Una Maoni Gani Kuhusu TECNO, Bajeti Yako na Namna Ulivyoanza Kutumia Smartphone

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Hello wadau! Ikiwa imebaki wiki moja tuumalize mwezi Januari, leo tujadiliane kitu kimoja. Kwa namna moja ama nyingine simu zetu za TECNO zimekuwa na watumiaji wengi sana Tanzania. Huku ikionesha kuwa asilimia kubwa ya watu walioanza kutumia smartphone kwa mara ya kwanza kulingana na tafiti zetu walianza na TECNO. Walioanza na TECNO bado wanaendelea nazo na wanaendelea kubadilisha kuendana na fasheni za matoleo mbalimbali.

Kwa upande wako TECNO imekusaidiaje kwenye uchumi na bajeti yako na wakati huohuo ukaingia katika ulimwengu wa mtandao?
 
Kinachonifanya nitumie TECNO ni utunzaji wake wa chaji, ila huwa siitumii zaidi ya miezi 8 huwa nabadilisha...Maana haikawii kupiga alarms bila kuicomand mtumiaji, au utashangaa tu ipo mfukoni inapiga mziki! Pia mtu kakupigia una slide kupokea imestack mpka uzime uwashe tena ndio inakaa sawa.

Ni hayo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kiboko ya zote kwa chaji L9

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru kwanza kutoka kwenye hiyo kampuni yenu ama hakika wengi walianza huko kabla ya kuhamia makampuni mengine.

Simu zenu hupungua ubora kadri muda unavyoenda kuanzia camera, speed na mambo mengine.

Kingine tunajua kuwa nyie ni kampuni bora kuliko Samsung, IPhone, Oppo na Nokia ila jitahidini kupunguza uzalishaji siyo kila baada ya siku mbili mnatoa simu mpya. Mtoto hajatembea mke ana mimba, huku mwingine ananyonya aiseee. Tumieni uzazi wa mpango kwenye uzalishaji wa bidhaa zenu hii inafanya muonekane bidhaa zenu hazina ubora au mnaziondoa sokoni mapema.

Kwani mkikaa miezi 9 bila kutengeneza simu nyingine mnajisiaje?
 
Tecno ni sawa na ile huduma ya kimboka, uwanja wa fisi, mwananyamala temeke nk. Yaani unatumia kwa sababu ya shida tu.
Simu gani mtu anakupigia halafu yenyewe inajifikiria kwanza ndio inaanza kuita!

God doesn't require us to succeed,he only requires that you try
 
Tecno hii hii ambayo ukiweka ukifungua meseji inaleta camera?
Ukiweka mezani unakuta ili piga na kutuma sms?

Yote kwa Yote! Nyie ni wakombozi mmefanya hata makabwela tumiriki smartphone.

Kama mtakuja kutoa simu inayokaa na chaji kama tecno L8 mniambie hata kama inauzwa milioni ntakuja kununua! Hii simu kiboko.

Ilikuwa inakaa na moto siku ngapi?
 
Tecno shida yake moja ambayo nlikataa watu waliponambi but nkaja thibitisha,.Ukiiweka mfukoni bila kuzma data utajuta,itafanya mambo ya ajabu kwa sekund chache , kujipiga kwa simu,text itawatumia watu wa 3,itajiunga wifi yenyewd yan hz sm n shida ase
 
Tecno ni sawa na ile huduma ya kimboka, uwanja wa fisi, mwananyamala temeke nk. Yaani unatumia kwa sababu ya shida tu.
Simu gani mtu anakupigia halafu yenyewe inajifikiria kwanza ndio inaanza kuita!
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom