Unaalikwa outing wewe unakuja na "Twiga stars" ni sababu nyingine kwanini huolewi dada

TADPOLE

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
2,794
9,035
Sasa mbele ya kioo nilionekana very smart... Suruali yangu Pana Aina ya Kodak Bwanga ilinikaa vizuri kabisa, leo niliivalia kifuani, yaani mkanda umepita chini ya kwapa kiasi kwamba koromeo na Zipu ya suruwali vinagonga Cheers!

Shingoni Cheni ya chuma iliyopakwa Majivu ionekane ya Silver... mkononi Funguo ya Banda la Mbuzi yenye Holder ya Mercedes Benz! Mfukoni laki 2 za mauzo ya pikapu 4 za mbolea! Hivi anachomokaje kwa mfano!.. leo nitampata tu!..nasema nitampata!

When it comes to LOVE Ubishi ni Sayansi tu, nani anaweza kuubishia Moyo?... hakika sasa ni rasmi nimenasa. Huyu Rose ana kila kitu, ananifaa kwa Mapenzi, Mke, Urafiki na hata kuwa Mama wa Familia... Lakini ni vipi ataingia Mikononi?, huu kwangu ni mtihani mwingine! Je, vipi kuhusu Class yake na yangu? Hii nayo ni tofauti nyingine.,.. Trust Me nitampata!

Sasa wakati Nishamaliza kutupia Viwalo Niliyakumbuka tena maneno ya Rafiki yangu SALIMU BULICHEKA "Rose ni msichana wa Class ya juu na ndiye Miss Vyuo vikuu kwa sasa,..hivyo unapomfuata punguza maneno mengi kama unasali Rozari, funga domo kabisa na uache Wallet au ATM Card ziongee, hapo utampata!...lakini ukimpelekea kisura cha upole kama unaungama basi umemkosa...peleka pesa"

Ndipo nikanyanyua Simu na kupiga tena ile Namba niliyopewa na Salimu..0654 908...nikasikia inaita na kupokelewa!
"Rose tafadhali usikose kuja Pale Blue Pearl tuonane, kama ni Taxi chukua nitalipa....Kama ni Bata usijali utakula....kama ni shopping usijali utakwenda hata Paris....please njoo unisikilize Pedejee!"(Nilisisitiza)

Ndipo ilipofika 10:00 jioni nikawa tayari nimetulia kwenye Meza ya kwenye Kona kabisa pale Blue Pearl Hotel , wapi Rose?...mbona haji?....Nina dukuduku la Moyo,Tafadhali Rose njoo nikutemee madini ya Uranium!"

Baada ya Kama Nusu saa hivi ndipo nikaliona kundi la Wasichana kama 10 hivi likiingia pale Hotelini, mwanzo nilidhani ni Twiga Stars wapo Kambini kwa ajili ya Mechi na Zimbabwe lakini hapana!...mmoja kati yao ni Rose aisee...kwa kweli ni yeye,..sasa wakaja moja kwa Moja mpaka nilipokaa..,viti vikaongezwa..sasa hii ikawa sio DATE tena bali ni Mkutano wa Saccos ya Wamama na Mimi nikaonekana kama Baba Mshauri,..aisee Uso ulinishuka kama Farisayo anasujudu,..ndipo nikajitutumua na kusema "Hi Girls!'
"Hi Shem'' (Wakaitikia).

Daah Huyu Rose niliyezoea kumuona kwenye Magazine tu sasa alikaa kushoto kwangu ameniegemea,...Twiga Stars nao hawakuwa Nyuma, ukawa mchezo wa Bandika bandua pale Mezani,zikitua sahani za Vyuku basi zinaondoka sahani tupu za Mbuzi choma!....warembo wanakunywa Redbulls nyingi kana kwamba wana pambano la Wrestling!...Mama wee! ...yaani ni mwendo wa kuagiza kana kwambo wapo sabasaba kwenye Banda la Maonyesho ya Vyakula Duniani!.

Yale Mabusu ya Rose pale Mezani niliyapokea kinyonge kwa tabasamu la Maiti,..nilikuwa nimeishiwa pozi kabisa!....hii bili ya kwanza ilipokuja ilisoma 734,500 aisee nilipagawa!

Kuchungulia ndani ya Wallet yangu ilikuwa sawa tu na kuchungulia Mahabusu ...hakika leo nitatangazwa ITV....
Bili ya pili nayo ikaja tshs 540,000/=Twiga Stars hawana huruma Kabisa
...kumbuka bili ile ya kwanza bado ni Unpaid na sasa in Total ni 1,274,500/=

Sasa wazo la kuacha Nyoya ndio lilitawala Kichwa!...nikatoka kama naenda Toilet na sasa nikawa natambaa na Ukuta wa Hotel....Ghafla nikatandikwa Rungu nikazimia!.

Leo ni Siku ya tatu nimezindukia wodi ya Kibasila,...nasikia sauti ya mama yangu Mpendwa ikisema "Jamani mgonjwa amezinduka leteni hiyo Hot pot ya Maboga!" .....Nikazimia tena.

This was a joke but nimeelezea uhalisia wewe ni mwanamke someone kakuinvite outing ana maongezi na wewe why hubebe kijiji cha marafiki zako? kuna faragha hapo? kwano ukienda kumsikiliza kipi unapungukiwa.

Sometimes huwa mnasumbua wachungaji kwa ujinga wenu mnaouendekeza,huwezi jua labda mme wako mtarajiwa ndio Huyo ambae umemuendea na Twiga stars unafikiri atakua tena na wazo la kukuoa?

Unadhani atakuchukuliaje tena..mkibadilika itakuwa fresh sana
 
Kuna jamaa yangu juzi kaita demu wake mpya maeneo fulani,
Demu kaja na wacheza rede wenzie!
Tumia tumia za hapa na pale, demu kaondoka kimya kimya! Kamuachia wacheza rede wenzie.
Walioachwa nao bia imekolea, wakamwambia jamaa kuwa, mwenzao kaenda kwa kibopa fulani wa serikali. Ilimpasa aende!
Jamaa akiangalia, hapo katumia hela za kutosha kulisha familia yake milo mitatu kwa wiki nzima!
Kesho demu anamtumia sms eti "nisamehe beib"
... Will be back
 
Nitashangaa sana jamaa akiwa kamsamehe demu hahaha
 
Hivi hakunaga topic nyingine kabisa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaruhusiwa kuanzisha nyingine kama una wazo LA tofauti...Mimi nimeanzisha topic kwa lengo langu la kuelimisha na kuchekesha pia kwa atakayeona inachekesha,.......kitu kama hukipendi pita kimya so lazima kuleta kejeli zisizo na maana after all una heshima kubwa sana kutoka kwangu tusiharibiane Siku basi
 
unajua mwanamke kama autaki mualiko si ukatae tuu kuliko kumfanya mwenzako poyoyo mnakuja timu nzima shubamit
 
Unaruhusiwa kuanzisha nyingine kama una wazo LA tofauti...Mimi nimeanzisha topic kwa lengo langu la kuelimisha na kuchekesha pia kwa atakayeona inachekesha,.......kitu kama hukipendi pita kimya so lazima kuleta kejeli zisizo na maana after all una heshima kubwa sana kutoka kwangu tusiharibiane Siku basi
Hii kweli imekuwa too much, leo huu uzi ni wa tatu kuusoma unaozungumzia jambo hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa yangu juzi kaita demu wake mpya maeneo fulani,
Demu kaja na wacheza rede wenzie!
Tumia tumia za hapa na pale, demu kaondoka kimya kimya! Kamuachia wacheza rede wenzie.
Walioachwa nao bia imekolea, wakamwambia jamaa kuwa, mwenzao kaenda kwa kibopa fulani wa serikali. Ilimpasa aende!
Jamaa akiangalia, hapo katumia hela za kutosha kulisha familia yake milo mitatu kwa wiki nzima!
Kesho demu anamtumia sms eti "nisamehe beib"
... Will be back
Tatizo la vijana, wanatongoza mademu wauza uchi, demu hata akikupa namba ya Fanya mawasiliano hata kwa muda wa WK 2 huku ukimtega kwa maswali akijifanya anataka umsaidie fedha inakula kwako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom