Unaanzaje kuoga maji ya baridi asubuhi na kuna baridi?

fatu2010

Senior Member
Mar 4, 2014
173
141
Dah enzi hizo niko Tukuyu nasoma sec school kati ya vitu ambavyo vilinipa kazi mpaka sasa ni kuoga maji ya baridi asubuhi ili kuwahi assembly. Hivi wewe ulikua unaoga maji baridi kwa staili gani ile asubuhi na ukungu ama baridi tu huku tukiaminishwa kuna ngiri (ugonjwa na sio warthog).

Style yangu ni kuimba imba kwa sauti kuubwa mpaka nazuga maji ya baridi nayazoea hatimaye naoga. Kuna mwingine alikua anapaka sabuni kwa boxer then ndipo anazoea...duh reminisce

Tiririkaaaaaaaaa,wewe unaanzaje kuoga maji baridi, hasa kama ni eneo la baridi?
 
Usioge asubuhi kama kuna baridi sana. Fanya hivi.

Asubuhi:
  • Tia sabuni na maji kwenye wash-cloth yako mpaka iwe na povu jingi.
  • Safisha uso na makwapa ukiwa kwenye sink la kupigia mswaki.
  • Ingia bafuni, safisha nyeti zote.
  • Jifute na taulo na usafi wa asubuhi utakuwa umekwisha.
  • Cha muhimu ni kuzuia maji baridi yasiingie kifuani/mgongoni (torso).

Jioni:
Ingia kiwanjani fanya mazoezi ya nguvu.
Pumzika kidogo mpaka jasho likauke lakini mwili bado una joto.
Yaingilie maji baridi uoge mwili mzima.

Fanya hivyo kila panapokuwa na baridi.
  1. Oga jioni
  2. Nawa asubuhi
 
Asubuhi,anza kwa kufanya mazoezi magumu (mfano kurukaruka na skipping rope, press ups, frog jumps nk) kwa dakika angalau 15 au zaidi. Kunywa kahawa moto (binafsi napendelea ya bila sukari).
Baas! Kimbia bafuni.
 
Baada ya maandalizi yote ya kuimba na kufanya mazoezi, jaribio la mwisho ni kuyavaa maji:
Unaanza na viganja vya mikono kisha vifuti, baadaye unanyunyiza maji kidogo kichwani..na baada ya hapo ndio unapanga ku-expose mwili mzima baada ya kuji-condition...na hii inakuja yenyewe tu.
 
Mimi nilikuwa naanza kwa kudumbukiza mguu mmoja ndani ya ndoo yenye maji baridii na kufanya kama nanawa mguu ulio nje kisha namwagia maji kidogo kichwani yakianza kuchuruzika hapo ndio najitoa muhanga completely vile kidogo maji nimeyazoea naoga faster.
 
Kuna ujinga huwa upo kwamba ukioga maji ya baridi asubuhi basi wewe uko fiti.Hawajui kwamba sudden drop in body tem is also a major cause of stroke !!!!
 
Hakikisha Kwanza Unavuta Sana Bangi Na Ikishakolea Mwilini Zama Mtoni au Ktk Ndoo Uoge Na Hutoona Maji Ni Ya Baridi Tena. Kazi Kwako!
Kwa anayetoa ushauri kama huo tafadhali sana ondoa avatar hiyo kwani ni kinyume kabisa na mhusika anavyofikiria.
 
Mie nilisoma Iringa, nilikua naoga kila siku asubuhi na nikitoka hapo sivai sweta. Mwili ulizoea hiyo hali kiasi kwamba nisipooga asubuhi wakati wa break saa nne lazima nikaoge kwanza.

Nikifika nilikua sijishauri ni kujipaka povu mwili wote na kujimwagia Maji, Maji ya moto nikioga naona yanaongeza kuhisi baridi na hayaondoi uchovu.
 
  • Thanks
Reactions: 5ty

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom