Uchaguzi 2020 Umuhimu wa Vyama vya Upinzani kushirikiana

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,912
30,254
*_Na Sheikh Ponda Issa Ponda_*

Vyama vikuu vya upinzani vinakamilisha michakato muhimu vikijiandaa kushiriki uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu. Kwa mujibu wa vyama hivyo lengo kuu ni kuwafariji Watanzania kwa kuwaondolea shida zao na kuwaletea maendeleo.

Kwa mujibu wa hotuba ya mmoja wa wagombea urais baada ya kuteuliwa na chama chake ameahidi kutatua mambo muhimhiUHIu yanayowakwaza Watanzania likiwemo suala la kupatikana Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia. Amesema endapo atashinda na kuwa rais wa Tanzania upatikanaji wa katiba mpya litakuwa suala lake la kwanza.

Aidha katiba mpya ni katika mambo muhimu na kilio kikubwa cha Watanzania. Swala hili ni rahisi mno endapo chama au umoja wa vyama vya upinzani watashinda urais kwa kuwa wanalihitaji na watakuwa na mamlaka makubwa ya kitaifa. Suala muhimu katika ajenda hii ni je, tutegemee katiba mpya kwa njia hiyo tuu au tunaweza kupata katiba mpya hata kama wapinzani watakosa urais.

Katika swali hilo napenda tukumbushane ifuatavyo:

Tanzania kama yalivyo baadhi ya mataifa inaongozwa na serikali ya chama kilicho kabidhiwa nchi na wakoloni. Uongozi wake ni wa halali kwa mujibu wa sheria za nchi. Kwa uzowefu tulionao vyama vilivyo kabidhiwa nchi na wakoloni, na serikali zake hujiimarisha zaidi katika utawala na huogopa sana mabadiliko. Huogopa mabadiliko hata yale yanayotakiwa na wananchi walio wengi na yenye maslahi makubwa ya Taifa.

Hapa kwetu Tanzania tunaweza kuona ugumu huo katika masuala muhimu kama yale ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Vilevile katika kutangazwa washindi wa chama cha siasa cha upinzani katika chaguzi za kitaifa (rejea chaguzi Zanzibar na malalamiko ya Bara 2015). Na vilevile katika hitajio la katiba mpya ya Tanzania. Aidha ni kawaida ya binadamu kuogopa mabadiliko na hivyo ndivyo zilivyo serikali hizi zinazoongozwa na binadamu.

Hata hivyo serikali hizi hufanya mabadiliko kwa njia kadhaa ikiwemo kubwa ya msukumo (presha), na kadhalika. Mfano mwaka1993, serikali ya Tanzania ilifanya mabadiliko ya katiba. Mabadiliko hayo yalimuondoa Rais wa Zanzibar katika nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hakika hayakuwa mabadiliko mazuri kwa kuwa yalikuwa yanaipunguzia hadhi Zanzibar katika muungano. Hata hivyo sababu ya mabadiliko hayo ni nguvu ya kambi ya upinzani ambayo ilionesha wazi wanachukuwa uongozi wa dola Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa 1995 na hatimaye kunyakua nafasi nyingine muhimu ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.

Aidha mwaka 1995, serikali ilifanya mabadiliko mengine ya katiba. Pamoja na mambo mengine mabadiliko makubwa yalikuwa ni kiapo kwa viongozi wa kitaifa cha kutovunja muungano. Sababu ya mabadiliko hayo ni nguvu ya kundi la wabunge 55, (G55), lililotengeneza nguvu kubwa ya kudai serikali ya Tanganyika. (Bunge pia lililazimika kupitisha azimio la kuundwa serikali hiyo ya Tanganyika).

Mwaka 2000, serikali ilifanya mabadiliko mengine ya katiba. Pamoja na kutumia fursa hiyo kuingiza mambo ya kujiimarisha lakini walikubali kuanzishwa kwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Tanzania. Sababu ya mabadiliko hayo ni msukumo mkubwa wa kambi ya upinzani.

Mifano hii michache ninakusudia kuonesha umuhimu wa nguvu ya kambi ya upinzani katika kusukuma na kuleta mabadiliko. Ninakumbusha haya kwa sababu nimeona ile njia ya kuleta mabadiliko baada ya kupata urais inafanyiwa maandalizi ya kutosha lakini hii ya nguvu ya pamoja ya upinzani haina mwelekeo wa kuridhisha.

Nirejee maelezo yangu ya mara kwa mara kwamba uchaguzi uliopo mbele yetu ni muhimu sana kwa kuimariha vyama vilivyopo lakini uchaguzi wa hakika ni ule wa katiba mpya. Na katiba mpya ni ajenda muhimu baada ya uchaguzi huu wa Oktoba 2020. Hata hivyo maandalizi ya ajenda hii lazima yafanyike sasa kabla ya uchaguzi. Endapo vyama vya upinzani vitaungana sasa kwa dhati vitatengeneza nguvu itakayo sukuma suala la katiba mpya baada ya uchaguzi. Na huo ndio msingi muhimu sana katika hitajio la Watanzania la uchaguzi huru na wa haki. Endapo wapinzani hawataungana sasa kwa dhati basi hawataungana baada ya uchaguzi na kwa muktadha huo hapatakua na nguvu ya pamoja baada ya uchaguzi.

Ieleweke mazingira ya siasa Tanzania yamebadilika sana. Huko nyuma taasisi au chama kimoja kiliweza kujenga nguvu kubwa na kuleta msukumo wenye maslahi kama tulivyogusa hapo nyuma. Sasahivi tuepuke ndoto kwamba CUF pekee, CHADEMA pekee, ACT pekee, vinaweza kusukuma suala la katiba mpya baada ya uchaguzi. Kwahakika umoja ndio njia sahihi katika kutafuta maslahi ya Umma.


*SHEIKH PONDA ISSA PONDA – 0710 933 344.*
 
Mohamed Said,

..shukran sana kwa kutuletea makala hii ya Sheikh Ponda.

..tunaomba utupatie kitabu cha Taasisi ya Shura ya Maimamu kinachohusu uchaguzi wa 2020.

..tungependa kitabu hicho kiwepo hapa jukwaani ili wanachama tukichangie.

..natanguliza shukrani.
 
Tatizo kuna vyama vya siasa na kuna vyama vya kusherehesha.

Zitto hakutaka UKAWA 2015, akiamini yeye ni shujaa na aliweka allegiance yake kwa ccm wakati huo. Chadema na Cuf walivuna viti vingi, na NCCR vichace.

Baadaye tumemsikia Lipumba kwa kinywa chake akisema hatoungana na Chadema, tulimsikia Mbatia akisema hata kwwnye baraza la mawaziri kivuli atolewe na Mbowe alimtoa.

Leo mnataka vyama vipi viungane?! NCCR na CUF, au ACT na CHADEMA?!

Kwanini Chadema wakubali kuungana na Zialiyeukataa ukawa 2015, leo kaona nini au kwa maslahi ya nani?!

Mbatia na Lipumba mmewasikia, mnaongelea vyama gani, Jahazi Asilia, na TADEA, au TLP na UDP?!

Maana hata DP haqataki muungano, achilia mbali TADEA ya Shibuda, nao hawataki muungano, mnaongelea vyama vipi au vya kina nani?! labda tuwaamshe marehemu kina Che Mponda, na akina Emanuel Makaidi, Kasanga Tumbo au Cheif Fundikira, hawa waliopo wote wabinafsi, muungano wafaidike wao sio chama chenye ushawishi.

Kila chama wanataka wagawane ruzuku hata wabunge hawajawapata, wataungana vipi.
 
Back
Top Bottom