumuiya za EAC tu
 
T.B Joshua na watumishi wa Mungu wanasali kuepusha hiyo makitu. so hata isipotokea ni matokeo ya unabii kuzuia maafa hayo
 
Huo utabiri wa T.B. Joshua bado usielekezwe South Sudan. Alitabiri kiongozi wa nchi atatekwa na hilo ndilo tunalolisubiri. South Sudan sio Afrika Mashariki hata kama wanataka kujiunga nasi. Tunasubiri utabiri wa kutekwa kwa kiongozi E.A. Nimekuwa na mashaka na PG kupotea kwa news hata alipoenda kwa msiba wa Mandela alienda kisirisiri na kuondoka kisiri. Kwenye sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Kenya sikumbuki kama nilimuona PG nadhani amegusiwa kuwa ajitahadhari.

hakuna sehemu aliposema kiongozi wa East Africa atatekwa. alisema kiongozi atatekwa but hakusema ni wa east africa. alichosema kuhusu east africa ni tukio la kigaidi kutokea nchi ya east africa jirani na kenya
 
alichofanya rais wa sudan kuwatimua mawaziri ambao pia walifight wote lazima yangetokea haya.

pia makamu wake alipotangaza nia ya kugombea urais uchaguz ujao na jamaa akaona amtimue ilo ni janga pia.

nilishawai kuwaambia watu lazima kitanuka south sudan muda si mrefu kwa sababu hizo na kweli. sijaonyeshwa na yeyote bali nimeangalia mambo anayofanya uyo rais nikajua kitanuka.

pia south sudan walikuwa wana matarajio ya maisha bora baada ya kujitenga lakin hawajapata viongoz wao wanafisadi mabillion ya dollar.

ukiona apo juba panatia huruma mji mbaya sana
Ndio uone mifano halisi ya wapinzani wanapopata madaraka, hata Mbowe na Babu wakiingia yatakuwa hayo hayo. Ona Kenya hali mbaya kwa watumishi wa serikali na migomo ya watoa huduma za afya inashamiri! heri mtu ukae kwenye chumba chenye mbu uliokesha nao kuliko kuhamishiwa chumba kipya chenye mbu wenye njaa kali!
 
T.B Joshua na watumishi wa Mungu wanasali kuepusha hiyo makitu. so hata isipotokea ni matokeo ya unabii kuzuia maafa hayo

Acha akili za kushikiwa. Yaani mtu anatabiri janga lisipotokea mnasema watumishi wa Mungu walikuwa wanasali kuepusha hilo janga. Basi kama ni hivyo hata mimi naweza kuwa nabii nitatabiri mauaji makubwa kutokea Tanzania halafu baada ya muda kadhaa nitasema nimeombea mauaji hayo yasitokee. Simple like that.
 
Ndio uone mifano halisi ya wapinzani wanapopata madaraka, hata Mbowe na Babu wakiingia yatakuwa hayo hayo. Ona Kenya hali mbaya kwa watumishi wa serikali na migomo ya watoa huduma za afya inashamiri! heri mtu ukae kwenye chumba chenye mbu uliokesha nao kuliko kuhamishiwa chumba kipya chenye mbu wenye njaa kali!

Wewe ni great thinker, ahsante
 
hakuna sehemu aliposema kiongozi wa East Africa atatekwa. alisema kiongozi atatekwa but hakusema ni wa east africa. alichosema kuhusu east africa ni tukio la kigaidi kutokea nchi ya east africa jirani na kenya

Na hili tukio la kigaidi jirani na kenya nalo bado halijatokea mpaka sasa.
 
Kuna baadhi ya waganga na wabashiri wanaotumia nguvu za giza kubashiri maovu kisha kuzitumia nguvu zao kuyatekeleza maovu hayo ili kuvuta waumini kuwa ubashiri umetimia!.

Hata baadhi ya waganga, mteja anapokwenda kumlilia shida zake, humsaidia kumuondolea, wateja wakikauka, huwachagua baadhi wenye neema na kuwapiga majanga ili warudi kwake aendelee kuvuta!.

Yesu alipofanya miujiza, hakuvuta hata senti tano!.

Pasco.
 
Back
Top Bottom