UN: Watu Milioni 235 duniani watahitaji msaada wa dharura 2021

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Umoja wa mataifa umesema kwamba dola bilioni 35 zitahitajika kwa ajili ya huduma za msaada katika mwaka 2021.Kiwango hicho kikubwa cha fedha kinahitajika wakati janga la virusi vya Corona likiwa limewaacha mamilioni ya watu katika hali ngumu ya mgogoro.

Ripoti ya mwaka ya Umoja wa Mataifa inayoangalia hali jumla ya kibinadamu duniani inakadiria kwamba watu milioni 235 duniani kote watahitaji namna fulani ya msaada wa dharura katika mwaka ujao wa 2021.Mark LowCork mratibu wa shughuli za msaada wa dharura katika Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi habari kwamba ongezeko hilo la watu watakaohitaji msaada mwaka ujao limetokana kwa kiasi kikubwa na janga la virusi vya Corona.

"Tunafikiri kwamba kiasi watu milioni 170 duniani watahitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu. Mwaka ujao 2021 tunafikiri idadi hiyo itaongezeka na kuwa watu milioni 235. Hilo ni ongezeko la asilimia 40 na ongezeko limekuja kwa kiasi kikubwa kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Hali halisi

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa katika mwaka 2021 katika kila watu 33 duniani mmoja atakuwa katika uhitaji wa msaada huku pia ripoti ya Umoja huo ikisisitiza kwamba ikiwa watu wote hao watakuwa wanaishi kwenye nchi moja basi nchi hiyo itakuwa ni nchi ya tano kwa ukubwa duniani.

Ripoti hiyo ya mwaka kimsingi ni ripoti ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibindamu ambayo inatowa mwito katika suala zima la msaada wa kibindamu huku ikionesha hali halisi ya kuongezeka kwa mahitaji,ambayo inasababishwa na migogoro,watu kuachwa bila makaazi,majanga ya kiasili na mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo mara hii ripoti hiyo imeonya kwamba hali hiyo ya kuhitajika msaada wa kibinadamu imeletwa zaidi na janga la virusi vya Corona ambalo limeshauwa zaidi ya watu milioni 1.45 duniani kote na imesababisha hali mbaya zaidi kwa wale ambao tayari walikuwa wakiishi katika mazingira magumu.

Fedha zilizotajwa na Umoja huo wa Mataifa kwa ajili ya msaada zinaweza kutosha kusaidia watu milioni 160 walioko kwenye hatari kubwa zaidi katika nchi 56 kote duniani.

Aidha ripoti hiyo imekumbusha kwamba kwa mara ya kwanza tangu miaka ya 1990 ufukara wa kupindukia uko kwenye hatua ya kuongezeka, na kiwango cha umri wa kuishi kitapungua huku pia idadi ya kila mwaka ya vifo vinavyosababishwa na HIV , kifua kikuu na Malaria inaweza kuongezeka mara mbili.
 
Hii Corona kila mtu ataangalia taifa lake na watu wake kwanza, manake nchi ya ulaya zinapitia msoto wa uchumi si wa kitoto.

Yaani sisi Wafrika tulivyojiachia kutegemea kupewa tujiandae manake misaada itapungua au watakata kabisa kuwasaidia Wafrica na nguvu zao kuzieleleza kwa wananchi wao kwanza na kufufua uchumi wao.

Yaani kwa kifupi Wafrika tufunge mikanda.
 
Hii Corona kila mtu ataangalia taifa lake na watu wake kwanza, manake nchi ya ulaya zinapitia msoto wa uchumi si wa kitoto.

Yaani sisi Wafrika tulivyojiachia kutegemea kupewa tujiandae manake misaada itapungua au watakata kabisa kuwasaidia Wafrica na nguvu zao kuzieleleza kwa wananchi wao kwanza na kufufua uchumi wao.

Yaani kwa kifupi Wafrika tufunge mikanda.
Swadaktaa kabisaa..
 
Back
Top Bottom