UN yawateua Majaji watatu watakaosimamia kesi ya mshukiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda, Felicien Kabuga

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
Saa 1 iliyopita
Majaji watatu walioteuliwa kusimamia kesi ya kabuga

Majaji watatu walioteuliwa kusimamia kesi ya kabuga

Mahakama ya Umoja wa mataifa imewateua majaji watatu watakaosimamia kesi inayomkabili Felicien Kabuga.
Kamati ya Umoja mataifa kuhusu mahakama za uhalifu imewateua majaji hao kutoka mataifa ya Uskochi, Uruguay na Uganda kusimamia kesi ya Kabuga atakapowasilishwa katika mahakama ya Tanzania kujibu mashtaka ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Siku ya Jumatano mahakama ya Ufaransa iliunga mkono kushtakiwa kwake katika mahakama ya Umoja wa mataifa iliopo Arusha.
Wakili wake Emmanuel Altit aliambia BBC kwamba atakwenda katika kaati hiyo ya Umoja wa Mataifa kuhusu kesi za uhalifu ili kuhakikisha kwamba anahamishwa hadi mjini The Hague, Uholanzi ambapo kamati hiyo ina tawi lake.

Sheria za uhamisho za Ufaransa zinatoa mwezi mmoja kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.
Katika taarifa yake, Mahakama hiyo ya Arusha haikusema ni wakati gani kesi inayomkabili Kabuga itaanza.

Jaji wa Uskochi Lain Bonomy, ataongoza usimamizi wa kesi hiyo akisaidiwa na majaji wa Uruguay Graciela Susana Gatti Santana na jaji wa Uganda Elizabeth Ibanda - Nahamya, ilisema mahakama hiyo ya UN.

Bwana Kabuga mwenye umri wa miaka 85, ndio mtu maarufu kuwahi kushtakiwa na mahakama hiyo ya kimataifa 1997, ilisema mahakama hiyo , lakini alienda mafichoni hadi alipokamatwa karibu na mji wa Paris mnamo mwezi Mei 2020.

Katika mahakama ya Paris ameelezea mashtaka yanayomkabili kama ya uwongo.

Je anashtakiwa na nini?
Kabuga anashtakiwa kwa kufadhili mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Anadaiwa kuwasaidia wapiganaji wa kabila la Hutu ambao waliwaua takriban raia wa Tutsi 800,000 pamoja na Wahutu walio na msimamo wa kadri 1994.
Alianzisha kituo cha habari cha redio Télévision Libre des Mille Collines (RTLM), ambacho kilidaiwa kutoa wito kwa watu kuwaua watu wa kabila la Tutsi .

Mwaka 1997 alishtakiwa kwa mashtaka 7 ikiwemo mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu na jopo la kimataifa lililokuwa likichunguza mauaji hayo.

Je alikwepa vipi mtego wa polisi?
Maafisa wa polisi wanasema kwamba bwana Kabuga alitumia majina 28 tofauti kujificha.

Akiwa mtoro , alidaiwa kuishi katika mataifa mbalimbali Afrika mashariki ikiwemo Kenya, ambapo yeye na familia yake walikua na biashara.
Kujificha kwa Kabuga kwa miaka 26 kulizua maswali mengi


Kujificha kwa Kabuga kwa miaka 26 kulizua maswali mengi
Muendesha mashtaka wa Ufaransa alisema kwamba amekuwa akiishi kupitia utambulisho bandia.

Je mahakama hiyo ya mjini Arusha ni ipi?
Miezi kadhaa baada ya mauaji hayo , baraza la usalama la umoja wa mataifa lilianzisha mahakama ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mjini Arusha, kaskazini mwa Tanzania.
Lengo lake ilikuwa kuwashtaki viongozi wa mauaji hayo na zaidi ya watu 60 walihukumiwa.

Mahakama hiyo ilifungwa rasmi mwaka 2015 na baadaye utaratibu wa Mahakama za Kimataifa za Jinai MICT ulichukua usimamizi wake ili kuwasaka washukiwa wa mwisho.
Mahakama hiyo haina maafisa wa polisi wala uwezo wa kukamata, na badala yake imekuwa ikitegemea serikali tofauti kuchukua hatua hizo badala yake.

Je Filicien Kabuga ni nani?
Ndiye aliyekuwa mtu tajiri zaidi nchini Rwanda kabla ya mauaji ya 1994.

Akijipatia utajiri wake kupita biashara ya majani ya chai mwaka 1970 na alifanya biashara katika sekta chungu nzima nyumbani na katika mataifa ya kigeni.
Alikuwa mshirika wa karibu wa chama tawala cha MRND - na alikuwa na uhusiano na rais wa zamani Juvenal Habyarimana ambaye alifariki 1994.

Akituhumiwa kwa kuwa mfadhili mkuu wa mauaji hayo na kutumia biashara yake na uwezo wake kupanga na kufadhili mauaji.
Mmiliki wa kituo cha redio ya kibinafsi RTLM alishutumiwa kwa kuwachochea watu wa kabila la Hutu kuwaua Watutsi.

Mwaka 2006, jopo la kimataifa la Rwanda lililokuwa likichunguza mauaji hayo lilisema lina ushahidi kwamba bwana Kabuga alizuru nchini Kenya ama hata kuishi nchini humo, ambapo alikuwa akisimamia maslahi yake ya kibishara.

Miaka mitatu baadaye, Bwana Stephen Rapp, ambaye alikuwa balozi wa Marekani aliishutumu serikali ya Kenya kwa kukataa kumtoa bwana Kabuga.
Kulikuwa na ushahidi kwamba bwana Kabuga alihudhuria hafla zilizoshirikisha watu maarufu, alisema madai ambayo Kenya imekana.

Ni wazi kwamba familia ya bwana Kabuga ilikuwa ikimiliki mali nchini Kenya baada ya mali moja kuzongwa na kesi 2015 wakati mkewe, Josephine Mukazitoni , ambaye alikuwa mmiliki mwenza , alipojaribu kumiliki.
 
Mmmm mauji yale nilikuwa mdogo lakini nilikuwa nayasikia yanasikitisha sana.
 
waliokufa waishakufa mngeachana na hayo mambo mkaganga yajayo sema Watusi ni wabishi kama nini...
 
Back
Top Bottom