UN: Zaidi ya watu milioni 49 wanaweza kuingia katika umasikini uliokithiri

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mwaka huu, watu milioni 49 zaidi wanaweza kutumbukia katika umaskini uliokithiri kutokana na athari za #COVID19

Pia Idadi ya watu watakao kuwa na upungufu wa chakula au ukosefu wa lishe bora itaongezeka haraka. Japo
alisema dunia ina chakula cha kutosha kulisha watu wote na ziada lakini cha kusikitisha, watu zaidi ya milioni 800 wanakabiliwa na njaa

Amesisitiza kwamba kunahitajika kuchukuliwa hatua ili kuepusha athari mbaya zaidi za kudhibiti ugonjwa wa #CoronaVirus

-----

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia ina chakula cha kutosha kulisha watu wote na ziada lakini cha kusikitisha, watu zaidi ya milioni 800 wanakabiliwa na njaa

Ameyasema hayo kupitia ujumbe maalum wa uzinduzi wa sera kuhusu uhakika wa chakula. Ameonya kwamba endapo hatua za haraka hazitachukuliwa, ni dhahiri kwamba kuna dharura ya chakula ulimwenguni ambayo inaweza kuwa na athari za muda mrefu kwa mamia ya mamilioni ya watoto na watu wazima.

Watu zaidi kuingia katika umasikini

Ameongeza kuwa“Mwaka huu, watu milioni 49 zaidi wanaweza kutumbukia katika umaskini uliokithiri kwa sababu ya janga la COVID-19. Idadi ya watu watakao kuwa na upungufu wa chakula au ukosefu wa lishe bora itaongezeka haraka. Na kila kiwango cha asilimia kinachoshuka katika jumla ya pato la taifa inamaanisha watoto milioni 0.7 zaidi watadumaa.”

Katibu Mkuu amesema hata katika nchi zenye chakula kingi kunashuhudiwa hatari za usumbufu katika mnyororo wa usambazaji wa chakula. Amesisitiza kwamba kunahitajika kuchukuliwa hatua sasa ili kuepusha athari mbaya zaidi za juhudi za kudhibiti ugonjwa huu wa corona.

Guterres amesem leo anazindua mpango wa sera wa athari za COVID-19 katika uhakika wa chakula na lishe. Ambayo ina matokeo matatu ya wazi.

Mambo matatu muhimu

Kwanza,
lazima kuhamasisha kuokoa maisha na uhai, kwa kuzingatia umakini ambapo hatari ni kubwa sana. Hiyo inamaanisha kubuni huduma za chakula na lishe kama ni muhimu, wakati wa kutekeleza kinga zinazofaa kwa wafanyakazi wa chakula.

Inamaanisha kuhifadhi chakula muhimu cha kibinadamu, utu na msaada wa lishe kwa watu walio hatarini. Na inamaanisha kutoa chakula katika nchi zenye shida ya chakula ili kuimarisha na kuongeza mifumo ya kuilinda jamii.

Nchi zinahitajika kuongeza msaada katika usindikaji wa vyakula, usafirishaji na masoko ya chakula ya ndani, na lazima ziweke maeneo ya biashara wazi ili kuhakikisha utendaji kazi endelevu wa mifumo ya chakula.

"Na ni lazima tuhakikishe kwamba vifurushi vya misaada vinawafikia walio hatarini zaidi, pamoja na kukidhi mahitaji ya ukwasi wa wazalishaji wadogo wa chakula na biashara za vijijini."

Pili,
lazima kuimarisha mifumo ya kuilinda jamii kwa lishe. Nchi zinahitaji kulinda upatikanaji wa lishe salama, hususani kwa watoto wadogo, wanawake wajawazito na na wanaonyoyesha, wazee na makundi mengine yaliyo hatarini.

Na zinanahitaji kuridhia na kuendeleza miradi ya kuilinda jamii ili kunufaisha makundi yenye uhitaji wa lishe yaliyo kwenye hatari. Guterres amesema hii ni pamoja na kusaidia watoto ambao hawawezi tena kupata mlo shuleni.

Tatu, lazima tuwekeze kwa ajili ya baadaye. Ameongeza kuwa dunia ina jukumu la kujenga jamii jumuishi na endelevu.

“Tujenge mifumo ya chakula inayoshughulikia vyema mahitaji ya wazalishaji wa chakula na wafanyakazi. Tutoe ufikiaji unaojumuisha zaidi chakula, afya na lishe ili tuweze kutokomeza njaa. Na turekebishe uhusiano kati ya mifumo ya chakula na mazingira asilia kwa kuzibadilisha zifanye kazi vizuri kwa asilia na kwa ajili ya hali ya hewa.”

Na biila kusahau kwamba mifumo ya chakula inachamgia hadi asilimia 29 ya uzalishaji wote wa gesi chafu, ikijumuisha asilimia 44 ya methane, na zina athari mbaya kwa bayoanuai.

Amehitimisha akisema “endapo tutafanya mambo haya na zaidi, kama tunavyozindia leo, tunaweza kuzuia athari mbaya zaidi za janga la COVID-19 katika uhakika wa chakula na lishe na tunaweza kufanya hivyo kwa njia inayounga mkono mabadiliko ynayojali mazingira ambayo tunahitaji kuyatengeneza.”
 
UN wakati mwingine hua hata siwaelewi nia na ripoti zao! Lockdowns walizokua wakizipigia chapuo na kuzichagiza nchi zote duniani na hata kuzisakama na kuzizodoa zile nchi zilizokataa huo upuuzi ndio zimesababisha yote haya wanayokuja nayo kwenye ripoti yao!!!

Kuporomoka kwa uchumi, watu kupoteza ajira, watu kutumbukia kwenye umasikini uliopindukia wakiwa wanashambuliwa na magonjwa ya kila aina sasa(sio korona peke yake), na pia upungufu mkubwa sana wa chakula ndio mambo waliyokua wanayataka ili sasa kampeni za kina Bill Gates na UNFPA za upunguzaji wa idadi ya watu zipate mashiko

Korona kweli ni ugonjwa unaoua, lakini umasikini hasa unaolazimishwa unaotokana na kupewa hofu ya uongo, unaua watu wengi zaidi kutokana na upungufu wa chakula na kuongezeka kwa magonjwa mengine ya hatari zaidi.

Kwa mabeberu hii ni fursa ya kutuuzia madawa, chakula na "ushauri" tena kwa hela wanazodai eti wametukopesha wao wenyewe huku kiuhalisia zikipishana kutoka mtaa mmoja wa mabeberu kwenda mtaa wa pili wa watu haohao!!!
 
Hawa ni wendawazimu, kwani huo upungufu wa chakula na umakini si umeletwa na Lockdown walizokuwa wanazishauri? Kiasi sisi tuliogomea lockdown tukaanza kupakwa matope na kidhalilishwa? Hivi wana akili sawa sawa hawa watu?
 
Back
Top Bottom