#COVID19 UN: Mamilioni ya watoto wakosa chanjo za kawaida mwaka 2020 kwasababu ya Covid-19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Umoja wa Mataifa umesema jumla ya watoto milioni 23 hawajapata chanjo za kawaida na hivyo kuwaweka katika hatari ya kupata surua pamoja na magonjwa mengine hatari.

Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa na Shirika la Afya Duniani, WHO pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto, UNICEF idadi hiyo imeongezeka kwa watoto milioni 3.7 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Mashirika hayo yamesema mwaka uliopita watoto hao hawakupata chanjo muhimu zinazotolewa kwa watoto, kutokana na mfumo wa huduma za afya ulimwenguni kukwama kutokana na vizuizi vilivyowekwa ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Mkuu wa idara ya chanjo na kinga wa WHO, Kate O'Brien amesema kuna uwezekano wa mlipuko kutokea mwaka huu. O'Brien amesema hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa za kuwalinda watoto ambao hawana kinga kwa kuwa hawajapata chanjo.

Takwimu zinaonesha kuwa watoto wengi hawajapata chanjo dhidi ya pepopunda, donda koo na kifaduro.
 
Wazungu wamekazana haoooo, kila mahali ni michanjo tu,sasa hapo ndio watawachoma hizo zao kwa jina la surua
Take care
 
Back
Top Bottom