N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 6,825
- 9,532
Nadhani ujenzi imekuwa kasumba hapa Tanzania, kila mtu ukikutana nae eti, bado hujajenga? ni maswali sawa na yale ya bado hujaoa? ....E bwana ee tusipangiane nikimbilie kujenga na ka milioni 50 halafu baada ya hapo narudi kuwa mkata ufuta na kuyaona maisha machungu, ooh noo! , better nitafakari namna bora ya kuizungusha hiyo pesa kwingineko lakini sio kujenga tena uswazi iwe kivyovyote kuishi au kupangisha,hakuna future kwenye ujenzi kama hujajijenga kimaisha hapa Tanzania, ,...fungua akili fikiria kutengeneza pesa kwanza ndipo ujenge...kodi ya nyumba wala sio kitisho usiitumie kama kisingizio...Hili povu nimelimwaga kuna kiumbe ananiulizauliza kila siku unajenga lini...Nikamjibu kobe ana nyumba anatembea nayo...