Una cheti nina mume

Wewe baki na mume yeye abaki na cheti ...mwisho wa season ndo utajua ....wewe utabaki na watoto mume ataenda kwa mwenye cheti
 
Wanangu kusoma shule nzuri tu ndio linakushuka shuuuuu! Kumbuka anayesomesha wanangu ndiye aliyesomesha wanao, ni baba yao. Hawa watoto ni ndugu, acha roho mbaya.
Mume mwenyewe ulikuwa unamuona boya. Nimemchukua nimemtunza kapendeza sasa ndio unakumbuka ulikuwa umeolewa. Kaa na cheti chako umechelewa stendi.....Pole weeeee!
Eti urithi? Unazungumzia urithi wa mtu ambaye yuko hai na anatimiza majukumu yote mpaka yale uliyosema hawezi hapa kwangu mbona anatimiza. Hujioni una matatizo?
Kwa taarifa yako wanangu hawahitaji urithi wako na wala hawana sababu ya kugombana na ndugu zao. Nilivyo navyo vinanitosha sana na nimeridhika sina tamaa kama za kwako.
Kama ulivyosikia kuwa baba yao kawanunulia viwanja ni kweli hati ziko hapa kwangu. Sijamzuia asiwanunulie hao wa kwako.
Eti gari kistaleti changu tu ndio unapiga domo kila siku kwa mashoga zako sasa kama na wewe ulitaka kununuliwa si ungemwambia akununulie. Mbona una magari au hayo hajakununulia? Kwa hiyo unaona wivu kuwa wewe umejinunulia magari lakini mimi kaninunulia. Tuliza mshono bibiye. Kwa taarifa yako gari nimenunua mwenyewe kwa biashara zangu. Ni kweli kanipa mtaji lakini biashara nimefanya mwenyewe kwa juhudi zangu. Umeshakuwa mtu mzima sasa tulia sasa usubiri wajukuu
Sisi ni familia moja sasa upende usipende. Watoto wetu ni ndugu na wanajuana. Jiheshimu uheshimiwe.
Daaah!
 
Natamani Sana ungesoma mkasa wa naipenda jmosi yangu unaoandikwa na Irene mbowe

Kuna maneno Fulani huwa nayapenda Sana anakwambia kahaba ni shimo ndefu

Kwako Dada uliyeandikiwa huu ujumbe naamini upo humu Ila mtafute Sana Mungu ,mbingu zinakujua Kama mke halali hata Kama danga limekupokonya usilie usimrushie vijembe ,lilia magotini omba Sana Kuna majibu ya kila chozi

Kwako mwanaume uliyechepuka na kuacha mke anasutwa huku karma is near

Ujumbe wenu: Mbingu hutaiona otherwise umebadilika na kutubu machozi ya mwanamke mwenzio hayataenda bure miaka itapita lakini lazima Mungu atalipa kwa namna usiyojua


#Huu ugomvi nimetamani uwe wangu Mana ningeupangua spiritual Mimi Ni mwanamke naelewa maumivu ya ndoa

mi minyukano ya hivi naipenda ni usiku namnyuka huyu mpango wa kando mpaka arudi kuniomba samahani
 
Aseee nimeenda kumfyukunyua huko doooooh huyu mtu ni mshari mnooo.... Ana kazi haswa but Nampa pole hata huyo mwanaume aliyejitoa mhanga
Vingine "vinakatikia" tu dada angu wala sio mipango.unaogopa kuongeza dhambi ya kuua kwenye ile ya kuzini na kutelekeza watoto inakua ngumu ndo yanatokea kama haya.
Nyumba ndogo ya "kiswahili" namna hii hapana aisee!!
 
Nyie wenye vyeti acheni kuharibu ndoa za watu.
Mmekalia kutafuta vyeti, mwisho mmekosa Wame, mnaanza kuiba Wame za watu.
Acheni hiyo tabia ni mbaya Sana.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom