UN: Vifo 745,000 vimetokona na kufanya kazi sana

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Utafiti wa Shirika la Afya duniani WHO, na la kazi duniani ILO unaonesha kufanya kazi kwa muda mwingi katika kipindi cha mwaka 2016, kumechangia vifo 745,000.
Katika utafiti weao huo, mashirika WHO na ILO kwa pamoja yanakadiria watu 398,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa kiharusi na 347,000 magonjwa ya moyo kwa 2016. Sababu ambao inaoneshwa ni kufanya kazi kwa muda mrefu kunakofikia masaa 55 kwa wiki.

Kati ya mwaka 2000 na 2016, idadi ya vifo vilivyotokana na magonjwa ya moyo kwa sababu ya kufanya kazi kwa muda mrefu vimeongezeka kwa asilimia 42, na kiharusu asilimia 19. Na mzigo mkubwa wa vifo hivyo kwa asilimia 72 wanaubeba wanaume. Maeneo ambayo yanatajwa kuwa na athari zaidi kwa wafanyakazi wa umri wa kati au wazee ni Magharibi mwa Asia Pasifiki na ukanda wa Kusini-Mashariki mwa Asia.

Masaa ya kufanya kazi kwa unafuu yawe 35 hadi 40.

Profesa Jian Li mmoja kati wa maafisa waandamizi wa WHO, walioshiriki utafiti huo anasema "Tumebaini kwamba, kufanya kazi kwa masaa 55 au zaidi kwa wiki, kuonaongeza hatari ya kufa kwa magoinjwa haya ya moyo kwa asilimia 17, baada ya miaka 10. Hilo limejikita katika takwimu za washiriki 340,000 za makundi ya tafiti 22 tofauti duniani. Vilevile tumebaini kufanya kazi kwa masaa 55 au zaidi kwa wiki kuonaongeza hatari ya kupata kiharusi kwa asilimia 35."
 
Inabidi ufanyekazi na Ule BATA.
Hapo ndio wanafail.
Tusione Wazungu wanahela sana Wanapofanyakazi miezi 10. Mwezi wa 12 wanakuja Kula Bata Serengeti au Zanzibar.

Tufanye kazi huku tukitunza hela kidogo ya BATA

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Ukipanga kazi zako vizuri, huwezi fanya kazi zaidi ya masaa 35-40. Tengeneza ratiba inayokuruhusu kupumzika, maisha yapo na yanapangwa.
 
Itakuwa China na Japan, siyo huku kwetu!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Back
Top Bottom