UN yalaani ukatili wa walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Wapalestina

KABAVAKO

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
229
32
Wakala za Umoja wa Mataifa na asasi nyingine zisizo za serikali zimelaani ukatili ulioshadidi wa walowezi wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina. Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF), jumuiya zisizo za serikali za huko Israel za Bet Saliim na Yash Din na taasisi ya Palestina ya al Haqq zimetoa taarifa ya pamoja zikitangaza kuwa mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina ambayo yamesababisha hasara nyingi za nafsi na mali ziliongezeka kwa asilimia 30 katika mwaka uliopita.
Mkurugenzi wa jumuiya isiyokuwa ya serikali ya Bet Saliim huko Israel Jessica Montel amesema walowezi wa Kiyahudi wamezidisha mashambulizi dhidi ya raia wa Palestina katika miaka ya hivi karibuni kwa lengo la kuwashinikiza ili waondoke katika makazi yao. Taarifa ya mashirika hayo pia imelaani misimamo ya viongozi wa Israel ya kuwapa kinga walowezi wanaofanya ukatili dhidi ya raia wa Palestina na kuwataka waheshimu sheria za kimataifa.
source; UN yalaani ukatili wa walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Wapalestina
 
Back
Top Bottom