Umuhimu wa Taarifa: Nini Nafasi ya Watunga Sera, Mahakama na Asasi za Kiraia?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1663743897986.png

NAFASI YA WATUNGA SERA:
1) Kujenga uelewa kwa Umma juu ya Haki ya Faragha na Ulinzi Wa Taarifa

2) Kushirikiana kwa karibu na Wadau wengine kuhusu Masuala ya Kulinda Taarifa

3) Kutengeneza Mifumo ya Kulinda Taarifa kulingana na Sheria na Viwango vya Kimataifa vya Haki Za Binadamu

ASASI ZA KIRAIA

Zina jukumu muhimu katika kuhakikisha Haki ya Faragha inaheshimiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa:

1) Kujenga uelewa mpana wa Haki ya Faragha/Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Jamii na Serikali

2) Kushiriki kikamilifu katika Michakato ya Kisheria inayolenga kupata Sheria itakayolinda Faragha na Taarifa zetu

MAHAKAMA:

Ulinzi wa Taarifa ni muhimu katika Usimamizi wa Haki, na katika hili Mhilimi wa Mahakama unashauriwa:

1) Kuhakikisha Faragha za Wananchi zinazingatiwa na kuheshimiwa

2) Kuweka Misingi imara ili kuimarisha Usimamizi wa Taarifa ndani ya Mahakama

3) Kuwezesha Mafunzo ya Haki ya Faragha na Ulinzi Wa Taarifa katika Mahakama
 
Back
Top Bottom