blogmaster
Senior Member
- Aug 15, 2015
- 167
- 74
Kama umepakua programu ya QuickTime kutoka Apple kwenye kompyuta yako ya Windows unashuriwa kuiondoa mara moja
Watafiti mbalimbali wa mambo ya kiusalama wa kimitandao wamegundua ni rahisi sana programu hiyo kutumika kuvamia data za kompyuta zako kwa sasa.
Tayari Apple walishatangaza kuacha kutoa updates kwa programu yao hiyo ambayo mara nyingi ilikuwa inakuja moja kwa moja pale unapotaka kupakua programu ya iTunes.
Ingawa programu ya QuickTimes bado inaendelea kuwa na uwezo wa kufanya kazi ila ina ubovu wa kiusalama (security vulnerabilities) ambao ni hatari kwa data zilizo kwenye kompyuta yako
kama una programu hiyo fuata hatua hizi kuiondoa kwenye kompyuta yako
KWA WATUMIAJI WA WINDOW 10
- Bonyeza start
- Chagua Setting
- Chagua ‘System’ na nenda eneo la ‘Apps and features’
- tafuta QuickTimes kwenye orodha na kisha bofya ‘Uninstall’
- Bonyeza Start
- Chagua ‘Control panel’
- Chagua ‘programs’ na kisha chagua na kubofya ‘Programs and Features’
- Tafuta QuickTimes kwenye orodha na kisha bonyeza ‘Uninstall’