UNAAMBIWA: Wanaume wenye ndevu hunufaika kiafya kuliko wasionazo

Ipo mitazamo tofauti juu ya wanaume wanaofuga ndevu, wapo wanaosema mwanaume kufuga ndevu humwongezea mvuto, wengine wakisema ni dalili ya uchafu na kutojipenda na mengine neyo mengi tu husemwa.

e261e4ab6d99e01dff434764dd0783cc.jpg

Shirika la Utangazaji la BBC lilishawahi kuandika katika chapisho la Maambukizi ya Hospitalini, ulifanywa utafiti ambapo wanaume 408 wenye ndevu na wasio na ndevu walitumiwa kwa kufanya uchuguzi huo.

Wanaume wote walipitishiwa kifaa maalumu kwenye videvu vyao ili kuona kama kuna vimelea vyovyote vinavyopatikana kwenye videvu na madhumuni makuu ya kufanya hivyo ni kwamba wataalamu wanaeleza kwamba hospitalini ndipo sehemu ambapo kuna maambukizi mengi sana ya vimelea mbalimbali.

Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa wanaume ambao hawakuwa na ndevu walikuwa hatarini kwa mara tatu zaidi wanabeba na kutunza vimelea hivyo kwenye ngozi zao za kidevu tofauti na wanaume ambao walikuwa wana ndevu.

Utafiti huu ukisapotiwa na tafiti nyingine ulihitimisha kuwa kunyoa ndevu mara nyingi husababisha kuchubuka kwa ngozi na hivyo kutengeneza makazi ya bakteria na mazalia yao.
huyo jamaa alikuwa anawekea mbolea
 
Tafiti za ulaya hizi
Na mwezi uliopita utafiti mwingine ulikuwa wa toilet paper
Unasema kumbe walikuwa wanakosea miaka yote kuchamba
Wameona maradhi mengi yanatokana na hizo karatasi (Toilet paper)
Yale yale, kazungu kamepata funding kakafanya research sisi tunaikumbatia, kifupi, hatutakiwi kunyoa misitu, ina maana yake, kuchamba ni maji na kunawa na sabuni, toilet paper inaacha uchafu, hatutakiwi kunyoa ndevu, hasa kwetu, inatulinda na hili jua kali, hatutakiwi kunyoa nywele kwenye pua zina maana yake, kutulinda na vumbi na wadudu, hatutakiwi kunywa sana maji, tule matunda zaidi, maji yapoteza baadhi ya kinga mwilini kila uendapo haja haja ndogo, hatutakiwi...
Tuna maisha yetu bana, watuache tuishi kiasili...
 
mbona mkuu nasikia kwamba maji nayo yana madhara???
Maji hayana madhara kabisa na ndio njia sahihi ya kujisafisha.
Kina mama wanawasafisha watoto kwa maji na wote tumepita huko, ila watu wanapokua wanabadilika na kuanza kutumia karatasi au majani kitu ambacho unapakaza mavi kwenye makalio badala ya kusafisha.
Lakini maji ni bora zaidi maana kama maji sio salama sasa sijui mbadala utakuwa nini hebu tusaidie kwa hili
 
but nasikia yanaleta fungus kuna ukwel juu ya hl??
 
Kufuga Ndevu Ni Sunnah Au Waajibu?

Ufugaji wa ndevu kwa mujibu wa dini ya kiislam

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ndevu baadhi ya Maulamaa wanasema ni Sunnah iliyokokotezwa, lakini Maulamaa wengi wa mwanzo na wa sasa wamesema ni zaidi ya hivyo, yaani ni WAAJIB, na mtazamo huu ni msimamo SAHIHI kwa dalili nyingi. Kuna shahidi nyingi kuthibitisha hilo.

Dalili katika Qur-aan tunaona kwamba hata mitume walikuwa wakifuga ndevu. Hii ni kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kuhusu Haaruun ('alayhis-salaam alipomwambia Musa ('alayhis-salaam) alipomshika ndevu zake baada ya kuwaona wana wa Israaiyl wamepotoka:

((Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea kauli yangu)) [Twaaha 20:94]

Hapa tunakupa dalili zilizothibitika katika Sunnah:

1. Mtawala wa Yemen, aliyechaguliwa na Mfalme wa Kiajemi Kisraa, alituma majumbe wawili kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumpelekea mwaliko. Wakati hao walipotokezea mbele ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), aliwaona hao wamenyoa ndevu na kufuga masharubu (ndevu za mdomo). Kwa hayo yeye alichukizwa kuwatazama hao (kwa sababu ya kuonekana visivyo sawa) na aliwaambia : "Ole wenu ! Je ni nani aliyewaambia kufanya hivyo ?" Wao walimjibu: "Bwana wetu! (wakimaanisha Kisraa)."
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia: "Lakini Mola wangu, aliye Mkuu
na Aliyetukuzwa, ameniamrisha mimi kuibakiza ndevu yangu peke yake na kunyoa masharubu yangu." [Imerekodiwa na Ibn Jarra-abar, na al-Albaaniy kuwa ni Hasan (nzuri) ]

2. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewaamrisha wanaume wafuge ndevu peke yake. Hadiyth zifuatazo pia zina maana hizi hizi : "Nyoeni masharubu na muziache ndevu".[Al-Bukhaariy na Muslim]

3. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:"Nyoeni masharubu yenu na muoteshe ndevu zenu. Muonekane tofauti na Wamajusi (wafuasi wa dini ya waabudu moto iliyokuwapo huko Uajemi [Iran]). [Muslim]

4. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nyoeni masharubu yenu na kuziacha ndevu zenu peke yake. Muwe tofauti na Ahlul Kitaab (Mayahudi na Manaswara)."[Muslim]

5. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muwe tofauti na Mushrikiyn, mnyoe masharubu yenu na kufuga ndevu" [Al-Bukhaariy na Muslim]

Kwa kifupi hizi ni dalili chache kuonyesha Uwajibu wa jambo hilo, na vilevile ni maarufu kuwa Maimam Abu Haniyfah, Maalik, Ash-Shaafi'iy, Ahmad bin Hanbal na wengineo wamesema ni HARAAM kunyoa ndevu.

Na kwa kufahamu kuwa jambo hilo ni baya na ni ukiukwaji wa sheria ambayo imetoka kwa Muumba na kuthibitishwa kimaelekezo na kivitendo kwetu na Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ndio Maimaam hao wakatoa maamuzi yao katika suala hilo.

Amiyr Muadilifu 'Umar ibn 'Abdul-'Aziyz inasemekana katika vyanzo vya kihistoria kuwa alikuwa hakubali katika utawala wake ushahidi wa mtu mwenye kunyoa ndevu! Vilevile tunaona kwenye madhehebu mbalimbali za Kiislam, haruhusiwi mtu kuswalisha ikiwa haweki ndevu kutokana na jinsi walivyofahamu uzito wa jambo hilo na Uwajibu wake.

Na ndevu ni mashavuni na kidevuni, unapaswa kufuga ndevu zote na si kidevuni pekee ambazo zaitwa mzuzu na ukanyoa za mashavuni; utakuwa unafanya makosa; zote hizo ni ndevu, ama zilizoko juu ya mdomo wa juu ambazo ni masharubu, hizo zatakiwa kupunguzwa
Hakika Mwenyezi Mungu Anajua Zaidi
 
saw mkuu
 
Back
Top Bottom