SoC01 Umuhimu wa Wanafunzi wa Vyuo vya Kati kupata mkopo

Stories of Change - 2021 Competition

cey03

New Member
Sep 6, 2021
4
4
Habarini wana jamii.

Katika kada ya Elimu hususani vyuoni Kuna umuhimu mkubwa wa wanafunzi wa vyuo vya Kati kuwekwa katika bajeti ya kupata mkopo.

Jumla ya wanafunzi katika vyuo vya kati au vyuo vya ufundi hujitegemea kwa kiwango kikubwa katika kujihudumia kuanzia malazi, makazi hata malipo ya ada chuoni. Hatua hii huwa ni ngumu Sana kufanikiwa kwa wanafunzi wote wanaochaguliwa kujiunga na vyuo vyakati.

Kwa sababu mfumo wa uendeshaji wa vyuo hivi havikuweza kuwahusisha wanafunzi kupata mikopo ambayo ingeweza kuwasaidi japo katika kusogeza maisha ya kielimu katika vyuo hivi.

Changamoto nyingi hutokea katika vyuo hivi, kwasababu unapochaguliwa katika chuo chochote Cha Kati au ufundi, unakuwa muhusika mkuu wa kila kitu chako kinachohusu fedha, bila kuangalia wewe ni mtoto wa mkulima au la, au wewe ni yatima au la, wote mwenye nacho na asiye nacho hapo wanakuwa kundi Moja..

Hatua hii husababisha shida nyingi kama:-

1. Asilimia kubwa ya wanafunzi wasio na uwezo kifedha kutopata fursa ya kuendeleza hatma yao kielemu kutokana na ukosefu wa fedha hvyo kuwafanya wasitiehe masomo yao.

2. Wadada wengi kujitumbikiza katika wimbi wa mahusiano na wafanyakazi wa vyuo kwa kusudio wanaweza wakapata fedha kwa ajili ya kujikimu hvyo kupelekea ongezeko la wimbi la magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.

3. Msongo wa mawazo hususani kwa vijana wanao jisomesha wenyewe, kujua namna gani au wapi wanaweza wakafanya michakato mabalimbali kwa ajili ya fedha za masomo hivyo kusababisha asilimia kubwa kupoteza umakini wao wanapokuwa darasani.

Ingawa si wanafunzi wote wa vyuo vikuu hufanikiwa kupokea au kupata mkopo lakini asilimia kubwa kwao hupata, kulingana na uhitaji wao angalau Kuna Yale makundi maalum hufikiliwa kwa kiasi kikubwa katika upewaji wa mikopo mfano walemavu, yatima na hata wasiojiweza.

Jicho hili la serikali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi hao linapaswa lielekezwe pia katika wanafunzi was vyuo vya Kati kwani hao ndo wahanga kabisa wa tatizo la kiuchumi katika Elimu.

Makundi au watu wanaopewa vipaumbele katika utoaji wa mikopo kwa Elimu ya juu, hayo makundi pia yapo katika vyuo vya Elimu ya Kati na wengine wanaotoka katika familia zisizo na uwezo kabisa wa lipia angalau ada ya masomo hvyo kupelekea wanafunzi wenzao kujitolea kuwachangia watu hao kusudi waendelee kubaki chuo kutimiza malengo yao.

Itapendeza na kuwa vyema zaidi Kama serikali itaweka fungu la bajet kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vya Kati kupata mkopo angalau kwa ajili ya ada za masomo kusudi kuweza kufanikisha ndoto za wanafunzi wengi kitaaluma, Kisha wanafunzi hao kutumia taaluma zao Kama chachu ya maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

Nakaribisha mchango wenu wanajamii katika hili.

Pia usisahau kupigia...🙏
 
Back
Top Bottom