Una swaga sana au mwenyewe tu alishakuelewa

Daniel Adrian

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
311
322
Habari za siku ya leo.

Leo nataka niwaambie jambo moja wanaume wenzangu. Hata hivyo mada ni huru na yeyote anaruhusiwa kuchangia.

"ukiona mwanamke amekukubali ujue yeye mwenyewe tu amekutamani (nashindwa kusema amekupenda kwa sababu upendo ni jambo zito kidogo lisilotokea immediately) na sio kwamba una swaga sana".

Kwanini nasema hivyo ?

Ushawahi kumtongoza mwanamke asie kutaka ?

Mimi nishawahi, nakwambia ni rahisi zaidi kwenda sayari ya Mars kuliko kutongoza mwanamke asiekutaka, "hataki kusikia wala kuelewa chochote". Kwahiyo tegemea kukatishwa katishwa na kupotezwa mada. Tena siku hizi wana mbinu mpya, atajifanya kummiss bwana ake atachukua simu atajichatisha vineno vya kimahaba halafu ataiweka vizuri na we ukichungulia uone. Atajifanya yuko busy na simu yake. Lengo hapa akuoneshe tu "sikutaki".

Sasa unakutana na mwanamke unamtongoza anakusikiliza, unamdanganya anasikiliza tu, unamwambia maneno ya chumbani anakuskiliza tu. Anasubiri uongee mpaka umalize. Halafu akija kukukubali unajisifu nna swagaa. Una swaga au naye alikutamani ?

Kwanza mimi sijawahi elewa maana ya neno swaga maana, mimi naweza mtongoza mwanamke kwa maneno yanayohesabika na akaelewa, "akakubali". Sasa hizo swaga tena saa ngapi ?

Sasa mi nataka kukwambia, sio swaga. Kilichofanya akubali ni hata yeye alishakutamani. Naweza kukuthibitishia kama kama hakutaki hizo swaga hazitofanya kazi.

Sijasema kwa nia mbaya. Nime-share uzoefu wangu tu kwa kaka na wadogo zangu wa kiume hapa JF

Halafu ladies,I am single man.(tangazo?, Hapana utani tu. Mmmhhh utani au kweli ?).

Kabla sijaweka nukta ya mwisho napenda kuwashukuru kwa kusoma hii post ila niwakumbushe kuwa "Leo bubu kasema". Mimi ni msomaji wa muda mrefu humu kwahiyo naishi kama bubu, sasa nikiamua kusema ujue nilichosema kina uzito, usipuuze.
 
Si hizi hawakukatai ila utapigwa bomu hilo wewe mwenyewe utaelewa kuwa hutakiwi.
Atakwambia sawa. Baada ya dakk kadhaa simu yake itatumbukia kwenye maji. Ni ww ndio ukanunue mpya. Kodi ya anakoisha kesho itaisha ni ww ndio umlipie. Broo mbona utasepa bila kuaga.😀
 
Mwanamke ukimtongoza na akakukataa ujue kakuthaminisha wewe na huyo alienane kwa wakati huo (kwa vipimo vyake anavyojua yeye) na mwishowe akakuona fala tu

Vilevile akikukubali, ni vile kuna baadhi ya vitu ameona umemzidi mtu wake.

Kwa hiyo masuala ya swagga sijui nini hayana umuhimu, kikubwa tujipandishe thamani kila siku.
 
Ulichoongea ni kweli labda niongezee in brief!

1. Mwanamke atakukubalia ikiwa una mvuto zaidi ya bwana alie nae, meaning kuna vitu vya dhahiri ambavyo huwa vinamvutia kwa mwanaume na bwana wake hana...Yaweza kuwa u smart kimuonekano, possesions kama gari, na level of confidence na namna unavyoongea.

2.Endapo akiwa single kwa muda na ana uhitaji wa kuwa na mtu, au hayupo in good terms na mtu aliye nae na anakosa peace of mind hivyo anatafuta pa kupumzikia.

Mara nyingi ukimuingia mwanamke ukamkuta yuko katika hizo situations ndio chap unakubaliwa af unaeza ukajihisi mwamba kumbe "Opportunity met preparation"
 
Luck is when opportunity meets preparation. Wao ndio waamuzi wa mwisho tusijimwambafy kwakweli
 
Back
Top Bottom