Unaacha mumeo unakwenda kudandia mume wa mwanamke mwenzako...Ebo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaacha mumeo unakwenda kudandia mume wa mwanamke mwenzako...Ebo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, May 10, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  Mpenzi msomaji, yapo matukio mengine ukisimuliwa unabaki unajiuliza maswali kibao. Unaona kabisa kwamba ni jambo lisilowezekana, lakini kwa wengine linawezekana kabisa. Hebu sikia kituko kifuatacho ambacho nilipenda sana nikumegee.
  Hivi majuzi nilimtembelea mama mmoja rafiki yangu kwa majadiliano kuhusu miradi fulani ya kujiendeleza. Katikati ya mazungumzo, akaja kaka yake mmoja kumpasha habari fulani ya kifamilia.
  Kaka huyo mcheshi akawa anamweleza dada yake kituko fulani ambacho kwa makini nilikisikiliza kwa kuwa kiligonga eneo ninalopenda kuchambua katika safu hii ya Maisha Ndivyo Yalivyo.
  Kaka huyo akasema kuwa yupo jamaa yao mmoja aliyeachwa na mke katika mazingira tatanishi, lakini mke huyu akaenda kuparamia mwanaume mwingine ambaye ni mume wa mtu. Jamaa huyu ambaye alifunga ndoa ya nguvu na kubahatika kupata mtoto mmoja, hivi sasa anahaha mke amrejee bila mafanikio. Unajua nini kimetokea?
  Kwa mujibu wa maelezo ya kaka huyo, mwanamama huyo inasemekana amemtosa mumewe kutokana na hali ngumu ya kiuchumi ndani ya familia yao. Mama huyo akaamua kwenda kutafuta kazi ya kuuza dukani ambapo alipata maeneo ya Kariakoo.
  Katika kutekeleza majukumu yake, mmiliki wa duka akamhusudu na kujenga mahusiano ya kirafiki. Hali hiyo iliendelea kwa muda hata kufikia hatua mke wa mwenye duka hilo akagundua mahusiano hayo.
  Siku moja akatinga dukani na kuamuru mumewe amfukuze bibie huyo. Hata hivyo, baba mwenye duka alikuja juu na kukataa. Lakini hali ya vitisho ikaendelea kuwa tete, hivyo baba wa duka akaamua kumuondoa bibie yule pale dukani.
  Pamoja na uamuzi huo, akaamua kwenda kumtafutia sehemu nyingine ya biashara. Akampatia fremu ya duka eneo la Mwenge Jijini Dar es Salaam na kumwanzishia duka lake. Akalijaza vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na soda baridi na vitafunwa.
  Kila ifikapo mwisho wa mwezi, baba huyo hufika dukani na kuonyesha mahesabu, kasha kuchukua fungu lake na kumbakishia bibie fungu lake. Ni moja ya maduka yanayochanganya kwa mauzo eneo hilo.
  Kutokana na maendeleo mazuri kibiashara ya mwanadada huyo, imefikia hatua sasa hata kuonekana hadharani akiwa na mzee wake huyo aliyemfadhili siyo kitu cha ajabu. Hata mke wa mzee huyo anapowakuta wawili hao wamekaa mahali wanapata kinywaji hafurukuti kwa kuwa mzee alishamwambia bayana kuwa huyo ni mke mwenzake.
  Kinachoshangaza wapambe ni kwamba mzee anagÂ’angÂ’ania huyo ni mke wa pili lakini mwenye mke bado anatafuta njia ya kurejeana na mkewe. Haifahamiki mchezo huu mwisho wake utakuwaje. Upo hapo msomaji wangu? Ama kwa hakika Maisha Ndivyo Yalivyo.
  Kituko hiki kinatuonyesha jinsi watu wasivyotosheka na kile walichochagua wenyewe, wakati mwingine kwa ahadi mbele ya viongozi wa dini zao. Kama siyo kumdanganya Muumba wetu ni kitu gani? Hizi tabia za kutamani vya wengine zinasababishwa na nini?
  Binafsi nafikiria yafuatayo: Umasikini/Ufukara na Mali/Utajiri. Vitu hivi viwili ni miongoni mwa vile vilivyochangia sana nyufa ndani ya nyumba zetu. Vimechangia sana familia zilizojengeka juu ya msingi imara wa maisha, zikabomoka au kusambaratika vibaya.
  Wapo watu waliooana wakiwa na uwezo wa kawaida kwa maana ya kipato cha kawaida, mfano mjasiriamali. Wakaendesha biashara fulani kwa lengo la kusonga mbele kimafanikio. Wapo waliojenga dhamira ya pamoja kama mke na mume na kufanikiwa kweli kweli. Lakini wapo ambao mmoja alikuwa kikwazo kwa mwenzake. Huyu anataka wasonge mbele lakini mwenzake anamkwamisha.
  Kwa mfano mama anasimamia biashara, inakwenda vizuri lakini baba anamega mapato na kwenda kugida machicha. Au mama anachepuka na kuzungusha raundi kwa washikaji zake. Mambo ya aina hii yamesababisha umasikini kwa familia kutosonga mbele kimaendeleo na kudumaa kimaisha.
  Matokeo yake, watu wa aina hii ndio hao wengine huchepuka na kutafuta mahusiano mengine ya pembezoni ili kuondokana na uduni wa maisha. Je, hawa ile ahadi ya kuishi kwa shida na raha wanaitekeleza au ni unafiki uliokubuhu? Naam.
  Wengine mali au utajiri huwatia uwendawazimu. Mtu anapojiona na mali nyingi au fedha nyingi basi huanza kupata mawazo tawanyishi na kuanza kuzitapanya kwa kuanzisha mahusiano mengine nje ya nyumba zao.
  Kwa mfano baba yule niliyemzungumzia hapo juu, tayari ana mke mzuri na watoto wake na wajukuu. Pia anazo nyumba tatu za kupangisha na maduka kadhaa. Lakini bado anatafuta nyumba ndogo. Na kibaya zaidi anamendea wake za wanaume wenzake. Kisa ni jeuri ya utajiri alionao.
  Maisha ya aina hii ni hatari sana. Yafaa watu wajirudi na waheshimu nyumba zao. Wanapaswa kutumia kile wanachopata kwa uangalifu na haki pasipo kukwaza wengine. Maisha Ndivyo Yalivyo.
  Hizi tamaa za hapa na pale mara zote zimeishia kuleta maafa ya kujitakia. Ukifanikiwa basi mafanikio yale yanufaishe familia yako na siyo kutapanya pasipo mpangilio. Kwa wale wanaojiona fukara au masikini wasikate tamaa kwani kwa kujishughulisha hakuna kisichowezekana mbele za Mungu.
  Kwa leo msomaji wangu niachie hapa na kama unayo maoni au ushauri usisite kuniandikia kupitia email ifuatayo;
  fwingia@yahoo.com
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. n

  nndondo JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  mbona hichi dada flora wala sio kisa ni hali halisi? kwa hiyo huyo mume wa bibie alitegemea mkewe aendelee kukumbatia umaskini wakati opportunity imejilengesha? tuwe wakweli ni ubora kawa wazi kuliko angekua anaiba kinafiki, pili hiki kisa kina mapungufu maana hakituelezi huyo mume anafanya nini kubadilisha maisha yake yawe bora ili walau labda mkewe aone mabadiliko analilia penzi tu mbona mambo ya kizamani?
   
 3. T

  Tall JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Unajuaje?inawezekana mara ya kwanza mwanamke alidanganywa kuwa jamaa yupo single/hana mtu kumbe..........
   
Loading...