Unaamini msaada huu wa wafanyabiashara kwa waziri wa Biashara na Viwandaa???

Bowbow

JF-Expert Member
Oct 20, 2007
541
31
Wafanya biashara wawili mkoani Arusha wasaidia shule mbili na hospital jimboni mwa Basili Pesambili Mramba.

Je nini kilichowavutia hadi kwenda Rombo na sio Umasaini? Mt Meru hakuna Vitanda wala magodoro yakutosha, kwa nini Rombo...?
Mimi ninao uwalakini tufungue macho tutazame....

soma hii kutoka alasiri
Kampuni ya utalii Arusha yasaidia ujenzi wa sekondari Rombo

2007-12-03 18:38:06
Na Radio One Habari

Kampuni moja ya huduma za watalii ya Arusha imetoa msaada wa shilingi milioni 15 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa sita ya shule mbili za sekondari za ghorofa zinazojengwa kwa nguvu za wananchi katika wilaya Rombo mkoani Kilimanjaro.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Leopard Bwana Zuhel Zafal ametoa msaada huo baada ya kutembelea shule hizo za Keni na Shimbi na Mbunge wa Rombo Mheshimiwa Basil Mramba kuona juhudi za wananchi katika ujenzi wa miradi yao.

Bwana Zafal amesema baada ya kukamilika kwa madarasa hayo ambayo yatawawezesha wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanza masomo mwaka ujao, atatembelea tena shule hizo kuangalia namna ya kuongeza misaada zaidi.

Wakati huo huo kampuni hiyo kwa ushirikiano na hoteli ya kimataifa ya Kibo Palace ya Arusha imeahidi kutoa vitanda 50 na magodoro 50 kwa ajili ya wagonjwa katika hospitali ya huruma wilayani Rombo.
 
Nafikiri ukishakuwa mbunge ni muhimu kuchangamkia nafasi yoyote kama hizi za misaada kwa manufaa ya wananchi wa jimbo lako. Kama Mheshimiwa Mramba ameivuta hii misaada ya kijamii jimboni kwake kwa manufaa ya wananchi nafikiri anastahili pongezi. Mbaya ni pale wabunge wanapoendelea kushiba kwa ufisadi na kuwasahau wananchi waliowapigia kura
 
Back
Top Bottom