Una ndoto gani unayotamani kuitimiza mwaka 2023?

trudie

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
3,334
7,655
Heri ya mwaka mpya wana JF wote. Tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuuanza mwaka mpya 2023 sifa na utukufu tunamrudishia yeye.

Tukiwa tumeanza siku mpya ya mwaka siku ya kwanza, ni siku ya kupanga malengo yako na ndoto unazotamani au unazotarajia kuzifikia na kukamilisha kwa mwaka mzima. Pia ni siku ya kuangalia ambayo hukukamilisha kwa mwaka uliopita na kuyapa kipaumbele mwaka huu.

Ni siku ya kuevaluate wapi ulikosea na wapi ulianguka kwa mwaka 2022 ili uyasahihishe na kuepuka kurudia mwaka mpya yasizibe malengo yako.

~ Je, umeshaandika malengo yako ya kuyafikia mwaka huu kwa miezi 6 na 12 ijayo?

~ Je, ni ndoto gani unatamani itimie kwa mwaka huu? Unatamani ufikie malengo yapi kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu?

Mimi binafsi namuomba sana mwenyezi Mungu mwaka huu;
1. Nipate kazi nzuri itakayomudu maisha yangu. Nipate pia connection za kutosha.
2. Nitengeneze cycle mpya ya marafiki ambao tutasaidiana kimawazo na kimaisha katika shida na raha na mengine mengi sana ambayo nimetulia nayaandika katika diary hapa.

Wewe je unatamani Mungu akutimizie nini kwa mwaka huu 2023? Mungu wetu siyo kiziwi wala kipofu, anasikia na kuona.

Heri ya mwaka mpya ukawe mwaka wa furaha, amani na mafanikio tele.


20230101_114907.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila la heri mkuu, binafsi namuomba Mungu anijalie afya njema na mipango yangu ya 2023 itekelezeke, awafungulie milango ya baraka na mafanikio wote wanaopambana kuboresha maisha yao na familia zao.
Herini ya mwaka mpya wakuu.
Glory to God.
Amina na Mungu aweke mkono wake wa baraka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haitakiwi mtu yoyote kujua mipango yangu hata mke wangu. Siri sirini
Kuna watu wana midomo mibaya sana. Ukisema jambo halitimii.
Kimya kimya sasa hivi hakuna kutoa code kwa watu.
Ni kweli kabisa mkuu kuna watu wana midomo mibaya kufanya ndoto isitimie. Ila pia kuna wengine wana baraka wanaweza kuwa lango la kufikia ndoto yako. Maisha yana siri kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom