Umuhimu wa tunda la nanasi katika mwili wa mwanadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu wa tunda la nanasi katika mwili wa mwanadamu

Discussion in 'JF Doctor' started by babalao, Mar 10, 2011.

 1. babalao

  babalao Forum Spammer

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwili unapokosa kinga imara, huwa katika hatari ya kushambuliwa na kila aina ya magonjwa. Katika orodha hiyo ya magonjwa, yamo pia yale ya kutokwa na uvimbe yakiwemo majipu. Kitaalamu magonjwa haya yanajulikana kama "Inflamatory diseases".

  Katika kukabiliana na matatizo kama hayo, nanasi ni moja kati ya matunda yenye vitamin nyingi na virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuupa kinga mwili wako dhidi ya magonjwa hayo na mengine.

  Siri na umuhimu wa nanasi upo kwenye kirutubisho aina ya "Bromelain" ambacho kinapatikana kwa wingi kwenye tunda hili. Virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa muhimu sana katika kujenga na kuimarisha kinga ya mwili.

  Ukilipa umuhimu na ukiliweka nanasi katika orodha ya matunda unayokula mara kwa mara, utajiepusha na utajipa kinga dhidi ya magonjwa mengi hususan ugonjwa wa kuwashwa na kuvimba koo, ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis) na ugonjwa wa gauti (Gout).

  Ili upate kinga dhidi ya maradhi hayo kwa kula nanasi, unashauriwa kula tunda hilo kabla au baada ya kula mlo wako. Usile nanasi pamoja na chakula kingine kwa wakati mmoja. Kwa kufanya hivyo, virutubisho vitafanya kazi nyingine tofauti na uliyokusudia. Faida nyingine za nanasi ni kama ifuatavyo;

  USAGAJI WA CHAKULA
  Nanasi lina virutubisho vinavyouwezesha mfumo wa usagaji chakula tumboni kufanya kazi yake ipasavyo. Pindi mfumo huu unapowezeshwa kufanya kazi yake vizuri, mtu huweza kupata choo laini na kwa wakati kama inavyotakiwa.

  KINGA YA MWILI
  Nanasi linaaminika pia kuwa miongoni mwa matunda yenye Vitamin C kwa wingi ambayo kazi yake ni kuupa mwili kinga dhidi ya "wavamizi" mbalimbali (free radicals), ambao wanapoingia mwilini, kazi yao huwa ni kuharibu chembembe hai za mwili.

  Kwa kuongezea, Vitamin C inaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Mwili huwa na uwezo wa kujikinga dhidi ya magonjwa madogo madogo kama vile mafua, kikohozi, homa na maambukizi mengine.

  CHANZO CHA MADINI
  Mbali ya kuwa ni chanzo kizuri cha vitamin C, nanasi pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya 'Manganese' ambayo yanaaminika kuwa na uwezo wa kuboresha ufanisi wa vimeng'enyo mbalimbali vya mwili, vikiwemo vya kuzalisha nishati na kinga. Hali kadhalika tunda hili lina kiwango cha kutosha cha Vitamin B1 (Thiamine).

  KUIMARISHA NURU YA MACHO
  Inawezekana karoti ikawa ndiyo inayojulikana na watu wengi kuwa na uwezo wa kuimarisha nuru ya macho lakini nanasi nalo lina uwezo mkubwa wa kuimarisha nuru ya macho. Utafiti unaonesha kuwa ulaji wa tunda hili na matunda mengine, kiasi cha milo mitatu kwa siku, kunaondoa hatari ya kupungua kwa nuru ya macho kwa asilimia 36 kwa watu wazima.

  NANASI BORA
  Nanasi bora ni lile kubwa na lililoiva vizuri. Ni kweli kwamba nanasi kubwa lina nyama nyingi kuliko nanasi dogo lakini hakuna tofauti ya ubora wa virutubisho kati ya nanasi dogo na kubwa, ili mradi lisiwe limeoza au lenye michubuko mingi. Chagua nanasi lilioiva vizuri na lenye kunukia.

  Mara baada ya nanasi kumenywa na kukatwa vipande, linatakiwa kuliwa mara moja, iwapo litahifadhiwa kwenye jokofu kwa ajili ya kuliwa baadaye, njia sahihi ya kuhifadhi ni kuliweka kwenye chombo chenye mfuniko (container). Hii husaidia kuhifadhi virutubisho vyake kwa kipindi cha hadi siku tano bila kupoteza ubora wake, ikiwa pamoja na ladha. Unaweza kula vipande vya nanasi au juisi yake, vyote vina faida.
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu kumbe sio mtaalam wa biashara na uchumi tu kumbe upo full mpaka kwenye afya hongera sana mkuu
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ahsante baba.
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dah asante sana!Nlikua sijui...ila nimefurahi maana napenda sana mananasi!Ngoja niongeze kasi ya kuyala!
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  nashukuru kwa kunifungua macho,hili tunda nilikuwa nalidharau kwa kweli,ngoja nilichangamkie maana huku ndio msimu wake
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Dah kumbe nanasi ni muhimu namna hii!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280

  Kuna uzuri mwingine wa nanasi miye nilikuwa siujui mpaka siku moja katika mtandao mmoja wa Black Amercans mchangiaji mmoja akauliza swali basi jibu lake lilihusiana na nanasi lakini siwezi kuweka hapa nisije kupata kibano bure. Maana hivi vibano vya siku hizi havieleweki kabisa.
   
 8. Chiwaso

  Chiwaso JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,570
  Likes Received: 1,734
  Trophy Points: 280
  Acha woga wewe, jiachie wangu. Ushakuwa mkubwa utaogopa vingapi na mpaka lini?
   
 9. upele

  upele JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poa mkuu be blessed
   
 10. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #10
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh! Elimu haina mwisho. ahsante kwa shule! Huku katani kwetu nanasi moja kubwa ni Tsh 1000.
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Pineapple Juice Benefits

  Pineapple juice has always been a favorite drink among people. Let us see what some of the pineapple juice benefits are:


  [​IMG]

  Tangy-sweet, ridgy crystals and the sinfully rich yellow color! The perfect blend of the tropics and a holiday, wouldn’t you say? I can just see you now – A sun kissed beach and you with a tall glass of chilled pineapple juice, a bright pink drink umbrella and a pineapple wedge adorning the glass. And all that made possible because of a single glass of pineapple juice. Now let’s get one thing straight, you don’t really need a holiday to enjoy a tall glass of pineapple juice, you can do it any which way. In fact, the magic of the pineapple juice is such that it plays magic. You could just close your eyes and sit sipping a glass and voila! You’ll see yourself on a holiday! OK, so the ethereal feel we are done with. Now let’s look at some pineapple juice benefits, shall we? Because of course there are those. Read more on pineapple nutrition facts.

  [​IMG]  Benefits of Pineapple Juice


  There are numerous pineapple juice health benefits for the taking. Pineapple juice tastes good, we know, but it would taste even better if you knew the pineapple juice benefits that came with it and the favor you were doing to your body. So here goes, these are some of the pineapple juice benefits:


  [​IMG]  Rich in Antioxidants


  The pineapple fruit belongs to the bromelain family which is a highly nutritious, protein digesting enzyme. It is also a rich source of vitamin C. Both bromelain and vitamin C are rich in antioxidants which help the body fight against free radicals and help in the overall healing of the body.

  Packed with Nutrients

  Pineapple health benefits include the fact that it is loaded with potassium, calcium, fiber, vitamin C and magnesium (among others). Thus it is packed with varied nutrients that are needed for our health. It is also beneficial for all age groups.

  Promotes Bone Health


  Magnesium that is present in the pineapple juice helps in building of bones and connective tissue. So also, pineapple juice being an excellent source of calcium helps in the strengthening of bones. It therefore promotes and maintains bone health.

  [​IMG]  Aids Digestive System Functioning


  As mentioned earlier, pineapple juice contains bromelain which is responsible for breaking down the protein in our bodies. This helps with effective digestion and is therefore important for the digestive health. In addition to that, pineapple juice also contains fiber which is extremely important to induce regular bowel movements. It is also said that pineapple juice helps with eradicating intestinal worms. Pineapple juice benefits also include the fact that it is a natural diuretic. Which means that it helps to get rid of the excess buildup of toxins and wastes from the kidney and liver.  Improves Immunity

  Pineapple juice strengthens the immune system greatly. Being rich in vitamin C, it helps in preventing the onset of common coughs and colds, sore throats and even severe conditions like bronchitis, thus maintaining a healthy respiratory system.

  Anti-Inflammatory Properties

  Pineapple juice also has anti-inflammatory properties so that it helps to heal infections and wounds better.

  [​IMG]

  Other Benefits

  * It has minimal quantities of fat, sodium and no cholesterol. In that way it is an extremely healthy choice to make for people who are trying to focus on a healthy diet for some weight loss, or maintain an ideal weight.
  * It helps in the smooth functioning of the heart by reducing the occurrence of blood clots in the blood stream.
  * It also has vitamin B1 which is important for converting blood sugar into raw energy.
  * Pineapple juice benefits those people who are suffering from rheumatoid arthritis. It reduces swellings and pains that are a part of arthritis.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2013
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  "Not from Concentrate"
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2013
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu Kizungu tatizo, naomba tafsiri kwa lugha yangu adhimu ya Kiswahili
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280

  NANASI:KINGA DHIDI YA MAGONJWA YA UVIMBE


  Mwili unapokosa kinga imara, huwa katika hatari ya kushambuliwa na kila aina ya magonjwa. Katika orodha hiyo ya magonjwa, yamo pia yale ya kutokwa na uvimbe yakiwemo majipu. Kitaalamu magonjwa haya yanajulikana kama ‘Inflamatory diseases’.


  Katika kukabiliana na matatizo kama hayo, nanasi ni moja kati ya matunda yenye vitamin nyingi na virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuupa kinga mwili wako dhidi ya magonjwa hayo na mengine.

  Siri na umuhimu wa nanasi upo kwenye kirutubisho aina ya ‘Bromelain’ ambacho kinapatikana kwa wingi kwenye tunda hili. Virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa muhimu sana katika kujenga na kuimarisha kinga ya mwili.

  Ukilipa umuhimu na ukiliweka nanasi katika orodha ya matunda unayokula mara kwa mara, utajiepusha na utajipa kinga dhidi ya magonjwa mengi hususan ugonjwa wa kuwashwa na kuvimba koo, ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis) na ugonjwa wa gauti (Gout).

  Ili upate kinga dhidi ya maradhi hayo kwa kula nanasi, unashauriwa kula tunda hilo kabla au baada ya kula mlo wako. Usile nanasi pamoja na chakula kingine kwa wakati mmoja. Kwa kufanya hivyo, virutubisho vitafanya kazi nyingine tofauti na uliyokusudia. Faida nyingine za nanasi ni kama ifuatavyo;

  USAGAJI WA CHAKULA
  Nanasi lina virutubisho vinavyouwezesha mfumo wa usagaji chakula tumboni kufanya kazi yake ipasavyo. Pindi mfumo huu unapowezeshwa kufanya kazi yake vizuri, mtu huweza kupata choo laini na kwa wakati kama inavyotakiwa.

  KINGA YA MWILI
  Nanasi linaaminika pia kuwa miongoni mwa matunda yenye Vitamin C kwa wingi ambayo kazi yake ni kuupa mwili kinga dhidi ya ‘wavamizi’ mbalimbali (free radicals), ambao wanapoingia mwilini, kazi yao huwa ni kuharibu chembembe hai za mwili.

  Kwa kuongezea, Vitamin C inaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Mwili huwa na uwezo wa kujikinga dhidi ya magonjwa madogo madogo kama vile mafua, kikohozi, homa na maambukizi mengine.

  CHANZO CHA MADINI
  Mbali ya kuwa ni chanzo kizuri cha vitamin C, nanasi pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya ‘Manganese’ ambayo yanaaminika kuwa na uwezo wa kuboresha ufanisi wa vimeng’enyo mbalimbali vya mwili, vikiwemo vya kuzalisha nishati na kinga. Hali kadhalika tunda hili lina kiwango cha kutosha cha Vitamin B1 (Thiamine).

  KUIMARISHA NURU YA MACHO
  Inawezekana karoti ikawa ndiyo inayojulikana na watu wengi kuwa na uwezo wa kuimarisha nuru ya macho lakini nanasi nalo lina uwezo mkubwa wa kuimarisha nuru ya macho. Utafiti unaonesha kuwa ulaji wa tunda hili na matunda mengine, kiasi cha milo mitatu kwa siku, kunaondoa hatari ya kupungua kwa nuru ya macho kwa asilimia 36 kwa watu wazima.

  NANASI BORA
  Nanasi bora ni lile kubwa na lililoiva vizuri. Ni kweli kwamba nanasi kubwa lina nyama nyingi kuliko nanasi dogo lakini hakuna tofauti ya ubora wa virutubisho kati ya nanasi dogo na kubwa, ili mradi lisiwe limeoza au lenye michubuko mingi. Chagua nanasi lilioiva vizuri na lenye kunukia.

  Mara baada ya nanasi kumenywa na kukatwa vipande, linatakiwa kuliwa mara moja, iwapo litahifadhiwa kwenye jokofu kwa ajili ya kuliwa baadaye, njia sahihi ya kuhifadhi ni kuliweka kwenye chombo chenye mfuniko (container). Hii husaidia kuhifadhi virutubisho vyake kwa kipindi cha hadi siku tano bila kupoteza ubora wake, ikiwa pamoja na ladha. Unaweza kula vipande vya nanasi au juisi yake, vyote vina faida.

   
 15. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2013
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Badala ya juisi, napenda kupambana na linanasi lenyewe nipate na roughage. Pia kama ni juisi, badala ya kutumia blender na kuongeza maji na sukari, juicer inatoa kinywaji safi kisichohitaji sukari ya ziada. Asante kwa shule.
   
 16. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2013
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,012
  Likes Received: 3,197
  Trophy Points: 280
  Ipi bora, kula nanasi lenyewe au juice yke?
   
 17. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2013
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Hili tunda kila siku asubuhi lazima liwepo kwenye menu yangu
   
Loading...