Una Milioni 50 na hujawahi kuzishika eti unawekeza kwenye nyumba

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,824
9,521
Nadhani ujenzi imekuwa kasumba hapa Tanzania, kila mtu ukikutana nae eti, bado hujajenga? ni maswali sawa na yale ya bado hujaoa? ....E bwana ee tusipangiane nikimbilie kujenga na ka milioni 50 halafu baada ya hapo narudi kuwa mkata ufuta na kuyaona maisha machungu, ooh noo! , better nitafakari namna bora ya kuizungusha hiyo pesa kwingineko lakini sio kujenga tena uswazi iwe kivyovyote kuishi au kupangisha,hakuna future kwenye ujenzi kama hujajijenga kimaisha hapa Tanzania, ,...fungua akili fikiria kutengeneza pesa kwanza ndipo ujenge...kodi ya nyumba wala sio kitisho usiitumie kama kisingizio...Hili povu nimelimwaga kuna kiumbe ananiulizauliza kila siku unajenga lini...Nikamjibu kobe ana nyumba anatembea nayo...
 
Swala ni pesa tu. ..kama unaishi kwako au umepanga siyo tija sana. ..mipango ya maisha tu.
Wengi tunakimbilia kibanda kujenga kwa sababu ya income isiyo eleweka, ambapo tunaona ukiwa na kibanda utakuwa unawaza kusomesha watoto na shida nyingine ndogo ndogo... Pia lifestyle ina changia maana kuna watu wanakufa hata choo ajawahi kujenga
 
Watu wote wangekuwa na Mawazo Kama yako Leo hii Wewe ungepanga wapi?

Wewe Fanya Biashara zako tutakuja kununua Mchana Jioni ukirudi unanilipa kodi ya nyumba ili Kesho nije tena kukuungisha Biashara yako ndio Mgawanyiko wa Najukumu
 
Mimi binafsi sijengi kwasababu sikuja duniani kuipendezesha dunia.
;););)
Sema pesa huna mku amna kitu kizuri kama kuwa na kwako hata dini yetu [HASHTAG]#Islam[/HASHTAG] inazungumzia swala hilo hata sisi tunaitaj kujenga ila pesa haija ka sawa
 
Sasa kama huna idea yoyote ya biashara na huna uzoefu nasio mla bata mjini hapa Mara 100 ujenge tu
Mkuu fursa sio biashara tu, tatizo wengi wetu Tanzania tunaigana kila mtu anawaza kujenga tumekuwa waoga sana matokeo yake tunaishi maisha ya kimaskini sana huku tukinyanyaswa na vimishahara vya mbuzi huku tukijifariji eti natokea kwangu...hadi tunaita "kwenye kibanda changu" hii mentality inatufanya kuishi maisha ya taabu sana sababu ya kukosa vipaumbele,binafsi siamini kama nyumba aka kibanda ndo kipaumbele, pesa kwanza kujenga NYUMBA sio KIBANDA kutafuata kwenye eneo rasmi...no wonder kila siku watu wanalia bomoabomoa
 
Watu wote wangekuwa na Mawazo Kama yako Leo hii Wewe ungepanga wapi?

Wewe Fanya Biashara zako tutakuja kununua Mchana Jioni ukirudi unanilipa kodi ya nyumba ili Kesho nije tena kukuungisha Biashara yako ndio Mgawanyiko wa Najukumu
Ni kweli mkuu na hiyo ndo ikolojia yenyewe ya maisha jengeni wapangaji tupo...nakulipa kodi ya nyumba miaka miwili unakula hiyo hela within a month halafu tunakodoleana macho hadi miaka miwili iishe kkk.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom