UN yahadharisha mafuriko Tanzania

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
UMOJA wa Mataifa umeihadharisha Tanzania kuwa itakumbwa na mafuriko yatakayosababishwa na mvua za El-Nino na kutaka kuanza kuchukua tahadhari mapema.

Taarifa ya Umoja huo ya uwezekano mkubwa wa mafuriko yatakayosababishwa na mvua za El- Nino imetolewa wakati serikali inaendelea kubomoa nyumba zilizojengwa maeneo hatarishi katika mabonde na maeneo yasiyoruhusiwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayehusika na Misaada ya Kibinadamu na Uratibu wa Misaada ya Dharura, Stephen O’Brien, Tanzania inaweza kukabiliwa na mafuriko ya El-Nino kati ya mwezi huu wa Januari na Machi, mwaka huu.

Pamoja na Tanzania, nchi nyingine ambazo zimetajwa kukumbwa na mafuriko hayo makubwa ni pamoja na Madagascar, Malawi na Msumbiji.

Taarifa ya O’Brien kuhusu madhara ya El-Nino na namna gani Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kujiandaa au inajiandaa na kadhia hiyo iliwasilishwa mbele ya wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na nakala yake kutumwa kwa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Pamoja na kutoa tahadhari hiyo, O’Brien amezisihi nchi ambazo zinatarajiwa kukumbwa na maafa ya El -Nino kujiandaa ipasavyo na kuyataja maandalizi hayo kuwa ni pamoja na utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wananchi watarajiwa wa athari za mvua hizo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi, upande wa Afrika ya Mashariki, nchi kadhaa hususan ukanda wa magharibi zimekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua na hivyo kuathiri kiwango cha upatikanaji wa chakula.

Nchi hizo ni Ethiopia, Sudan, Djibouti na Eritrea ilihali baadhi ya nchi zikipata kiwango cha mvua kilichovuka mipaka. “ Kuanzia mwezi Januari hadi Machi, nchi za Tanzania, Msumbiji, Madagascar na Malawi zina uwezekano mkubwa wa ku kumbwa na mafuriko ya El- Nino,” alisema O’Brien.

Alisema nchi hizo zitahitaji pamoja na mambo mengine misaada ya kujiandaa na kushughulikia kile kinachotabiriwa kwani kina uwezekano mkubwa wa kutokea.

Ukiacha nchi za Afrika ya Mashariki, nchi nyingine kwa upande wa Afrika ambazo zimekumbwa na hali tete ya uhaba wa mvua na hivyo kutishia usalama na upatikanaji wa chakula ni Angola, Botswana, Malawi, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.

O’Brien alisema nchi hizo zimekuwa na uhaba wa mvua kiasi kwamba zitakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kusababisha watu zaidi ya milioni 28 katika mataifa hayo kukukosa chakula.

Akizungumzia kuhusu misaada ambayo imekwishakutolewa na nchi wahisani ili kukabilia na ukame na madhara yatokanayo na El-Nino , Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi huyo alisema kuwa hadi wakati anatoa taarifa yake kiasi cha Dola za Marekani milioni 360 kilikuwa kimetolewa na wafadhili kwa lengo la kukabiliana na madhara yatakayotokana na ElNino ikiwa ni pamoja na usalama wa chakula.

Pamoja na michango hiyo, O’Brien alisema haitoshi kutokana na ukweli kwamba maafa yatakayotoka na madhila ya El-Nino yanahitaji misaada zaidi. Mbali ya nchi za kanda ya Afrika baadhi ya nchi nyingine ambazo zitakumbwa na zilishawahi kupata balaa la El-Nino ni pamoja na nchi ambao zimo katika Bara la Latini Amerika na nchi za eneo la Pasifiki ambazo nyingi ni visiwa.

Shirika la Kimataifa la Hali ya Hewa (WMO) linatarajiwa Mwezi Februari kutoa taarifa zaidi kuhusu mwelekeo za mvua hizo za El-Nino. Mvua kama hizo zilishawahi kunyesha nchini Tanzania mwaka 1998 na kusababisha maafa makubwa na watu kadhaa walipoteza maisha, huku maelfu wengine wakijeruhiwa na kupoteza makazi.

Mwaka jana mwezi Agosti Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa tahadhari kuwa Tanzania ni kati ya nchi za Barani Afrika zitakazokumbwa na mvua za El Nino kati ya mwezi Septemba na Desemba, mwaka jana.
 
Last edited by a moderator:
Hii habari tunaiangalia kwa jicho la kawaida hadi sasa lakini ikitokea mvua inayoendana na joto tuliloshuhudia henda hali ikawa mbaya.
Ukiangalia hizi graphics za utabiri wa hali ya hewa ni wazi tuombe Mungu mwelekeo wa hili wingu ubadilike loakini likisalia kama lilivyo huenda jumamosi kama ya leo tukawa tunaongea mengine!

rain.jpg
 
Badala wamalize maandaliz ya jecha huko zanzibar kwaajili ya umwagaji damu wao wanatuletea hoja ya maforiko! Hayabhana

Hii habari usibeze kisiwa chenyewe cha Zanzibar chaweza zamishwa na EL-Nino huo mgogoro wa zanzibar ukawa umeisha kwa kuwa wazanzibari watakuwa wamezama wote ndani ya maji.Usicheze na El nino wewe ni habari kubwa kuliko huo uchaguzi .EL NINO YAWEZA WAMEZA WOTE wapiga kura,wagombea na ZEC
 
Akili yako unaijua mwenyewe..wewe unataka na wanachi wengine wapate majanga ili tuongeze matatizo..just think a little before you post your nonsense
 
Badala wamalize maandaliz ya jecha huko zanzibar kwaajili ya umwagaji damu wao wanatuletea hoja ya maforiko! Hayabhana
siamini jinsi hii habari ulivyoichukulia kirahisi ....unashauri tupuzie hilo onyo kwa vile zanzibar kuna mgogoro.
 
Hii habari usibeze kisiwa chenyewe cha Zanzibar chaweza zamishwa na EL-Nino huo mgogoro wa zanzibar ukawa umeisha kwa kuwa wazanzibari watakuwa wamezama wote ndani ya maji.Usicheze na El nino wewe ni habari kubwa kuliko huo uchaguzi .EL NINO YAWEZA WAMEZA WOTE wapiga kura,wagombea na ZEC
Aisee nimecheka sana
 
SASA WALE WANAOPINGA WATU KUHAMISHWA MABONDENI KWA LAZIMA (MAANA KWA HIARI IMESHINDIKANA) WATAKUWA RESPONSIBLE KWA WOTE WATAKAOPOTEZA MAISHA!!!

Queen Esther

UMOJA wa Mataifa umeihadharisha Tanzania kuwa itakumbwa na mafuriko yatakayosababishwa na mvua za El-Nino na kutaka kuanza kuchukua tahadhari mapema.

Taarifa ya Umoja huo ya uwezekano mkubwa wa mafuriko yatakayosababishwa na mvua za El- Nino imetolewa wakati serikali inaendelea kubomoa nyumba zilizojengwa maeneo hatarishi katika mabonde na maeneo yasiyoruhusiwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayehusika na Misaada ya Kibinadamu na Uratibu wa Misaada ya Dharura, Stephen O’Brien, Tanzania inaweza kukabiliwa na mafuriko ya El-Nino kati ya mwezi huu wa Januari na Machi, mwaka huu.

Pamoja na Tanzania, nchi nyingine ambazo zimetajwa kukumbwa na mafuriko hayo makubwa ni pamoja na Madagascar, Malawi na Msumbiji.

Taarifa ya O’Brien kuhusu madhara ya El-Nino na namna gani Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kujiandaa au inajiandaa na kadhia hiyo iliwasilishwa mbele ya wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na nakala yake kutumwa kwa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Pamoja na kutoa tahadhari hiyo, O’Brien amezisihi nchi ambazo zinatarajiwa kukumbwa na maafa ya El -Nino kujiandaa ipasavyo na kuyataja maandalizi hayo kuwa ni pamoja na utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wananchi watarajiwa wa athari za mvua hizo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi, upande wa Afrika ya Mashariki, nchi kadhaa hususan ukanda wa magharibi zimekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua na hivyo kuathiri kiwango cha upatikanaji wa chakula.

Nchi hizo ni Ethiopia, Sudan, Djibouti na Eritrea ilihali baadhi ya nchi zikipata kiwango cha mvua kilichovuka mipaka. “ Kuanzia mwezi Januari hadi Machi, nchi za Tanzania, Msumbiji, Madagascar na Malawi zina uwezekano mkubwa wa ku kumbwa na mafuriko ya El- Nino,” alisema O’Brien.

Alisema nchi hizo zitahitaji pamoja na mambo mengine misaada ya kujiandaa na kushughulikia kile kinachotabiriwa kwani kina uwezekano mkubwa wa kutokea.

Ukiacha nchi za Afrika ya Mashariki, nchi nyingine kwa upande wa Afrika ambazo zimekumbwa na hali tete ya uhaba wa mvua na hivyo kutishia usalama na upatikanaji wa chakula ni Angola, Botswana, Malawi, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.

O’Brien alisema nchi hizo zimekuwa na uhaba wa mvua kiasi kwamba zitakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kusababisha watu zaidi ya milioni 28 katika mataifa hayo kukukosa chakula.

Akizungumzia kuhusu misaada ambayo imekwishakutolewa na nchi wahisani ili kukabilia na ukame na madhara yatokanayo na El-Nino , Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi huyo alisema kuwa hadi wakati anatoa taarifa yake kiasi cha Dola za Marekani milioni 360 kilikuwa kimetolewa na wafadhili kwa lengo la kukabiliana na madhara yatakayotokana na ElNino ikiwa ni pamoja na usalama wa chakula.

Pamoja na michango hiyo, O’Brien alisema haitoshi kutokana na ukweli kwamba maafa yatakayotoka na madhila ya El-Nino yanahitaji misaada zaidi. Mbali ya nchi za kanda ya Afrika baadhi ya nchi nyingine ambazo zitakumbwa na zilishawahi kupata balaa la El-Nino ni pamoja na nchi ambao zimo katika Bara la Latini Amerika na nchi za eneo la Pasifiki ambazo nyingi ni visiwa.

Shirika la Kimataifa la Hali ya Hewa (WMO) linatarajiwa Mwezi Februari kutoa taarifa zaidi kuhusu mwelekeo za mvua hizo za El-Nino. Mvua kama hizo zilishawahi kunyesha nchini Tanzania mwaka 1998 na kusababisha maafa makubwa na watu kadhaa walipoteza maisha, huku maelfu wengine wakijeruhiwa na kupoteza makazi.

Mwaka jana mwezi Agosti Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa tahadhari kuwa Tanzania ni kati ya nchi za Barani Afrika zitakazokumbwa na mvua za El Nino kati ya mwezi Septemba na Desemba, mwaka jana.
 
Tusiwe kama Tomaso kwenye biblia. El Niño ni habari nyingine. Serikali itoe tahadhari kila siku hii kitu ikija tutatafutana baada YA matukio. Siasa hapa si mahala pake
 
Daaah hii habari inatakiwa ichukukiwe kwa uzito mkubwa sana na hatua za haraka na za maana zianze kuandaliwa kwa ajiki ya kukabiliana na janga hili. Vilevile kuna umuhimu wa kuwapa elimu zaidi watu wa mabondeni juu ya madhara ya mvua hizi zinazotarajia kunyesha Mwenyezi Mungu akipenda na serikali kuwaandalia maeneo mengine kwa ajili ya makazi ya kudumu. Usumbufu na matatizo yatakayo tokea iwapo mvua za el nino zitanyesha haziwaathiri watu wa mabondeni bali hata sisi wa maeneo salama kwa kupata ugeni wa mandugu wa ghafla.
 
Hii habari tunaiangalia kwa jicho la kawaida hadi sasa lakini ikitokea mvua inayoendana na joto tuliloshuhudia henda hali ikawa mbaya.
Ukiangalia hizi graphics za utabiri wa hali ya hewa ni wazi tuombe Mungu mwelekeo wa hili wingu ubadilike loakini likisalia kama lilivyo huenda jumamosi kama ya leo tukawa tunaongea mengine!

View attachment 317258

Hii kitu si cha kubeza kabisa anyway hivi ... wale wenzetu wa mawio na machweo hawajaiona hii?
 
Hivi hata hili la hali ya hewa tunasubiri tuambiwe na UN? Mamlaka yetu ya hali ya hewa iko wapi? We need to be serious El nino ni hatari sana. Na wanatuarifu mapema ili wasije beba huo mzigo wao.
 
This is spining. Wanawatoa watu kwenye suala za Z NZ.

Hii ishu ya El Nino walianza kusema tokea mwaka jana mwezi wa 9.

Huu ni mwezi wa 4 sasa tunasubiri hiyo El Nino. Huu utaburi wa hali ya hewa ni wa aina yake na unapaswa uingizwe kwenye records za Guinness
 
SASA WALE WANAOPINGA WATU KUHAMISHWA MABONDENI KWA LAZIMA (MAANA KWA HIARI IMESHINDIKANA) WATAKUWA RESPONSIBLE KWA WOTE WATAKAOPOTEZA MAISHA!!!

Queen Esther
Waache bomoa bomoa inafanywa na mwenyezi mungu tutawakuta kule salenda na vigodoro vyao
Ubishi ni hatari kwa afya yako.....
 
Back
Top Bottom