Una tatizo la panya nyumbani kwako? Dawa hii hapa

Traveller X

JF-Expert Member
May 2, 2017
271
500
Kama kwako unatatizo la panya basi wala usihangaike kwenda kununua ma sumu ambayo mwisho wake panya anafia pasipojulikana na harufu ya panya aliyekufa kujaa nyumba nzima, jaribu kutengeneza mitego hii rahisi sana ambayo utawadaka wakutosha tu, Jaribu alafu uje unipe matokeo, mi nishadaka kama 8 usiku wa jana.


 

Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
334
250
Nashukuru kwa hiyo information ya indocid nitaifanyia kazi.manaake mimi nilitumia trick ya kurekodi sauti za paka kwenye simu yangu waziogopa siku ya kwanza baadae wakagundua kuwa siyo paka kumbe paka akitoa sauti inakuwa kwenye frequency fulani ambazo panya wanazifahamu tofauti na zile ya kurekodiwa.
 

Friday Malafyale

JF-Expert Member
Jan 18, 2017
1,390
2,000
Hii mada imenikuta siku haswaa, leo hii siwezi kulala chumbani kwa sababu panya kafia huko na kuna harufu sana toka jioni, nafika toka kazini mke wangu ananiambia kuna harufu ya panya lakini kaangalia hajaona chochote imenibidi kulala sebuleni kwenye viti na familia ntafanyaje mie malafyale... But ntajaribu hiyo
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,198
2,000
Tumia endosine una I changanya na dagaa au Samaki Panya hatoboi
Mkuu endosine ama endocid?
Maana hiyo dawa ni ya kutulizia maumivu ya nyonga ama mifupa ya binadamu.
Dawa hii kwa panya haina mbadala. Unga wa dawa hiyo hauna harufu ya kufukuza panya. Kwa hiyo unachanganya na unga wa sembe ama dagaa unavyosema.
Watakufa hadi utaona kinyaa.
 

muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
11,251
2,000
Hii mada imenikuta siku haswaa, leo hii siwezi kulala chumbani kwa sababu panya kafia huko na kuna harufu sana toka jioni, nafika toka kazini mke wangu ananiambia kuna harufu ya panya lakini kaangalia hajaona chochote imenibidi kulala sebuleni kwenye viti na familia ntafanyaje mie malafyale... But ntajaribu hiyo
Vaa ujasiri,nenda kapangue vitanda na makochi umtoe huyo panya...ukichelewa zaidi si ndiyo anazidi kuoza mkuu?...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom