Una cheti nina mume

Daah! Nimekaa nikawaza huyo mwenye cheti anachambwa kwenye msg kupitia simu yake ya kiganjani kwa maneno ka hizi. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Haya bana muwe na mwisho mwema katika hizo mbio zenu.
Vita vya wanawake vinachekesha sana, sasa sijui kama anayekusudiwa anapitaga huku!
 
Huu uzi naona wachangiaji wengi wanawake wengine sijawah kuwaona sjui hii Mada itakuwa na nini?
Itakuwa leo Pombe hazipo kichwani bana MLEVi Mmoja πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜….

πŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈ
 
Kumbeee


Kuna Shida kichwani sio bure ,Bwana Yesu amtetee aweze kujitambua
 
Nafikiri hiyo ndoa ya mwenzake inamtesa Sana ,ametamani kuingia kashindwa ,kwa hayo maneno nawaza kama kazaliwa Manzese vile na kukulia uzuri ,Mungu amsaidie ajitambue kama ni mwanamke mwenye watoto wanaomtegemea wapate malezi bora
 
Ili nalo neno unakuta mtu anakomaa na shule weee anakuja kumaliza ana 40 ndo anatafuta Mume dah,
 
Mume mwenyewe ulikuwa unamuona boya. Nimemchukua nimemtunza kapendeza sasa ndio unakumbuka ulikuwa umeolewa. Kaa na cheti chako umechelewa stendi.....Pole weeeee!
 
Wanangu kusoma shule nzuri tu ndio linakushuka shuuuuu! Kumbuka anayesomesha wanangu ndiye aliyesomesha wanao, ni baba yao. Hawa watoto ni ndugu, acha roho mbaya.
 
Eti urithi? Unazungumzia urithi wa mtu ambaye yuko hai na anatimiza majukumu yote mpaka yale uliyosema hawezi hapa kwangu mbona anatimiza. Hujioni una matatizo?
Kwa taarifa yako wanangu hawahitaji urithi wako na wala hawana sababu ya kugombana na ndugu zao. Nilivyo navyo vinanitosha sana na nimeridhika sina tamaa kama za kwako.
Kama ulivyosikia kuwa baba yao kawanunulia viwanja ni kweli hati ziko hapa kwangu. Sijamzuia asiwanunulie hao wa kwako.
Eti gari kistaleti changu tu ndio unapiga domo kila siku kwa mashoga zako sasa kama na wewe ulitaka kununuliwa si ungemwambia akununulie. Mbona una magari au hayo hajakununulia? Kwa hiyo unaona wivu kuwa wewe umejinunulia magari lakini mimi kaninunulia. Tuliza mshono bibiye. Kwa taarifa yako gari nimenunua mwenyewe kwa biashara zangu. Ni kweli kanipa mtaji lakini biashara nimefanya mwenyewe kwa juhudi zangu. Umeshakuwa mtu mzima sasa tulia sasa usubiri wajukuu
 
Sisi ni familia moja sasa upende usipende. Watoto wetu ni ndugu na wanajuana. Jiheshimu uheshimiwe.
 
Kama cheti mali kitandike kitandani kwako ukilalie. Au jaribu kujifunika nacho kikutie joto. Nachekajeeee? Halooooooooo?
Na wanangu wana haki zote kwa baba yao.
Nakukumbusha tu.
Taarabu tena Jf!!!!!!!!!!
 
Nafikiri hiyo ndoa ya mwenzake inamtesa Sana ,ametamani kuingia kashindwa ,kwa hayo maneno nawaza kama kazaliwa Manzese vile na kukulia uzuri ,Mungu amsaidie ajitambue kama ni mwanamke mwenye watoto wanaomtegemea wapate malezi bora
Ndoa ipi? Cheti tu anaringia. Na hakimsaidii. Kila siku mikelele tu huko anakokunywa mipombe na mashangingi wenzie wa kwenye masemina na warsha. Na sasa anko M alivyozipiga panga hizo makongamano mbona mishauo kwishneeeee!
 
Back
Top Bottom