Una tatizo la panya nyumbani kwako ,suluhisho ni NYOKA tu ndani ya wiki panya wote watakimbia

Achana na hao wazungu Tupe picha ya nyoka unayemfuga kwako mkuu
Karibu

f02a705996e67941bc61acba65d2aef7.jpg
 
Hili tata tamanika, ka Magufuli na Acacia
Dili hasa makanika sifuri kuambulia
Toa panya weka nyoka, kufanya nachoka
Kukanya seleka toka, mke utapokwa
Nyoka mwenye makengeza, mtafuta fedha
Chenge hajui gereza, usitake kugeza
Sio nabeza naweza kucheza na mistari
Na jedwali,jemadari wa awali, kaambali na ajali
Miamala ya msafara, yatafutiwa kafara
Kwa mikwala ya hekaya kuliko za Jakaya
Na hata kina Kigwangalla,wamepigwa ngwala
Seuze kapuku aliyoksa hata gwala?
Shari tushanunua, kwa bei rahisi
Watu wanapumua na kushangilia raisi
Makufuli funga, swaumu ka Ramadhani
Maigizo dunga kwa hisani ya wapinzani
Dili matata, kiazimbatata, wanaume wa Dar
Wakili nanata, ujanja kupata si kushinda bar
Kalamu naweka chini kwa mtindo wa Andanenga
Kaditama naadhini, nyoka bado kulenga

Daah!
 
Mkuu tunawapata vipi hawa nyoka???!!!Hivi kuna eneo lenye panya wengi kama Kigogo kwa hapa dsm??
 
Fleemason huyu Freemason huyu kwa hapa bongo ndio litageuka jina lako not in bongo uswahilini watakuita kwa lafudhi zote kikurya na kisambaa mkuuu hawawezi kuelewa!
 
Mimi ilinichukua week moja tu kumaliza tatizo la panya,baada ya miaka mingi ya kutumia sumu za panya,mitego,paka na hata theorem ya kuhakikisha usafi na kuwa na vitu vichache ndani.
Siku moja kuna mtundu akanielekeza niwatege kwa kuwachanganyia unga unga wa indomethacin capsule (Indocid) kwenye unga unga wa dagaa kavu.nakumbuka nilichukua dagaa kama kiganja cha mkono na kuchanganya na unga wa capsules mbili za indocid.Ajabu asubuhi nilikuta panya kama wanne hivi wamekufa na sikuwahi kuona panya tena hom kwangu huu mwaka wa tano, mwanzoni nilipoambiwa nilidharau nikajaribu kwa shingo upande na ndiyo iliyosolve. Ni Indocid ile ile ambayo hutumika kama pain killer ambayo watu wa medical wameiweka kwenye group la NSAID (Non Steroidal Antiinflamatory Drug)

Najiuliza chatu mdogo siku akikua panya hawatamtosha kwa shibe na atatumeza mmoja baada ya mwingine mwishowe mtaa utamalizika.
 
Sio bure kuna kalaana kanatunyemelea! Mada za nyoka zinaongezeka sana, mmoja alikuja na kilimo cha nyoka na wewe unakuja na kuzuia panya kwa kutumia nyoka bila kutuambia paka wameenda wapi. Kwa mujibu wa kitabu kitakatifu, nyoka ni adui wa binadamu, wewe unaleta ushosti na nyoka.
Acha fikra potofu mkuu
 
undefine nakushauri anzisha biashara ya kuuza nyoka alafu ndiyo uje na hili bandiko kutushawishi tutakuunga mkono kwa vitendo
Haa sawa ushauri wako nauchukua ila hii bandiko ni kuangalia muitikio ya watu upo vipi

Ntakutafuta uwe mteja wangu wa kwanza na nitakupa na nyongeza za nyoka bure kama karama kwako ww
 
Nb:Hii ni njia rahisi kutokomeza panya fanya experiment kama nyumba yako ina panya wengi chukua nyoka wa aina hii muweke wiki tu hakika panya wote watakimbilia nyumba ya jirani na baada ya hapo mrudishe nyoka kwake .[/IMG]

[
nyoka ukisha mleta kwako, kwako ndio panakuwa kwake. Naye ataenda kumleta demu wake.Watazaana hadi ukoje.
Na huo ndio mwanzo wa kuwa mchawi
 
Nimesoma mada mpaka mwili umesisimka.Fanya fanya paaa..ukajua umefuga Chatu mtoto halafu kumbe likiumbe..dubwana linakuaa na humo humo ndani unaliona kwa Manati.Hao wazungu waachane kama walivyo.
 
Thubutu eti nifuge nyoka weeeeeeee....hakuna mdudu nisiempenda katika maisha yangu kama nyoka lohhhh! Hao panya wataisha kwa sumu tu kudadekiii!
 
Back
Top Bottom