Guru Master
JF-Expert Member
- Jan 14, 2017
- 224
- 591
"CCM itatawala Milele" CCM hoyeee..... Watu wakashangilia hoyeeee....
Kuna mtu alishangaa wakurugenzi wanateuliwa na kulipwa na yeye, sasa wanapata wapi Ujasiri wa kutangaza ushindi wa wapinzani? Watu wakashangilia tena.
Tambueni hizi ni dalili tu za uchungu bado uzazi wenyewe haujafika. Siku hizo kwa wale wanaojifanya ni wapinzani na wazalendo wa nchi zitakuwa mbaya za mateso,zitakuwa zenye kilio na kusaga meno. Na wengi wataomba siku hizo zisifikie wakiwa hai.
Wengi watatiwa magerezani katika siku hizo za mwisho, jua litatiwa giza.na Mungu ataendelea kufunga macho na masikio. Asitizame na kusikia kilio cha wananchi wa Tanzania maana wao pia waliziba macho na masikio yako wasisikie na kuyaona yale waliyopaswa kutenda.
Naam siku hizo zaja ambazo mwana wa uharibifu ataketi sambamba na babaye wakipanajisi mahali pa juu. Nao watazunguko miisho yote ya nchi wakitema moto na kumwaga mafuta.ole wao watakaokuwa katika siku hizo. Maana watataman kama wasingezaliwa na kuziona siku hizo.
Tizama nchi itatetemeka waliolala watapaza sauti zao na walio macho watameza sauti zao. Naaam.... Kitasikika kilio kwa wamama, wakiwalilia watoto wao na watoto wakiwalilia baba zao.... Nchi itakuwa ukiwa.... Na ndipo hapo wananchi watatizama wana nini mikononi na mioyoni mwao. Nao wataamka na kupoteza woga. Watasimama imara kupinga machukizo yote na nchi itaanza kujengwa upya.