Umuhimu wa tz kudhibiti dhahabu yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu wa tz kudhibiti dhahabu yake

Discussion in 'International Forum' started by Sijali, Oct 16, 2012.

 1. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Wakati huu ambapo nchi nyingi, kama Uswisi, wanazungumzia kurudi kwenye mfumo wa 'Gold Standard' kuachana na mfumo wa 'paper money' (fiat money) au angalau warudie mfumo wa 'Gold Exchange Standard' kama hiyo ya kwanza haiwezekani kwa sasa, inasikitisha kuona Afrika kwa ujumla na Tanzania hasa bado ziko katika mentality ya kuwapa wazungu dhahabu yao.
  Dhahabu ndiyo iliyokuwa kigezo cha biashara na utajiri wa nchi kwa zaidi ya miaka 200 ya historia ya maendeleo ya viwanda hadi mwanzo wa vita vya kwanza vya dunia, ambapo Uingereza ilishindwa kuigharamia vita hiyo kwa mizani ya dhahabu, ndipo ikaamua kuacha kigezo cha dhahabu kwa fedha ya Pound. Na tangu siku hiyo Pauni imeendelea kuporomoka ukilinganisha na dhahabu. Na Wamarekani nao walipofuatia hivyo miaka ya sabini dola yao imeshuka kiasi hii leo dola moja ni sawa na zilizokuwa senti 8 tu za mwaka 70!
  Kuna sababu nyingi ya nchi hizo kuamua kuachana na dhahabu.... sitazizungumzia kwani zitawakoroga watu hapa, lakini mimi naamini kuna 'conspiracy' Jiulize: nani anahodhi dhahabu nyingi duniani hii leo?
  Nchi nyingi kubwa duniani kwa kweli zimeweza kuendelea kwa sababu ya dhahabu: Australia, Marekani, Uingereza (kwa kuiba) na hata South Africa.
  Ukisoma historia ya fedha duniani, utaona wakati dhahabu ilikuwa ndiyo fedha, au hata ilipotoholewa na kuwa 'kigezo' cha fedha, ndipo uchumi wa kweli ulipokuwa. Pia kuwa dhahabu ndiyo fedha au ndiyo kigezo (Gold exchange standard) kunaimarisha uhuru wa mtu (kwa vile serikali haimudu kuweka bei au kuchezeachezea biashara) na kusimamisha vita vya kiholela duniani, kwa vile hakutakuwa na nchi itakayogharimia vita kwa kuchapisha karatasi tu- kama ifanyavyo Marekani hivi sasa.
  Inasikitisha kwamba wakati huu 'watu wenye akili' wanafikiria kurudia vigezo vya dhahabu, Tanzania ndiyo kwanza inatoa dhahabu yake kwa chee!
  Hakuna sababu hivi sasa ya Tanzania kuchimba dhahabu yake- kama wanasema hawana uwezo wa kuchimba wenyewe ila 'wawekezaji'. Ni vizuri zaidi kuiacha ardhini kuliko kuitoa kwa watu hawa wanaoichukua bure kwa kubadilishana na ushanga.......kama vile vile walivyorubuniwa wazee wetu. Yaelekea akili ya Mwafrika haijakomaa tangu zama hizo!
   
Loading...