Una ndoto ya kwenda kusoma Chuo kikuu Cha Harvard? Fanya haya

Mama Edina

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
747
1,814
Uwe na IQ ya kutosha maana Harvard si pa mchezo kama udsm...Hapana.
Screenshot_20230206-162810.jpg

Pale Harvard Kuna wakati IQ yako haifai chochote. Haijalishi una IQ ya 125, 135, 145, 155, 165, au 175. Vyuo vikuu vya wasomi vinataka kusajili wanafunzi walio na rekodi za mambo ambazo zinaonyesha kuwa wao ni aina ya watu ambao watafanukisha jambo fulani.

Harvard wanatafuta wanafunzi wanaofanya vizuri kitaaluma. Ikiwa unataka kuingia katika chuo kikuu cha wasomi, unapaswa kuchukua mtaala mgumu kama wao unaotolewa na shule hiyo na uwe umepata alama bora. Wanatafuta wanafunzi ambao alama zao za mtihani sanifu zinaonyesha kuwa wamejiandaa kimasomo kufanya vyema katika chuo kikuu Kwa Muda wa miaka minne. Harvard mlango utakaoingilia sio utakaotokea.

Hawa watu wa Harvard ni wanasayansi, sio ka mwalimu mwalimu kawanakoweza kukupa degree ya pichu. wale wababa na wamama scientist.

Wanadahili wanafunzi wanaoweza kujitegemea, wanafunzi ambao wanavutiwa na ulimwengu unaowazunguka, Wanatafuta wanafunzi wanaochangia jamii zao, wanafunzi wenye uwezo wa uongozi, wanafunzi walio na rekodi zinazoonyesha kujitolea na ubora wa mitazamo yao
 
Kila kimoja kina ubora kwenye angle yake..
Ila dunia ya sasa ni bora MIT maana wame specialize kwelikweli harvard wao wana course nyingi mpaka kero chuo kama kijiji bana law,engineering, medicine,political science, uwanasayansi yaani ni mchanganyiko

Uzuri wa MIT kipo focused kwenye technology hasa hasa full nondo mkuuu
 
Chuo ambacho kilikuwa kinanitoa udendaa.. kwa marekani ni Stanford University basi.. ila ndio ivyo nimeishia kusoma zangu TEKU tu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Teofilo Kisanji University, nimepiga zangu pale Human Resource Management, ila paka leo mie mwenyewe sijaajiliwa na sina wa kumuajiri πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Taabu sana- Mbeyaa moyaa
Duuuh vyuo vingine bana vinachekesha kuna mdau huku alininanga kuniambia eti nimefeli
A level nimetupwa TEKU nikasema basi chuo kina CV chafu hiki

Ila mkuu ulimaliza mwaka gani?

Haujutii kupoteza muda wako?

πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ˜΅
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… toka 2010 mkuu.. sina cha kujutia napambana na hali yangu tu.. ukidondoka usikae , nyanyuka songa mbele.. ila nina degeree langu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… ni kurogana tu basi sasa hivi huku kitaa
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… toka 2010 mkuu.. sina cha kujutia napambana na hali yangu tu.. ukidondoka usikae , nyanyuka songa mbele.. ila nina degeree langu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… ni kurogana tu basi sasa hivi huku kitaa
Duuh naomba Mungu haya maisha yanipiteeee mbali kabisa

Ila sawa mkuu all de best πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ na huko kulogAna
 
Back
Top Bottom