SoC02 Umuhimu wa Teknolojia kwenye ukuaji wa uchumi

Stories of Change - 2022 Competition

More ideas

Senior Member
Jun 2, 2019
115
89
Salaam wakuu,

Kwenye kichwa cha habari ya mada hapo juu tutaangalia;

1.Utangulizi

Maana ya teknolojia na ukuaji wa uchumi
2. Sekta ambazo zinatumia teknolojia kwenye kukuza uchumi.
3. Hitimisho.

Teknolojia ni matumizi ya sayansi katika kurahisha maisha ya mwanadamu.
Hatuwezi kizungumzia teknolojia pasipo uwepo wa sayansi.
Kutokana na (wikipedia) sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.

Ukuaji wa uchumi(kukua kiuchumi) ni uwezo wa uchumi kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma. Tukija kuangalia maana ya utandawazi ni kukua kwa uchumi, kijamii, kisiasa na kitamaduni kwenye maeneo mbalimbali nchini. Utandawazi ni uthibitisho wa ukuaji wa kiuchumi, mwingiliano kati ya teknolojia na shughuli za kijamii inapelekea uchumi uweze kukua kwa kasi.

Uchumi wa Tanzania umekua kwa 4.9% mwaka 2021 ukilinganisha na 4.8% kwa mwaka 2020. Chanzo Africa development bank (Afdb).

Kuna njia 3 za upimaji wa pato la Taifa nazo ni;

1. Ongezeko la thamani(value added approach)
2. Njia ya matumizi(expenditure approach)
3. Njia ya kipato (income approach)

Teknolojia ina mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi katika sekta mbalimbali nchi, Tunaangalia technolojia imesaidia vipi iyo sekta kwenye kukuza uchumi wa nchi;

Kilimo; Ni moja ya sekta muhimu kwenye nchi mbalimbali duniani kama chanzo cha pato la taifa. Mfano kwa Tanzania ndiyo uti wa mgongo wa nchi imechangia 29.7% kwenye robo ya mwisho ya mwaka 2021 ukilinganisha 20.5% na robo ya mwaka iliyopita ya mwaka huohuo 2021 chanzo (nbs).

Matumizi ya vifaa au zana za kisasa kwenye kilimo kama matractor imekua chachu ya maendeleo ya kilimo nchini kwa kushirikiana na benki ya kilimo Tanzania (TADB), imefadhiri miradi 71 ya kimkakati na kuwawezesha wakulima wadogo wapatao 10,493,370 katika uwapaji wa zana za kisasa za kilimo pamoja na mikopo kwa lengo la kuwainua wakulima ili kuweza kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kupelekea kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Usafirishaji;
Ni sekta muhimu inatumika kama kiunganishi kutoa mzigo au bidhaa na huduma kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.mfano magari, garimoshi, meli, ndege n.k.

Mabadiliko ya mifumo ya magari kutoka kutumia mafuta na kwenda kwenye mifumo ya gas itapunguza gharama za uzalishaji, kupitia miradi ya treni za kutumia umeme utapunguza gharama za za bidhaa kwa mtumiaji pia uwepo wa usafiri wa anga itafungua urahisi wa uingiaji na utokaji wa bidhaa nchini ambayo itatoa soko la uhakika duniani na kujipatia fedha za kigeni na kuweza kukuza uchumi wa nchi.

Viwanda;
Mapinduzi ya viwanda ni moja ya mkakati wa maendeleo ya nchi ya Tanzania, ulianzwa kutekelezwa toka miaka ya 1960s baada ya Tanzania kupata uhuru.

Viwanda vinabadilisha malighafi kwenda kwenye bidhaa lili mtu wa mwisho aweze kutumia, matumizi ya mashine za kisasa zina mchango mkubwa kwenye kuongeza wingi wa uzalishaji wa bidhaa kwa muda mchache. Mfano uwepo wa teknlojia (mashine) ya ukamuaji wa mafuta ya alizeti nchini umewapa uhakika wakulima wa alizeti kwa kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Masoko; Hii ni sehemu ambayo muuzaji na mnunuzi hukutana. Kuongezeka kwa masoko ya mtandaoni kumekuwa na mchango chanya kwenye kusaidia kukuza uchumi wa nchi, Mitandao ya kijamii na majukwaa ambayo yana husiana na masoko mtandaoni imerahisisha uuzaji wa bidhaa sehemu mbalimbali duniani.

Mfano uwepo wa mitandao kama jumia, kikuu, amazon, kupatana, ebay n.k., imepunguza wakati madalali ambayo itamkutanisha muuzaji na mnunuzi wa mwisho inampa motisha mzalishaji wa huduma au bidhaa aweze kuzalisha kwa wingi kwa sababu ya uwepo wa soko la uhakika wa bidhaa na huduma zake.

Huduma za kibenki; Ni sekta muhimu katika utunzaji wa fedha na utoaji wa mikopo kwa wananchi, mifumo ya kimtandao ya kibenki imerahisisha upatikaji wa huduma hiyo sehemu mbalimbali duniani, Huduma kama moneygram, simbanking, mashine za kutolea hela(ATM), credit card na uuzaji wa hati fungani kutoka benki kuu mtandaoni(Treasure bill and bonds) zimekuwa na matokeo chanya kwenye jamii na kupelekea ukuaji wa uchumi nchini.

Afya; Ni sekta muhimu ambayo inahitaji umakini mkubwa, Taifa lenye afya njema (watu) hata uchumi wake unakuwa imara maradufu. Uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya unahitajika kuwepo na mashine za kisasa ambazo zitasaidia wananchi kupata vipimo sahihi ilikupata matibabu ya haraka kabla magonjwa hayajawaathiri.

Mifumo ya bima ni udhihirisho wa uwepo wa teknolojia katika sekta ya afya imerahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wafanyakazi na wanafunzi wa elimu ya juu. Serikali na mashirika binafsi wanatakiwa wajikite kwenye mifumo ya utoaji wa huduma za afya kisasa ili kuweza kuwafikia wagonja wengi kwa muda mchache tuweze kupata nguvu kazi kama taifa kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja.

Ulinzi; Amani na usalama ni chanzo cha uzalishaji wa huduma na bidhaa kuongeza, ukiangalia Taifa kama Congo wana rasiliamali nyingi sana ila wanakosa utulivu kama nchi sababu ya vita na kupelekea wawekezaji kusimamisha au kupunguza shughili za uzalishaji.

Matumizi ya zana za kisasa za kivita na mafunzo imara ya kijeshi itachangia amani ya nchi kuongezeka, uwepo wa amani na utulivu nchini itavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ambapo itaongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma na kusaidia uchumi wa nchi kukua

HITIMISHO; ukuaji wa uchumi unaenda sanjari na ukujuaji wa teknolojia, serikali na mashirika binafsi yanahitajika kuwekeza kwa vijana wenye ndoto za kuwa wanasayansi, kuandaa mazingira rafiki na kuondoa vikwazo kwa wabunifu ili tuweze kupata teknolojia ambazo zitatusaidia kuzitumia kwenye sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wa nchi.

Mwandishi; ABDALLAH A MOHAMMED
Carrier; BSc.ECONOMICS- POPULATION AND DEVELOPMENT
Mawasiliano; 0675227175
#stories of change
# kura kwa mabadiliko
 
Kweli kabisa muhimu kuwekeza katika technolojia .


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa muhimu kuwekeza katika technolojia .


Sent using Jamii Forums mobile app
Muhimu sana ili kuweza kukua kiuchumi kama Taifa na mtu mmojammoja
 
Back
Top Bottom